We sincerely appreciate your feedback, Sis @VwalaViola. Thank you for choosing us.
We look forward to serving you again soon with even more excellence.
📍 Kisonge, Zanzibar
🤙 0774105389
#PembaTaste2026#Organicspice
USIMAMIZI WA BAJETI YA AFYA KULINGANA NA KODI ZA WAKAZI NI UTARATIBU WA KAWAIDA DUNIANI
Katika mjadala unaoendelea kuhusu kauli ya Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, ni muhimu kutenganisha hisia na uhalisia wa usimamizi wa fedha za umma. Hoja iliyotolewa haizungumzii ubaguzi wa wananchi kwa misingi ya uraia, bali inahusu misingi ya kawaida ya upangaji wa bajeti, uwajibikaji wa kifedha na uendelevu wa huduma za afya.
Duniani kote, mifumo ya afya hujengwa na kuendeshwa kwa kutumia kodi na michango ya wakazi wa eneo husika. Kwa sababu hiyo, serikali na taasisi za umma hulazimika kupanga matumizi yao kwa kuzingatia uwezo wa bajeti na idadi ya watu wanaochangia moja kwa moja katika mifumo hiyo.
Muungano wa Ulaya (European Union) ni mfano mzuri. Ingawa raia wa nchi wanachama wana uhuru mkubwa wa kusafiri na kuishi katika nchi mbalimbali za Umoja huo, kila nchi ina mfumo wake wa afya unaofadhiliwa na kodi za wakazi wake. Raia wa Ujerumani hawezi kuhamia Ufaransa na kupata huduma zote za afya bila kufuata taratibu za usajili, bima au makubaliano maalumu ya kikanda. Mfumo huu umewekwa ili kuhakikisha kuwa bajeti ya nchi moja haibebi mzigo usiohusiana na walipa kodi wake.
Nchini Canada na Marekani, mifumo ya afya na huduma za kijamii pia inasimamiwa kwa kiwango kikubwa na majimbo au mikoa. Kila eneo hupanga bajeti yake kwa kuzingatia kodi na michango ya wakazi wake. Mtu anayehama kutoka jimbo moja kwenda jingine hulazimika kufuata taratibu za uhamisho wa huduma hizo ili kuhakikisha uwiano wa kifedha unaendelea kuwepo.
Mfano mwingine ni China na Hong Kong. Ingawa zote ziko chini ya mamlaka ya taifa moja kupitia mfumo wa “Nchi Moja, Mifumo Miwili”, Hong Kong ina mfumo wake wa afya, bajeti yake na utaratibu wake wa utoaji wa huduma za kijamii. Upatikanaji wa baadhi ya huduma za ruzuku hutegemea hadhi ya ukaazi wa Hong Kong na mchango wa wakazi wake katika mfumo huo. Hii ni kwa sababu bajeti ya Hong Kong hupangwa kuhudumia wakazi wake na si idadi yote ya wananchi wa China Bara.
Hata ndani ya Uingereza, ambayo ni dola moja yenye serikali kuu, mifumo ya afya imegatuliwa. England, Scotland, Wales na Northern Ireland zina bajeti tofauti za afya na sera zinazotofautiana katika baadhi ya huduma. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila eneo linapanga matumizi yake kulingana na fedha linazopokea na mahitaji ya wakazi wake.
Kwa mantiki hiyo, hoja ya msingi iliyotolewa Zanzibar ni suala la uwezo wa bajeti na usimamizi wa rasilimali. Bajeti ya Zanzibar hupangwa kwa kuzingatia idadi ya wakazi wake, kiwango cha mapato ya ndani na huduma zinazohitajika kutolewa. Hakuna mfumo wowote wa afya duniani unaoweza kutoa huduma zisizo na kikomo kwa idadi ya watu ambayo haikupangiwa bajeti bila kuwepo utaratibu maalumu wa uchangiaji, bima au makubaliano ya kifedha.
Iwapo kutakuwa na utaratibu wa kitaifa wa kugawana gharama za matibabu, mfuko wa pamoja wa afya, au makubaliano maalumu ya kifedha kati ya pande husika, jambo hilo linaweza kujadiliwa kisera. Hata hivyo, bila kuwepo mfumo huo, kila mamlaka hulazimika kulinda uwezo wa bajeti yake ili kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa wananchi waliopangiwa kuhudumiwa.
Kwa hiyo, mjadala huu unapaswa kueleweka katika muktadha wa usimamizi wa fedha za umma na uendelevu wa huduma za afya. Lengo si kuwabagua Watanzania, bali kuhakikisha kwamba rasilimali zilizopo zinatumika kwa uwajibikaji, kwa kuzingatia uwezo wa bajeti na mchango wa walipa kodi wanaofadhili mfumo husika.
Masuala ya afya, kodi na bajeti ni masuala ya hesabu, mipango na utawala. Yanahitaji mjadala wa hoja, takwimu na sera, badala ya mihemko ambayo inaweza kupotosha uelewa wa jambo lenyewe.
Tandoori Masala ya Pemba Taste Products huifanya harufu na ladha ya kuku kuwa mtego usioepukika.
📍Kisonge, Zanzibar
🤙 0774105389
#PembaTaste2026#Organicspice
Pemba Taste Products wishes you and your family a blessed Eid Al Adha Mubarak! 🌙✨
May this special occasion bring peace, happiness, good health, and abundant blessings to your home. Eid Mubarak!
#PembaTaste2026#EidAlAdha2026
Tandoori Masala by Pemba Taste Products. A premium blend of natural spices crafted for rich aroma, vibrant color, and authentic taste. Perfect for chicken, meat, and fish.
Quality you can trust.
📍 Kisonge, Behind House No. 5.
📞 +255 774 105 389
#PembaTaste2026#Spiceshop
Is your daily tea missing something? ☕
Pemba Taste Tea Masala is crafted from natural spices sourced in Zanzibar, bringing rich aroma, bold flavor, and natural warmth to every cup.
One sip and you’ll taste the difference.
🤙 0774105389
#PembaTaste2026#Spiceshop
Je, jikoni kwako kuna spice za Pemba Taste Products? 🌿
Kama bado, huu ndio muda sahihi wa kubadilisha ladha ya mapishi yako.
Viungo vyetu ni organic, safi na vya asili, vinavyokupa ladha halisi na ubora unaoaminika.
#PembaTaste2026#spiceshop
Health Benefits of Turmeric.
• Helps reduce inflammation and body pain
• Boosts the immune system
• Aids in detoxifying the body
• Promotes liver health
• Helps regulate blood sugar levels
• Improves skin health and natural glow
🍃Organic & chemical-free.
#PembaTaste2026
Pemba Taste Herbal Tea Supports healthy cholesterol levels, helps detoxify the body, and naturally boosts fat burning for overall wellness.
Carefully crafted from pure medicinal herbs and spices grown in Zanzibar.
A refined taste of natural health in every ☕
#PembaTaste2026
Pemba Taste Products tunajivunia kushiriki mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika 29 na 30/ 01/2026 chini ya programu ya Ajira YE2 kwa CRDB Bank Foundation & GIZ (WE4D).
Pemba Taste Products
Tunaendelea kujifunza, kukua na kuinua bidhaa za asili kutoka Zanzibar.
#PembaTaste2026