Klabu ya Simba imetangaza kumtambulisha aliyekuwa kocha msaidizi, Juma Mgunda kuwa mwalimu wa program maalum kwenye maeneo mbalimbali ya timu za vijana, wanawake na senior team kwa ajili ya kuisambaza falsafa ya Simba kwenye maeneo hayo.
Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Imani Kajula amesema Mgunda atakuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya vijana chini ya miaka 17 na 20, timu ya wanawake na senior team.
"Niwaambie wazi kuwa mwalimu Mguda sasa hivi tunamtumia kwa program maalum, kwa hiyo mtamuona kwenye maeneo mengi sana.
"Tutamtumia kama mwalimu ambaye anazunguka kwenye timu zetu zote [U17, U20, Simba Queens na Simba senior team]."
"Klabu yoyote kubwa huwa na mwalimu ambaye anafanya kazi zaidi ya moja kwa sababu lazima zile falsafa za timu zianzie kwenye timu za vijana hadi timu ya wakubwa lakini pia hata timu ya wanawake."
Mgunda alijiunga Simba SC mnamo Septemba 2022 kama kocha wa muda akitokea Coastal Union, na baadaye aliteuliwa kuwa kocha msaidizi baada ya ujio wa kocha mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’.
#KitengeSports