#HuyuAnatakiwaAlipweFedhaNyingi
Mara nyingi nakutana na waandishi wakongwe na mara zote huambiwa siku hizi waandishi hakuna. Lakini, huyu dogo Baraka Adson Mpenja @BarakaMpenja anatutoa kimasomaso wengi. Baraka anawapa watu sababu ya kuangalia mechi ya Namungo na Biashara Musoma
🔥🙌🙌SAKATA LA BERNARD MORRISON.......
.
Kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti Elias Mwanjala, kimemalizika jioni hii ya leo, lakini hakuna maamuzi yoyote rasmi yaliyotangazwa.
"Nilikuwa nasoma chuo kikuu cha DSM kuanzia mwaka 2011 hadi 2014, nilikuwa nimetoka kijijini Itete mkoani Mbeya shule ndiyo ilinileta huku, nilivyotoka chuo moja kwa moja nikaenda @azamtvtz, nilikuwa nimejiandaa"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka
"Kikubwa ninachokifanya mimi ni utofauti wa sanaa ya maneno na kuyaleta maneno ya mtaani kwenye mpira, nikitupa maneno na misemo ya kimtaani mtu anafurahi kukusikiliza"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka
"Wakati nipo shule ya msingi Baba yangu alikuwa anpenda sana mpira, alikuwa akiwekaga redio yake kusikiliza matangazo ya mpira wote tunakuwa kimya, mimi nilikuwa napenda sana kutangaza na nimeishi kwenye ndoto zangu"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka
"Kwangu ninachojivunia kikubwa ni kazi tu, kupata marafiki na kufahamiana na watu wengi, mzee wangu alikuwa ananiambia ukiwa na kipaji sio cha peke yako bali ni kwa ajili ya watu wengine na napenda sana kukosolewa"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka
"Kazi ya mtangazaji kwenye mpira ni kusherehesha matukio ya mechi, mtangazji lazima uwe sehemu ya timu iliyoshida, mimi naenda kwa matukio, shutuma za kuwa mshabiki wa @SimbaSCTanzania zilianza kwenye mechi ya Simba na Nkana"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka
"Shutuma nimezisikia mambo kuwekeana na kupuliziana dawa za kunyongesha mtu nina uhakika zinafanywa ila sijaona kwa macho yangu, ila kuchinja paka na kondoo nimeshaona hata pale Taifa nimeona ila siwezi kutaja ni timu gani maana zina fitina"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown
"Kuna wakati mimi naambiwa ni shabiki wa @SimbaSCTanzania kuna wakati naambiwa mimi ni Yanga ila timu ninayoipenda tangu nikiwa mdogo ni Tukuyu Stars wale ndiyo wana Koma Kumwanya orijino sio hawa Mbeya City"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka
"Mimi nimeoa mwaka 2016 ila sijajaaliwa watoto, Mke wangu nilikutana naye shule, nilimfukuzia akasema haamini wanaume waongo ila nikamwambia nitamuoa, nilimpatia kwenye kuvuka maana alikuwa muoga sana kuvuka barabara"
@BarakaMpenja@ecejay@yahstonetown#SalamaNaBaraka