MISSION NGUMU ILIYODHIHIRISHA UBABE WA RWANDA AFRIKA
Zaidi leo tutazungumzia tukio lililoacha midomo wazi watu wengi kwenye tasnia ya kivita na intelijensia duniani kiasi inatumika kama Case study kwenye vyuo vya kijeshi duniani.
Mwaka 1996 DRC iliokuwa chini ya utawala wa Mobutu sese seko uliingia kwenye vita kali baada ya Marais Watutsi Paul kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda kumuunga mkono (kumtumia) kiongozi wa waasi huko DRC Laurent Kabila ili kuipindua serikali ya Mobutu.
Kiufupi tu baada ya vita ya kimbari 1994, majeshi ya kihutu yaliyopinduliwa yalikimbilia Mashariki ya DRC. Hivyo utawala wa kagame uliona kma watapinduliwa saa yoyote kma hawatowateketeza mapema. Kilichotokea ni Rwanda kuvamia makambi ya wahutu na kuwateketeza na waliokimbilia Katikati ya DRC walifuatwa hadi huko na ndipo Mobutu akatoa order ya wavamizi hao kushughulikiwa hivyo vita ikabadilika malengo kutoka kuwamaliza waasi wa kihutu hadi kumpindua Mobutu.
Kufikia May 1997 Majeshi hayo ya wa Tutsi yalifanikiwa kuondoa utawala wa Mobutu ambaye alifariki muda mfupi baadae huko Morocco. Utawala mpya uliowekwa na watutsi ulishuhudia Rais Laurent Kabila akiteua wanyarwanda kwenye nafasi nyeti za serikali kama kulipa fadhila kwa majeshi hayo ya kigeni.
Lakini!! Ulipofika mwaka 1998 Kabila akaona hana kabisa mamlaka na utawala wake maana maamuzi yote mazito yanafanyika Kigali. Ukizingatia Mkuu wa majeshi ya DRC alikua mnyarwanda pure Gen James Kabarebe hivyo unaweza ona alivyopokwa ushawishi wa kiutawala.
Mnamo july 13,1998 Kabila akaamua kutimua wanyarwanda na waganda wote kwenye serikali yake na kufikia tarehe 27 alitoa amri kuwa masalia wote wa kitutsi waondoke nchini mwake lasi hivyo watatolewa kwa nguvu.
Kigali yajibu mapigo
Kiburi hiki kiliwakera sana serikali za kitutsi (Rwanda na Uganda, pia Burundi) hivyo wakadhamiria kumtoa madarakani ili waweke kibaraka mwingine atakayelinda maslahi yao. Ndipo ikaamriwa kuwa Gen James kabarebe aongoze kikosi cha makomandoo cha kuiteka kinshasa na kumpindua Rais Kabila kwa spidi na ufanisi wa hali ya juu.
Ikumbukwe Jiografia ya DRC sio rafiki sana kwa logistics za kivita maana ni nchi kubwa sana iliojaa misitu na mito, na miundombinu ya usafirishaji ni migumu mnoo hivyo majeshi yakitoka Rwanda yatachukua miezi zaidi ya 6 kufika Azma yao ya Kinshasa.
Kwa kutathmini hili ikapangwa moja ya operation nzito katika historia ya Afrika ilioitwa Operation kitona ambayo ilikua na mpango wa kufikisha majeshi kwenye kitovu cha congo yaani Kinshasa kwa spidi ya mwanga wa radi na kumaliza mission yao haraka.
Operation Kitona
August 1998, wakitumia ndege za kiraia kabisa Boeing 727 walitua katika uwanja wa ndege wa kitona pembezoni na jiji la kinshasa kwa usiri mkubwa na kuweza kuteka uwanja wa ndege na kufanikisha majeshi zaidi kufika hapo kujiandaa na uvamizi.
Mpango ni kuwa wakiteka jimbo maalum zaidi la Bas Congo (kwa sasa Congo Central) ambalo lina bandari na umeme mkubwa wa nchi unazalishwa pale basi ingekuwa ameparalayse nguvu yote ya serikali kujiendesha.
wakiwa na askari 800 pekee waliopo Katikati ya congo zaidi ya Km 1000 kutoka nyumbani kwao walianza safari ya kuuteka mji wa kinshasa na ikumbukwe kutoka Kitona hadi Kinshasa ni km 320 na ndani ya siku 5 walikuwa wamefika kinshasa!!
Serikali ya kabila ikapatwa na shock kwa ''spidi ya umeme'' ya watutsi ikabidi aombe msaada kwa majirani.
Ikumbukwe Kwenye 1st congo war ya kumtoa mobutu Angola ilisaidia majeshi ya Rwanda maana mobutu alikuwa akisupport majeshi ya waasi wa Angola UNITA chini ya jonas savimbi. Hivyo Rwanda walitegemea kupata support tena ya Angola, lakini ambacho walisahau ni kwamba maadam maslahi ya Angola yaani waasi wa UNITA walikua hawana support tena ya DRC hawakuwa na haja ya kumtoa kabila na ndio hapa vita ikapata sura mpya kabisa iliobadili historia.
Mnamo agost 22 majeshi ya Angola,zimbabwe na Namibia yaliingia kwenye uwanja wa vita kupitia kusini mwa kinshasa hivyo majeshi ya watutsi 800 (yaliyoongezwa nguvu na askari