Tunamshukuru sana mdau huyu! Ni kweli wapo madaktari wengi na wataalam wengine wa afya wazuri, wanaojituma na kuwajibika mno katika Hospitali zetu za umma. Tunapaswa kuwatia moyo. Hakika ujumbe huu unatia moyo na kujenga ari ya kujituma kwa madaktari wetu. Tunakushukuru sana.
Hii ndio sekta ya Afya tunayopambana kuijenga awamu hii ya Rais mwenye maono Dkt @SuluhuSamia ambapo kipaumbele chetu ni #UboraWaHuduma tukiweka mkazo kwenye
1. Weledi, Maadili na Kujituma kwa Wataalam
2. Upatikanaji wa Huduma kwa wakati
3. Urahisi wa Rufaa inapolazimika
4. Gharama Zinazohimilika
5. Huduma bora kwa wateja ikiwemo lugha nzuri na ya upendo kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.
Kipekee, ninawapongeza wataalamu wote waliohusika kuhudumia wagonjwa siku hii ktk Hospitali ya Mwananyamala na Taasisi ya Mifupa MOI hadi kuvutia mrejesho chanya kutoka kwa jamii. Asanteni sana sana sana. Mungu awabariki @TaasisiyaMifupa #MwananyamalaRRH #HRMMwananyamala
@antonioguterres@UN_HRC I really love this kind of thoughts, mentality and visions of you and UNHCR, that are actually focused to serve the humans regardless of the surrounding environmental.