Biashara Tz ni jukwaa la habari na taarifa za biashara, uchumi, uwekezaji na fursa za kibiashara nchini Tanzania na Afrika. Tunawaletea wasomaji habari, uchambu
Changamoto ya Wafanyabiashara wageni kufanya kazi za Watanzania kutatuliwa.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo ameunda Timu ya watu 15 kwa ajili ya kufuatilia changamoto inayowakumba wafanyabiashara wa Kariakoo ya wawekezaji wageni wanaokuja nchini na ajenda ya uwekezaji kinyume chake wanajishughulisha na biashara za rejereja (Wamachinga) na kuathiri uchumi wa wafanyabiashara wazawa.
Dkt. Jafo alitangaza Timu hiyo Februari 02,2025 jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo ambapo kuhusu utatuzi wa Changamoto mbalimbali zilizopo katika Soko hili ili kuliwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Dkt Jafo alifafanua kuwa Timu hiyo inayojumuisha wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi itafanya kazi kwa siku 30 na itaanza kazi hivi karibuni ikiongozwa na Mwenyekiti wao Edda Tandi Luoga Mkuu wa Chuo cha Elimu ya biashara (CBE)
Aidha, Dkt. Jafo akieleza majukumu ya timu hiyo amesema Timu hiyo inatakiwa kufanya utafiti kwa kina kwa soko la kariakoo, kubaini ukubwa wa tazizo la wageni kupewa vibali na leseni za kufanya biashara nchini zinazoweza kufanywa na watanzania, kuchambua uhalali wa vibali na leseni zilizotolewa kwa wafanyabiashara wageni.
Aidha Dkt Jafo amesema Timu hiyo itafanya kazi ya kubaini sekta na aina ya biashara na maeneo yenye changamoto kwa wageni hapa nchini, kuchunguza utaratibu na upatikanaji wa nyumba za kufanyia biashara kwa wageni, kuchunguza udhaifu wa mfumo na uwezekano wa wageni kutumia njia zisizo rasmi kufanya biashara hapa nchini,
Aidha, Timu hiyo inatakiwa kutoa mapendekezo ya hatua za haraka zitakazoweza kuchukuliwa na taasisi katika kudhibiti wageni wanaoingia kufanya biashara na ajira zinazostahili kufanywa na Watanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera akizungumza akitoa salamu kabla ya kumkaribisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo(Mb) kuzungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo Februari 02, 2025 jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara Ndg. Sempeho Manongi akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo kushiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lenye kaulimbiu βkuongeza ushiriki wa Tanzania katika Biashara na Uwekezaji Kikanda na Kimataifaβ lililofanyika Jijini Dar es Salaam, Januari 31,2025.
Jukwaa hilo limelenga kujadili sera, mipango na mikakati itakayoweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania kukamatia fursa za kimasoko na uwekezaji zilizopo nje ya mipaka ya Tanzania.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaohusu nishati unaofanyika Januari 27 na 28, 2025 katika Kituo cha Kimatalfa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe amesema ni muhimu kuongeza ufanyaji biashara kati ya Tanzania na Misri kwa kuwa Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara
Aidha, amewakribisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Alexandria Misri kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji.
Kigahe ameyasema hayo Januari 27, 2025 wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Misri na Tanzania linalofanyika katika Chemba ya Biashara ya Alexandria jiji la Alexandria, Misri.
Kongamano hilo limehudhuriwa na Wawekezaji na Wafanyabishara wa jiji hilo, Viongozi na Wanachama wa Chemba ya Biashara ya Alexandria pamoja na ujumbe wa Tanzania kutoka Taasisi za umma na binafsi.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe ameongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Misri na Tanzania kutembelea Kongani ya Viwanda vya kuchakata mazao la SILO FOODS for Food Industries katika Mji wa Sadat nchini Misri Januari 26, 2025
Viwanda hivyo vinajishughulisha na uchakataji wa mazao kama ufuta, ngano na maziwa na kisha kuzalisha bidhaa mbalimbali za vyakula kama vile Unga wa ngano, Snacks, Biskuti, Tambi, Pasta, Chocolate, Mikate, Maziwa, Yoghurt, n.k.
Aidha, kabla ya kutembelea viwanda hivyo, ujumbe huo ulitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi wa ILMONTE katika eneo la Galala, Sokhna Misri.
Lengo la ziara hizo ni kujufunza, kubadiloshana uzoefu pamoja na kuwahamasisha wawekezaji kutoka Misri kuja kuwekeza Tanzania.
Katika Ziara hiyo, Mhe. Kigahe aliambatana na Mhe. Balozi Richard Makanzo ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dkt. Stephen Nindi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo pamoja na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania.
Kongamano la Biashara na Uwekeza kati ya Misri na Tanzania linafanyika nchini Misri kuanzia tarehe 23/1/25 hadi tarehe 1/2/25 katika miji ya Cairo, Alexandria na Aswan.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC), Prof. Valerian Silayo akiapa kiapo cha Maadili cha Utumishi wa Umma. Ameapa kiapo hicho mbele ya Kaimu Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini, Bw. Tumaini Mgalla Januari 24, 2025 Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC), Prof. Valerian Silayo akiapa kiapo cha Maadili cha Utumishi wa Umma. Ameapa kiapo hicho mbele ya Kaimu Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini, Bw. Tumaini Mgalla Januari 24, 2025 Jijini Arusha.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. NeedPeace Wambuya alipowasili katika ofisi za Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini- CAMARTEC Januari 24, 2025 jijini Arusha.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Selemani Jafo ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kuleta mabadiliko zaidi katika uzalishaji na udhibiti wa zana za kilimo zinazoingia kutoka nje ya nchi ikiwemo kutopata hati chafu sanjari na matumizi sahihi ya fedha.
Waziri Jafo ameyasema hayo Januari 24, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa CAMARTEC, Jijini Arusha ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo kula kiapo cha Maadili.
Alisisitiza Bodi hiyo kusimamia vema kazi za kituo hicho ikiwemo kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuhakikisha zana za kilimo zinawafikia wananchi wengi hususani wakulima ili waweze kuwa na matumizi sahihi ya zana za kilimo na vema ili kuhakikisha CAMARTEC inapata maendeleo.
Vilevile Dkt Jafo ameishauri Bodi hiyo kuendelea kutoa ushauri ikiwemo kusimamia Menejinenti na Wajumbe wake kufanya kazi kwa upendo na nidhamu kazini ili kuhakikisha wanaleta tija katika kituo hicho ili kuhakikisha wanatoa matunda bora.
Vilevike Dkt Jafo ameziagiza Taasisi zote zilizochini ya Wizara yake ikiwemo CAMARTEC kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kiweze kutejeleza majukumu yake ipasavyo katika kuelimisha umma kuhusu jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta ya viwanda na biashara.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt,Hashil Abdalah amesema anaamini Bodi hiyo itasimamia kwa ukamilifu tafiti na majaribio ya teknolojia kwa ajili ya zana za kilimo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchini
Akisoma taarifa ya kituo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama amesema Kituo hicho kimefanikiwa kuunda zana mpya 42 zinazozalisha zana mbalimbali kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya CAMARTEC, Profesa Valerian Silayo alisema Bodi hiyo imepokea maelekezo yote yaliyitolewa na iko tayari kuyafanyia kazi ili kuhakikisha CAMARTEC inafikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kusaidiwa upatikanaji wa fedha za kuendesha kituo hicho kwa wakati