Mwanariadha nyota wa Tanzania wa mbio za Marathon, Gabriel Geay, amevuna kiasi cha Shilingi milioni 30 baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za Berlin Marathon zilizofanyika leo, Jumapili, Septemba 27, 2026, nchini Ujerumani.
Geay amemaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 2:03:59, huku ushindi ukienda kwa Adola Guye wa Ethiopia, aliyemaliza kwa muda wa saa 2:02:50.
Nafasi ya pili imeshikwa na Muethiopia mwenzake, Diriba Dida, aliyetumia muda wa saa 2:03:19.
Kwa mujibu wa zawadi za mashindano hayo, Guye ataondoka na kitita cha Euro 30,000, sawa na takribani Sh91 milioni, huku Dida akipata Euro 20,000, sawa na takribani Sh60 milioni.
Kwa upande wa wanawake, Morocco imeibuka kidedea baada ya mwanariadha wake, Zeroual Oussama, kushinda mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 2:10:09.
Tendai Zimuto wa Zimbabwe amemaliza katika nafasi ya pili baada ya kutumia muda wa saa 2:10:27, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Erick Sang wa Kenya, aliyemaliza kwa muda wa saa 2:10:31.
#KitengeSports
"kwanza niwashukuru Watanzania Kwa kunichangia, hao ni watu mhimu sana, halafu pili niwashukuru Madee, Babu Tale na Fid Q Kwa Kunilipia faini.
Hii milioni tatu ambayo nilipanga Kulipa faini, nitampelekea Baba yake na Banana Zoro, Mzee zahir Zoro mgonjwa wa Muda mrefu, pia ndugu yangu prof Jay ambaye pia ni mgonjwa wa Muda mrefu, pia mama yangu mzazi naye ni mgonjwa wa Muda mrefu sana, wote nita wakabidhi Milion Moja Moja, hiyo ndo sadaka yangu"
🗣️ Amesema Dudu Baya
Sasa yule Suma mnazeleti aliye sema Dudu Baya katapeli sura yake ataificha wapi?
Shabiki maarufu wa Klabu ya Yanga, Mzee Mpili amefariki dunia usiku huu huko Ikwiriri, Rufiji.
Mzee mpili alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mgongo, kiuno na magonjwa ya uzee.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa na familia ya wana Yanga.🕊️🕊️
#RIP🕯️ MZEE MPILI
Kaallu inna lillah wainna illah raaj uun
#KitengeUpdates
#HABARI Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakiwa tayari Mhakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuendelea kufuatilia majumuisho ya kesi ya Uhaini inayomkabili mwenyekiti wao Tundu Lissu.
#EastAfrivaTv#TogetherTunawakilisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha azma ya Tanzania kufikisha thamani ya uchumi wa Taifa hadi dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Septemba 27, 2026 Jijini Doha, Qatar alipokutana na Makamu wa Kwanza wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda cha Qatar (QCCI), Mohammed bin Ahmed bin Twar Al Kuwari pamoja na ujumbe wake.
“Tunaamini kwamba Serikali peke yake haiwezi kufanikiwa katika uwekezaji huo bila kushirikisha wawekezaji wa ndani au wa nje, ndiyo maana Serikali imeweka vivutio vya kiuwekezaji ili kuvutia mitaji,” amesema Dkt. Mwigulu.
Katika kikao hicho, Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya uchumi na uwekezaji, pamoja na kuainisha fursa zilizopo Tanzania na Qatar, pamoja na fursa zinazotokana na ushiriki wa Nchi hizo katika jumuiya za kikanda za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Kiarabu za Ghuba (GCC).
#MillardAyoUPDATED
On December 6, U.S. equities take their biggest step yet toward an always-on market.
Nasdaq will introduce a new trading session from 9:00 p.m. to 4:00 a.m. ET — creating 23/5 trading: 23 hours of continuous markets, five days a week. 🧵
Zahanati ya Iganduka iliyopo Kata ya Msia, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeezuliwa sehemu ya paa kufuatia upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha jana, Septemba 27, 2026.
Kwa mujibu wa Mashuhuda, upepo huo uliibuka ghafla na kusababisha madhara katika zahanati hiyo pamoja na nyumba za baadhi ya Wananchi.
Miongoni mwa Wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa ni Vale Mosses Mwilenga, Jakaya Tulyanje na Abed Pazza.
Diwani wa Kata ya Msia, Godwell Mgalle, ametembelea Zahanati hiyo na kujionea madhara yaliyosababishwa na upepo huo.
Mgalle amesema Zahanati ya Iganduka ni miongoni mwa Zahanati zinazotegemewa na Wananchi wa kata hiyo kupata huduma za afya, hivyo ameiomba Serikali pamoja na Wadau mbalimbali kushirikiana kuirejesha katika hali yake ili Wananchi waendelee kupata huduma katika mazingira salama.
Aidha, Mgalle ametoa pole kwa Wananchi ambao nyumba zao zimeathiriwa na upepo huo, huku akisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa hatua za haraka kuwasaidia waathirika.
#MillardAyoUPDATES
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi amezitaka Taasisi na Mashirika ya Umma kupunguza baadhi ya matumizi na kuelekeza fedha katika kuwajengea uzoefu Vijana wanaohitimu vyuo ili kuwaandaa kuingia katika soko la ajira.
Akizungumza leo, Septemba 28, 2026, katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) Jijini Arusha, Ndejembi ametolea mfano uwezekano wa kuchukua Vijana 10,000 na kuwapeleka kupata uzoefu katika Taasisi mbalimbali za umma, ikiwemo TANESCO, TPA na TANROADS, akisema mpango huo unaweza kugharimu takribani shilingi bilioni 120.
Amesema fedha hizo zinaweza kupatikana endapo Taasisi za Umma zitajipanga na kupunguza baadhi ya matumizi, ikiwemo posho za vikao, safari na ziara za mafunzo nje ya Nchi.
“Kama tunaweza kulipana posho za vikao, safari, kwenda study tour nje na kadhalika, tukawa tunaweza kujiminya, tukakata spending yetu, tunaipata bilioni 120 ya kuweza kusaidia Taifa letu, kuweza kuwainua Vijana wetu,” amesema Ndejembi.
kutazama video bonyeza link hii——————>
https://t.co/9C8Q6axPAe
#MillardAyoUPDATES
#HABARI Baadhi ya wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Mtwara wamehoji wananchi wa mkoa huo kutonufaika ipasavyo na gesi asilia inayozalishwa mkoani humo, huku nyumba 125 pekee zikiwa zimeunganishwa na huduma hiyo hadi sasa.
Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mtwara, ambapo wabunge hao wameshangazwa na idadi hiyo ikilinganishwa na Dar es Salaam, ambako zaidi ya nyumba 1,000 zimeunganishwa na gesi kwa ajili ya kupikia.
Akijibu hoja hiyo, Afisa Maendeleo wa TPDC, Ally Mruge, amesema shirika hilo kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), limeanza kufanya tathmini katika maeneo ya vijijini kwa lengo la kuanza kusambaza gesi asilia kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amemtaka Afisa Maendeleo ya Jamii wa TPDC kuwasilisha mpango kazi wa shirika hilo na utekelezaji wake, ili utumike kama rejea katika kuiandikia Wizara ya Nishati kuhusu uhitaji wa wananchi kuunganishiwa gesi majumbani.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha