Neno urafiki na unafiki ni maneno yanayoshabihiana sana, na tofauti zake zinatofautishwa na herufi moja tu pekee. kwaiyo wakati unatengeneza urafiki kumbuka pia umetengeneza unafiki ila tofauti ni aina ya mtu ambaye unatengeneza naye.
Kuna wale watu wana taarifa zako kuliko unavojifahamu mwenyewe,wape nafasi za kazi ofisini kwako ili kuwapunguzia gharama za udadisi na usambazaji taarifa zako kitaifa na kimataifa .
Kuna watu Mungu anawaondoa katika maisha yako alafu unabaki na huzuni,maumivu na uchungu usio wa kawaida kwa kua kusudi la Mungu ni kubwa.watu hao huenda ndio wange kupa machungu maumivu, na mateso yasiyo kawaida katika maisha yako
Wakumbushe maadui zako kwamba zile chuki , unafiki na fitina vimechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yako. kwaiyo waungane na maadui wengine waliobakia ili kufanikisha mafanikio yako kwa urahisi zaidi
Maisha ni usafiri ambapo kila anayeianza safari anajua anapotaka kushuka maamuzi yapo kwako msafiri. kusinzia upitishwe kituo,kua macho ushuke unapotaka kushuka au kuona unapotakiwa kushuka na kuaihirisha kituo.....
Usipende kuwaaminisha watu uhalisia wa maisha yako acha wajionee wenyewe
Kuna watu kwenye maisha wapo macho kila unapofungua mlango wako kuelekea mishe mishe zako
Na wao wanafungua milango yao kuangalia je? kweli ni wewe au ni mgeni kalala kwako .