Nyota wa Muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz (@diamondplatnumz) amewasilisha mapendekezo ya kuomba Wimbo wake wa Komasava uchaguliwe kuwania vipengele viwili katika tuzo maarufu Duniani za Grammy Awards zinazotarajiwa kufanyika Jumapili, Februari 02, 2025 huko https://t.co/YXJUjOBOa6 Arena, Los Angeles, Marekani.
Kupitia taarifa iliyotolewa na lebo ya Msanii huyo, WCB Wasafi (@wcb_wasafi) imeeleza “tunajisikia fahari kutangaza kuwa Msanii wetu mwenyewe amewasilisha mapendekezo mawili katika tuzo za Grammy, Video bora ya Muziki na Mtumbuizaji bora wa Muziki Afrika.” taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa lebo hiyo imeeleza.
Aidha lebo hiyo imewaomba Watanzania kumuunga mkono Msanii huyo bora barani Afrika ili kufanikisha ndoto yake ya kuweka historia na kutangaza sauti na kipaji chake cha kipekee Ulimwenguni kote kupitia Muziki anaofanya, kura za Wanachama wa Grammy ni muhimu kumfanya Platnumz kuchaguliwa kuwania tuzo hizo.
Wanachama wa kupiga kura za Grammy ni Wasanii, Watunzi wa Nyimbo, Waandishi, Watayarishaji wa Muziki, na wengineo wengi wanaofanya kazi katika tasnia ya Muziki Duniani wanaotambulika na Waandaji wa tuzo hizo (Recording Academy), 66% ni Wanaume, 49% ni Wazungu na 66% ni wenye umri zaidi ya miaka 40.
Wanaowania tuzo hizo wanatarajiwa kutajwa Novemba 08, 2024, zoezi la kupiga kura litaanza Disemba 12, 2024 hadi Januari 03, 2025 kabla ya hafla ya utolewaji wa tuzo hizo ambayo ni Februari 02, 2025, Wasanii wa Nigeria walioripotiwa kuwasilisha kazi zao ni kama vile Ayra Starr, Tems, Asake na Burna Boy.
#MillardAyoENT