Kuwa mwanaume anayeweza
1. Kusimama baada ya kuachwa
2. Kupoteza ajira.
3. Kustahimili usaliti,
4. Kukubali kufeli na Kupoteza kila kitu alichonacho
Na BADO akasimama kidete na kusema, ' Sitokata Tamaa Nitapambana na nitashinda
Kama wewe ni kijana wa miaka 20 hadi 40 na unataka kuona mabadiliko na mafanikio ya kweli mwaka huu wa 2026, huu ni ujumbe wangu kwako.
Nimejifunza mambo haya kwa vitendo, na nataka nikupe ukweli ambao ukishika, hutabaki pale ulipo.
Usijishauri mara mbili kufanya haya mambo 12 kuanzia sasa hivi:🧵
BRO TO BRO
Usikate tamaa haijalishi unapitia kipindi kigumu kiasi gani Usiogope kuanza upya kila unapoanguka. Jipe Moyo kwamba na kujiambia maneno haya "hapa ndipo nguvu yangu inapojengwa nitasimama tena"
Weka focus yako mbele, Badilisha mindset yako, Toka kwenye Comfort zone yako. Amini mchakato hata kama unaenda polepole.
Weka tumaini lako kwa MUNGU Hakika utainuka 💪
BRO TO BRO
Haijalishi unapitia wakati gani katika maisha Usikate tamaa bro
Ili mradi bado unaishi. Basi mapambano lazima yaendelee
Bado una muda.
Bado una pumzi
Bado una nafasi ya kubadilisha mambo.
Mwanaume wa kweli hakimbii changamoto anajifunza kuhimili na kuzoea mikikimikiki.
Anaweza kuanguka, anaweza kuumia, lakini anainuka tena akiwa imara na mwenye nguvu zaidi.
Siku zote Hadithi ya mwanaume haimaliziki pale maisha yanapokuwa magumu mara nyingi hapo ndipo safari yake halisi inapokuwa inaanza.
Inuka tena, Jipange upya na Endelea kupambana. 💪
MAKOSA 17 YA KAWAIDA AMBAYO MWANAUME MWENYE AKILI HAPASWI KUFANYA.
1. Usifanye maamuzi ukiwa na hasira kali au maumivu ya moyo.
2. Usishiriki mipango yako mikubwa na kila mtu.
3. Usipuuzie afya yako kwa sababu ya kazi au pesa.
4. Usikopeshe pesa ambayo huwezi kuhimili kupoteza.
5. Usikae mahali ambapo huthaminiwi.
6. Usikimbilie mahusiano kwa sababu ya upweke.
7. Usipuuze ishara za hatari (red flags) mapema.
8. Usijifananishe na mafanikio ya wengine.
9. Usivunje ahadi bila sababu ya msingi.
10. Usifanye mambo makubwa bila mpango au akiba.
11. Usipoteze muda mwingi na watu wasiokuongeza thamani.
12. Usikimbie wajibu wako kama mwanaume.
13. Usisahau kujiheshimu, hata kama dunia haikupigii makofi.
14.Usifanye ngono bila kinga na mtu ambaye huna umuamini
15. Usisaini nyaraka yoyote kama hujaisoma na kuielewa vizuri
16. Usimtembelee mtu bila taarifa, isipokuwa kama ni dharura
17. Ukiwa sehemu yenye mkusanyiko wa watu wengi iwe Bar, Mgahawani au kwenye sherehe, usiondoe macho yako kwenye chakula au kinywaji chako