Katibu Mkuu @ccm_tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika 18-19/1/2025
KATIBU Mkuu wa @ccm_tanzania, Balozi @nchimbie Nchimbi akipokelewa Wilaya ya Nzega, tarehe 20/12/2024. Kabla ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Jimbo la Nzega mjini,Amezindua ukumbi wa mikutano unaomilikiwa na CCM (W) Nzega, wenye uwezo wa kutumiwa na watu takribani 1,500 - 1,900.
Katibu Mkuu wa (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Tabora 19/12/2024 kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Tabora, na kupokelewa na wenyeji wake, waliiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Said Juma Nkumba.
Usiku wa kuamkia leo Desemba 18 2024 tumepoteza ndugu zetu 15 kwa ajali ya barabarani, iliyohusisha lori la mizigo na gari la abiria aina Coaster katika eneo la Mikese, Barabara Kuu ya Morogoro - Dar es Salaam (A7 Highway).
Ninawapa pole familia, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Adam Malima, ndugu, jamaa na marafiki. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu ndugu zetu hawa wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka.
Mbali na wito wangu kwa umma na maelekezo niliyolipa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama Desemba 4 mwaka huu kuhusu kuongeza umakini na usimamizi katika Sheria za Usalama Barabarani, leo nimeliagiza Jeshi la Polisi kuwa na mfumo wa Leseni za Udereva utakaoweza kuwapunguzia alama (points) madereva wanaofanya makosa yenye kuhatarisha usalama na uhai barabarani. Mfumo huu uweke taarifa (records) kielektroniki za mwenendo wa makosa ya madereva barabarani kitakwimu, na kisha utumike kuamua kama wanastahili kuendelea kuwa na leseni za udereva au la. Hii ni katika kuboresha mfumo wa sasa ambao mara nyingi dereva hulipa faini pekee na kuachwa kuendelea kuwepo barabarani.
Uhai wa binadamu hauna mbadala, na hatuna budi kuendelea kuchukua hatua za pamoja na madhubuti kuhakikisha unalindwa kwa nguvu zote. Hatua hizi ni pamoja na kuhakikisha vyombo vya moto vinavyoingia barabarani vina sifa na vigezo vya kutumia barabara, na wale wanaoviendesha wana sifa, vigezo na rekodi za kustahili kuendelea kufanya hivyo.
UHURU NA MAENDELEO 🇹🇿
Haijuzu muwe huru ,mnajitawala wenyewe ,mnajipangia masuala yenu ya ndani ya kisera na kimikakati , kwa uwazi na ushirikishwaji , lakini mkibaki bila kufanya juhudi za kujiletea maendeleo itakuwa ni kazi bure.
“Maendeleo huzaa uhuru, ikiwa maendeleo yenyewe ni maendeleo ya watu. Lakini watu hawaendelezwi,ila watu hujiendeleza wao wenyewe” [J.K.Nyerere].
UHURU NA KAZI
Uhuru ulipopatikana , Baba wa Taifa akasikika akisema kwa msisitizo, kwamba kuwe na Uhuru na Kazi.
Kupata uhuru maana yake ni kila mtu afanye kazi. Azalishe mali, aidha viwandani au mashambani. Kuwa huru kisha kukawa na wananchi wasiofanya kazi ,kunaondosha mantiki ya taifa kuwa huru.
Kila mmoja anapojituma katika kufanyakazi. Analiongezea pato taifa lake na kukuza uchumi wa Taifa
#63yauhuru
Nukuu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
GAVU AWASILI GEITA KUZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
KATIBU wa Halmashauri Kuu(NEC) Oganaisheni na Mjumbe wa Kamati Kuu Issa Gavu amewasili mkoani Geita kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Gavu amewasili mkoani Geita leo Novemba 20,2025 na baada ya kuwasili amefanya mazungumzo na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Geita kabla ya kuelekea katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo zitakazofanyika katika Viwanja vya Shilabela Geita Mjini.
DKT. BITEKO AINADI CCM MARA
📌 Asema CCM Inaweza Kazi, Ipewe Kura
📌 Wabunge Waeleza Mafanikio ya CCM Mara
📌 Wagombea Uenyeviti Wajinadi kwq Wananchi
📌 Wananyamongo Wahaidi Ushindi CCM Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Nyamongo na Mkoa wa Mara kwa ujumla kufanya kampeni za kistaarabu na kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika Novemba 27, 2024.
Dkt. Biteko ameeleza kuwa maendeleo hayaletwi kwa Mathis wala kuvunjiana heshima na kuwq wananchi hao washinde ubaya kwa wema. Aidha, wamefika eneo hilo kwa lengo la kuwaomba wananchi wa Nyamongo wachague watu ambao wataungana na Serikali katika kuwaletea maendeleo.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Novemba 20, 2024 wakati akifungua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Mara zilizofanyika m katika Uwanja Nyamongo Wilaya ya Tarime.
“ Mwaka huu tuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni uchaguzi mkubwa wa kumchagua mtu atakayejua hali na maisha ya watu katika ngazi ya mtaa na ambaye atabeba shida za watu na kuzitatua,” amesema Dkt. Biteko.
Amebainisha kuwa uchaguzi huo ni muhimu na sio wa majaribio hivyo ni lazima wananchi wachague viongozi ambao sio walalamikaji na kuwa maendeleo hayaletwi kwa matusi bali kwa kufanyakazi.
Amefafanua kuwa Rais Samia ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kuwa na maisha nafuu hivyo wananchi wa Nyamongo wamuunge mkono kwa kuchagua wagombea wa CCM.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa kuna fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi kwa jamii (CSR) zinazohitaji kibali kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kuwa amemuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuhakikisha zinapatikana ili wananchi wa eneo hilo waweze kunufaika kwa kupata miradi ya maendeleo.
TUNA MTAJI WA IMANI YA WATANZANIA: NCHIMBI
_Azindua kampeni Mwanza akitamba na takwimu za kura za uhakika_
_Awasihi wanaCCM kila mmoja kutafuta kura 10 kwa ajili ya ushindi wa kishindo_
_Ahamasisha kampeni za nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu, isiachwe kura hata moja, wakiwemo wapinzani_
_Awataka washindi kuwatumikia Watanzania kwa kupinga dhuluma na rushwa_
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema CCM inaingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kikiwa na imani kubwa ya Watanzania kutokana na uimara wa chama na uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa uimara wa CCM unatokana na wingi na umakini wa wanachama wake, akitoa takwimu jinsi wanachama wapatao milioni 8 wa CCM walivyojitokeza kupiga kura wakati wa mchakato wa ndani ya chama hicho kupata wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Balozi Nchimbi amesema mtaji wa imani ya Watanzania, utumishi wa CCM kupitia sera zake, na uongozi makini unakipatia chama hicho uhakika wa ushindi mkubwa wa kishindo katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Katibu Mkuu huyo wa CCM aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Mwanza, uliofanyika katika Viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza, leo tarehe 27 Novemba 2024.
Katika kujihakikishia ushindi huo wa kishindo, Balozi Nchimbi alisisitiza kampeni za kuomba kura ziwalenge hata wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani, ili kuhakikisha kila kura inapatikana kwa ajili ya CCM, akiwahamasisha kupiga kampeni “nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu” nchi nzima.
“Pamoja na uhakika wa kura, msiridhike na ushindi. Twendeni nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu. Tusiache kura hata moja. Kila mwanachama atafute kura 10. Hata wa vyama vya upinzani, wawe ACT, NCCR, Chadema, na wote, watatupigia kura. Tumalizeni huu mchezo kwa kuipatia CCM ushindi mkubwa wa kishindo.
“Wajibu wetu ni kuwakumbusha tu Watanzania kazi kubwa ambayo CCM imeendelea kufanya katika kutoa uongozi wa nchi hii. Uhakika wa kesho ya Tanzania uko CCM. Watanzania wana imani kubwa na CCM kila wanapofikiria maendeleo, umoja wa nchi yetu, utaifa wetu, amani na utulivu. Tunataka wagombea wetu mtakapochaguliwa mkalinde heshima na imani hii ya Watanzania kwa kuwatumikia vizuri, mkijiepusha na dhuluma na rushwa,” alisema Balozi Nchimbi.
Aidha, akisisitiza kuhusu uimara wa CCM, Balozi Nchimbi alisema CCM ndiyo chama pekee ambacho wanachama wake, kwa mamilioni, walijitokeza kushiriki mchakato wa ndani wa kupata wagombea, hasa kupitia kura za maoni. Hii ndiyo sababu kimesimamisha wagombea maeneo yote nchi nzima katika uchaguzi huo, kwa kuwa kimeenea nchi nzima, tofauti na vyama vingine vya upinzani.
CPA MAKALA: MBOWE ANASEMA CHAMA CHAO HAKINA ILANI, WAGOMBEA WATABUNI.
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC ) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi,Siasa na Mafunzo CPA Amos Makala amesema amemsikia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe Akieleza kuwa Chama chake hakina Ilani na wagombea wao watatakiwa kubuni buni Ilani tu.
CPA Makala ameyasema hayo leo Novemba 20,2024 mbele ya wananchi wakiwemo wana CCM wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizindua kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa,vijiji na vitongoji unaotarajia utafanyika Novemba 27 mwaka huu.
Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi hao CPA Makala amesema amefuatilia hotuba ya Mbowe jana na amemsikia akisema Chama chake hakina Ilani na ameagiza kila mgombea atakayeteuliwa katika Kijiji chake au katika mtaa wake abuni Ilani yake
“Nilisikia hivyo kwamba wao hahawawezi kuandika Ilani, hawana jambo lolote la kusimamia uchaguzi huu ila wamewaagiza wagombea wao kubuni buni Ilani ya mtaa au kama kuna kijiji abuni yeye Ilani ya pale…
“Kwahiyo mnaweza kupata picha mnaenda katika uchaguzi kuna Chama kimeleta maendeleo na mafanikio,kuna chama kina Ilani lakini kuna chama kingine kinakuja kuomba kura lakini kinawathabitishia Watanzania kwamba wao hawakujipanga na wanataka wagombea wao wabuni Ilani katika kijiji anachokaa
“Pamoja na Ilani sisi Chama Cha Mapinduzi tumetoa tamko la kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,hawa wagombea wetu watakuwa wanajinadi lakini watakuwa wanatumia tamko la Chama Cha Mapinduzi.”
#KaziIendelee
GAVU AWAOMBA WANANCHI KUCHAGUA WAGOMBEA WA CCM UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
KATIBU wa Halmashauri Kuu( NEC) Oganaizesheni na Mjumbe wa Kamati Kuu Issa Gavu amewataka wananchi wa Mkoa wa Geita kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novembe 27 mwaka huu nchini.
Gavu ametoa kauli hiyo leo Novemba 20,2024 mbele ya mamia ya wananchi wakiwemo wanachama wa ccm alipokuwa akizindua rasmi kampeni za uchaguzi huo ambapo Chama
hicho pia kimezindua kampeni zake nchini kote.
“Nawaomba wananchi wa Geita na wanachama wa chama cha Mapinduzi,kuchagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi ili kusukuma mbele maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Wetu Dk.Samia Suluhu Hassan.”
Gavu pia amewaomba wagombea kunadi maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika maeneo yao na kusisitiza wagombea wanayo nafasi ya kuyaelezea mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020-2025.
#KaziIendelee