@Rydx_017 Kwa picha na maneno nafikiria viongozi wengi wa CHAMA hiko wametawaliwa na kiwango kikubwa Cha hofu, Woga, wasiwasi kutoka kwa mwenyekiti wao, na hayo ndio matokeo yake.
@eastafricatv Huu ndio ujinga wa Mtanzania, Hapa tunalijenga Taifa au tunalibomoa, huwezi kumfukuza Shule mtu ambae muda mchache unategemea kumtumia ktk kulijenga na kuendeleza Taifa,
"Katiba yetu ilivyoandikwa zile zinazoitwa haki za kikatiba zinaanzia Ibara ya 12 mpaka Ibara ya 29: Haki ya Kuishi, Haki ya kuwa huru, haki ya maoni, haki ya kushiriki shughuli za umma nakadhalika, hizo zinazoitwa haki za binadamu ndizo haki za kikatiba, kama kuna kitu hakijaandikwa kuanzia hiyo Ibara ya 12- 29 ya katiba hiyo siyo haki ya kikatiba. Ukienda mahakamani ukasema nimekataliwa kuandikishwa kupiga kura, nimenyimwa haki yangu ya kikatiba, Mahakama Kuu itakutupa nje kwasababu hiyo inayoitwa haki ya kupiga kura haipo katika zile ibara nilizozisema, maana yake ni kwamba tumewekewa inayoitwa haki lakini hatuna namna yoyote ile ya kuitekeleza, tukinyimwa hatuwezi kwenda mahakamani hatuwezi kwenda popote kwasababu siyo haki ya kikatiba. Matokeo yake katika hali halisi ni nini? Ni kwamba hatuandikishwi kuwa wapiga kura kama sheria ya uchaguzi inavyosema. Sheria ya uchaguzi inavyosema"- Lissu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatano Februari 12, 2025.
โTunaposema bila mabadiliko hakuna uchaguzi tuna maana kwamba kusipokuwa na mabadiliko yanayohitajika ya mfumo wa uchaguzi tutafanya kila tunaloweza kwa nguvu tulizonazo kuhakikisha uchaguzi mkuu haufanyiki mwaka huu, hatuzungunzii kususia uchaguzi hatutosusia, tutaenda kuwaambia Watanzania na tutaiambia Jumuiya ya Kimataifa, tutawaambia Walimwengu kwamba kama CCM na Serikali yake haipo tayari kufanya mabadiliko ili kuwe na uchaguzi huru na haki, uchaguzi mwaka huu usifanyike kabisa ndio maana ya no reform no electionโ
โHuu sio uamuzi wa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu, ni msimamo wa Chama cha CHADEMAโ
โNatoa wito kwa Viongozi wetu wa Dini, Maaskofu, Mapadri na Masheikh wetu, na wao ni Watanzania, yakiharibika yanaharibika na kwao yakitengamaa yanatengamaa na kwao, wasikubali kuambiwa wajibu wao ni kuombea roho za Waumini wao tu, wajiulize je miili ya Waumini wao ipoje, wahangaike na njaa ya haki ya Waumini wao, wasikubali kuambiwa wasijihusishe na siasa kwasababu siasa ndio maisha yenyeweโ
โโ Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, akitoa hotuba kwa Taifa leo February 12,2025
#MillardAyoUPDATES