Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) ni shirika la Kikristo lisilo la kidhehebu lililosajiliwa mwaka 1965 chini ya Sheria ya Udhamini wa Vyama. Na kusajiliwa nchini Tanzania kwa mujibu wa sheria mwaka 1970.
CBT ni mwanachama wa Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni
1 Wathesalonike 4:3, 7 (SRUVDC)
[3] Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
[7] Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Mika 2:1 (SRUVDC)
[1] Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
1 Wakorintho 1:10 (SUV)
[10] Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Yeremia 5:28 (SUV)
[28] Wamewanda sana, wang’aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Warumi 8:2 (SRUVDC)
[2] Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Mhubiri 12:13 (SRUVDC)
[13] Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Ndugu mpendwa mwanachama wa Chama cha Biblia cha Tanzania,
Unakaribishwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 40 (AGM) utakaofanyika tarehe 29 Mei, 2026.
Neno la Mungu lasema:
“Tazama, jinsi ilivyo vema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja.” (Zaburi 133:1)
Karibu.
2 Timotheo 2:21 (SRUV)
[21] Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Waroma 13:14 (BHNTLK)
[14] Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Yakobo 5:20 (BHNTLK)
[20] fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
3 Yohane 1:11 (BHNTLK)
[11] Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Yeremia 39:18 (BHNTLK)
[18] Maana, kweli nitakuokoa na hutauawa vitani; utapata faida ya kuokoa maisha yako kwa sababu umeniamini mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
#NenolaSiku#NunuaBiblia#Bibliakwawote
Chama cha Biblia cha Tanzania kinawatakia Ijumaa Kuu yenye tafakari na baraka tele, tunapokumbuka sadaka ya Yesu Kristo na upendo wake usiotetereka kwa wanadamu.
Neno la Mungu lasema:
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili