Tarehe na Mwezi Kama Leo ni Kumbukizi ya Siku Yangu ya Kuzaliwa, Ni Siku Yenye Maana Sana Kwangu, Nimshukuru MUNGU kwa Kuendelea Kunipigania, Niwashukuru Wazazi, Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa Kuendeleza UPENDO na USHIRIKIANO Wao Kwangu🙏🏽
HAPPY BIRTHDAY TO ME✌🏽
Asubuhi ya Leo nimefika stend Arusha to Singida, Nikiwa nimevaa Combat za Chadema, Ile nakata ticket akatokea Mzee mmoja akalipa fedha yote, Nageuka nimtambue akanishika bega akasema."Pambaneni msichoke, tunatambua Juhudi zenu, tupo na Nyie" Kisha akaondoka.
NIMETIWA NGUVU KUU✌🏽
Kwa niaba ya Mwenyekiti wangu wa Chama Taifa Mh.@freemanmbowetz natangaza Punguzo la Bei za Bia Jimbo la Hai, Bia zitauzwa nusu bei leo😌
Eid Mubarak ✌🏽
Kuna Taarifa zinazagaa Mitandaoni kuwa sitoweza kuhudhuria Mialiko ya Sikukuu ya Idd kutokana na kuwa Busy sana,
Naombeni hizo taarifa mzipuuze nipo Free Siku mbili nzima leteni Mialiko😌
Happy Mother's Day kwa MAMA zetu Duniani, Muwe na Afya na Maisha yenye Kheri.
Waliotangulia mbele za Haki Mwenyenzi Mungu awape NURU ya milele, Wapumzike kwa Amani🙏🏽
Anachokifanya Spika Job Ndugai kwasasa Sio tuu Kuvunja KATIBA bali ni kutudharau WATANZANIA tulioiweka hiyo Katiba kwamba anaweza kufanya chochote na asizuiwe.
Mkuu Wa Mkoa Kilimanjaro Mh. Anna Mwigira amechukuwa Uamuzi wa Hekima Kutangaza Hadharani Kuwa Amepata Maambukizi ya Corona.
Hii Itawasaidia Wananchi Wazidi Kuchukua Tahadhar Na Itaondoa Dhana Iliyojengwa Na Serikali Kuwa Corona Ni Ugonjwa Wa Aibu...!
Get Well Soon Mama Mwigira🙏
Nimefanya Ziara Binafsi Kijiji Cha Longoi Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Nimekuta Wananchi Wapo Bize Kunawa Mikono Kwa Maji Tiririka, Wakiamini Kuwa Hiyo Ni Mbinu Kuu Ya Kuwakinga Na Corona, Nimeumia Sana Kuona Mpaka Sasa Mipaka Ya Nchi Bado Ipo Wazi😥
Nimemskia Mbunge Mmoja Wa Ccm Ambaye Zaman Alikuwa CDM Ametowa Maoni Yake Bungeni Kuwa CDM Ifutiwe Usajili kwa Sababu Inavuruga Amani Ya Taifa.
Niwashauri CCM Kwamba Kwa Wingi Wao Bungeni Wafute Vyama Vya Upinzan Nchini, Kenge Kabisa Hawa, Wanasubiri nini?🚮