Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akitangaza taarifa ya msiba wa Mhe. Hafidh Ameir Hassan ambaye ni mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akimfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia kufiwa na Mume wake, Hafidh Ameir Hassan, wakati alipofika katika makazi yake, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki maziko yamarehemu Hafidh Ameir Hassan, mwenza waRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika Kizimkazi, Mkoawa Kusini Unguja, leo tarehe 07 Septemba 2026.
𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐔𝐀 𝐙𝐀𝐈𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐁𝐈𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐀
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Dhamana za Mali Zinazohamishika 2026.
Sheria hiyo itasaidia mikopo kupatikana kwa dhamana za mali zinazohamishika kama vile magari, mitambo, mazao, mifugo na hakimiliki.
Serikali inalenga kukuza biashara, kuongeza ajira, uwekezaji wa ndani na kuongeza mikopo binafsi kutoka 22.5% hadi 50% ifikapo 2030.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma siku ya Jumanne tarehe 8 Septemba, 2026.
Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu akizungumza na Waandishi wa Habari kutoa taarifa ya tukio hili kubwa na la kihistoria kwa Tanzania.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, leo Septemba 1, 2026, amekutana na viongozi wa Taasisi ya Culture and Development East Africa, Bi. Ayeta Wangusa na Ndugu Madaraka Nyerere, ofisini kwake katika jengo la Tume ya Utumishi wa Mahakama, jijini Dodoma.
HOMERA: HAKUNA TAIFA IMARA BILA SHERIA IMARA
Makamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, wametakiwa kutumia uzoefu na maarifa waliyonayo kuhakikisha Taifa linakuwa na sheria bora zitakazosaidia katika kutekeleza Dira 2050.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe, ametembelea Kituo cha Usuluhishi cha Kimataifa cha Kigali (KIAC) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala.
Wajasiriamali 33,594 Wanufaika na Mikopo ya Asilimia 10
Vikundi vya wajasiriamali 33,594 vimewezeshwa kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali, hatua inayolenga kukuza mitaji, kuongeza ajira na kuimarisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi.
MRADI WA LNG LINDI ✍️
Mradi huu Una manufaa makubwa kwa Watanzania kwani utaongeza thamani ya gesi asilia,Ajira na biashara mpya,mapato kwa Serikali,Fursa Kwa Viwanda vya ndani pamoja na kuifanya Tanzania kuwa mdau mkubwa wa LNG Duniani.
Serikali imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha inadhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwalinda manusura wa matukio hayo, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha haki inapatikana kwa wananchi wote na kwa wakati.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuimarisha ushiriki wake katika majukwaa ya kikanda na kimataifa ya haki za binadamu, kwa kuweka mikakati ya pamoja ya kuratibu na kusimamia masuala ya haki na wajibu.
MRADI WA LNG LINDI FURSA MPYA, HATUA MPYA KWA TANZANIA
Lindi inaelekea kuwa kitovu muhimu cha uchumi wa gesi asilia. Mradi wa LNG unaashiria fursa kubwa za uwekezaji, ajira kwa Watanzania, kukuza biashara za ndani na kuongeza mapato ya Serikali.
Hii ni Tanzania inayojenga uchumi kwa kutumia rasilimali zake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Tunasonga mbele kwa kazi na maono! 🇹🇿
#KaziNaUtu #TunasongaMbele
BOMBA LA MAFUTA LA EACOP
Thamani: USD Bilioni 3.5+ | Urefu: Km 1,443
Kwa Tanzania ni fursa ya ajira, biashara, mapato, uwekezaji na kuimarisha nafasi yetu kama lango la nishati Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Viongozi na Watumishi mbalimbali wakati akiwasili katika Ofisi yaMakamu wa Rais (Muungano na Mazingira) iliyopo Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma, leo tarehe 31 Agosti 2026
🔥🇹🇿 LNG LINDI — MRADI WA KIHISTORIA!
💰 Thamani ya mradi: USD bilioni 42
⛽ Uwezo wa uzalishaji: MT milioni 10 kwa mwaka
Hii ndiyo Tanzania ya Dkt. @SuluhuSamia — nchi yenye maono, rasilimali na ujasiri wa kugeuza fursa kuwa maendeleo. 🇹🇿🔥
Tanzania Inasonga Mbele!