Rasmi:
Chelsea yakamilisha uhamisho wa Kai Havertz akisajiliwa akitokea Bayer Leverkusen na kusaini mkataba wa miaka mitano kubaki Chelsea.
Dau linalotajwa kukamilisha uhamisho huo ni paundi milioni 72.
Karibu Darajani๐
Rasmi;
Mason Mount na Tammy Abraham wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwenye ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2019-2020 kwa tuzo zinazotolewa na chama kinachosimamia wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza na Wales maarufu kama PFA.
Tarehe kama ya leo mwaka 1989, nahodha wa Chelsea, Cesar Azpilicueta Tanco alizaliwa huko nchini kwao Hispania.
Takwimu zake ndani ya Chelsea;
Mechi 386
โฝ13
๐ ฐ๏ธ49
๐๐Premier League
๐๐Europa League
๐Kombe la FA
๐Kombe la Ligi
Anatimiza miaka 31...Happy Birthday kwake!
Rasmi;
Kocha Anthony Barry (wa kwanza mkono wa kulia) amesaanza majukumu yake klabuni Chelsea akiwa sehemu ya makocha wasaidizi klabuni hapo akisajiliwa akitokea Wigan Athletic.
Tarehe kama ya leo mwaka 2003, Chelsea ilikamilisha uhamisho wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina, Hernan Jorge Crespo.
Chelsea ililipa paundi milioni 16.8 kwa klabu ya Inter Milan ili kumpata nyota huyo aliyedumu Chelsea kwa miaka mitano.
Rasmi;
Nyota wa zamani wa Chelsea, Pedro Rodriguez amejiunga rasmi na klabu ya AS Roma iliyomsajili kama mchezaji huru.
Amejiunga na klabunhiyo ya nchini Italia na amesaini mkataba wa miaka mitatu ikimaanisha mkataba wake utamalizika mwaka 2023.
Maisha mema uendako!๐
Nyota wa Chelsea, Tammy Abraham na Mason Mount wamejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa wachezaji 24 watakaocheza mechi za kitaifa kuitumikia timu hiyo.
Hongera kwao!๐๐๐