TRANSFER FROM CHADEMA TO CCM
NOW ACTIVE MEMBER OF CCM PARTY
2020 GENERAL ELECTION CANDIDATE OF COUNCILOR FOR KALOLENI WARD IN KITETO DC GTBWLB3X GTBWLB3X
Serikali Inapesa za Kuwalipa Wabunge Feki Bungeni
Lakini Haina Pesa za Kuwaongezea Mishahara Watumishi wa Umma
WATUMISHI ....ukifika wakati wa uchaguzi CCM mbelekwambele
Endeleeni kufumba macho tu ............KAZI IENDELEE
Ukiinuliwa Wacha Kiburi Duniani Sio Pazuri Ndo Mana Watu Hulia Mara Tu Wanapozaliwa Na Kuingia Ulimwenguni Kwa Mara Ya Kwanza Kuashiria Duniani Sio Pazuri
Siasa ya ukombozi ni harakati takatifu ya kupigania haki, utu na uhuru wa watu. Haipaswi kabisa kubadilishwa kuwa biashara ya udalali au njia ya kujinufaisha binafsi. Ndani yake kuna maumivu, vifo, na mateso ya kweli ya wapigania haki. Ni jambo la kusikitisha kuona watu wanaojitokeza leo wakitafuta uhalali wa kisiasa tena, ilhali jana walishirikiana na watesi na wakatili. Ushirikiano huo hauwezi kufutwa kwa maneno matamu , kwani ni doa katika historia ya ukombozi.
Mtu yeyote ambaye hakusimama upande wa haki wakati ulipohitajika, bali akajitahidi kuzima sauti za waonewa, ni mtesaji na muuaji kama wale tunaowalaumu leo. Sasa wanarudi kwa mbinu mpya kama “drones” zinazojaribu kutua kwa ujanja lakini ukweli unabaki pale pale, hawa ni wanafiki wanaojificha nyuma ya kivuli cha siasa.
Ukombozi wa kweli hauwezi kuletwa na walafi wa mamlaka, bali na watu waaminifu kwa misingi ya haki, uadilifu, utu wa mwanadamu. Tunapaswa kukemea tabia hizi, kwani hii haipaswi kuwa tabia ya Nchi yetu na watu wake.
#BREAKING: UN YASISITIZA KUACHILIWA KWA TUNDU LISSU BILA MASHARTI
Umoja wa Mataifa umetaka kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa kiongozi wa upinzani wa Tanzania, Tundu Lissu, pamoja na viongowengine waliokamatwa kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, tarehe 11 Novemba 2025, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN, Volker Türk, alilaani kukamatwa kwa viongozi wa upinzani, akieleza kuwa ni hatua za kiholela zisizo na msingi wa kisheria.
Kwa mujibu wa ripoti za UN, zaidi ya watu 150 wamekamatwa tangu uchaguzi, wakiwemo watoto, na baadhi yao wanadaiwa kushtakiwa kwa kosa la uhaini.
Türk alisisitiza kuwa waliokamatwa wanapaswa kufikishwa haraka mbele ya vyombo vya sheria na kupewa haki kamili za kisheria chini ya sheria za kimataifa.
Pia ameitaka serikali ya Tanzania kuheshimu uhuru wa kisiasa na kuhakikisha uwazi katika kushughulikia waliokamatwa baada ya uchaguzi.
WATANZANIA
Waliitwa Kwenye Maandamano Ya Amani Na Hawakutokea Kama Walivyotarajiwa
Leo Muwaite Kwenye Maandamano Yenye Viashiria Vya Uvunjifu Wa Amani Ndo Mtegemee Waje ? NIKO PALEEE
Niko hapa nachat nikiwa angani Ft 40,000 juu ya bahari ya Atlantic , lakini Internet iko vizuri kuliko Bongo…!
NB: Na wala situmii VPN kama anavyotumia @MsigwaGerson 😎
#NoReformsNoElection
Nimekuwa nikifuatilia maoni kuhusu andiko langu la mgodi wa Tancoal (Intra Energy 70%, NDC 30%). Ningependa kusisitiza kuwa nilichokiandika ni mawazo yangu binafsi baada ya utafiti, si utetezi wa mtu yeyote kisiasa. Naheshimu walioguswa tofauti, na kwa wakati mwafaka nitafafanua jambo hili kwa kina zaidi.
Sehemu ya Wananchi wa Kigoma waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Katosho mkoani humo tarehe 14 Septemba, 2025.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12
Anaendelea Mhe. Lissu
Tatu. Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Dodoli Kapufi ilisema nini kuhusu kifungu cha 183?
Jaji Chande alisema in essence that section is deal with trial not deal with Committal. Section inayodeal na committal ni S. 261.
Nimemaliza na hiyo niendeleee na kesi yao nyingine.
Hii nayo imeletwa bure kabisa.😂
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nishughulike na JOB MREMA.
Huyu Katuga nimemaliza nae.
Anasimama Katuga anasema kifungu cha 187 hajakisemea.
Mhe. Lissu anasema nawashukuru sana Katuga. Ngoja nije hapo.
Hicho cha 187 trial at a place where act done.
Hii section is about trial na section about committal is 262, 263 hadi 265.
Hivyo basi kama ambavyo sect. 183 ilivyo irrelevant basi hata section 187 nayo ni hivyo hivyo haihusiki hapa tunazungumzia committal. Tofautisha Committal na trial.
Sasa nirejee kwenye suala la Mashahidi. Nalo lilizunguzwa na Mrema na nimesema naanza kushughulika nae.
Suala la Mashahidi wangu kutokuandikwa. Walilizungumza.
Katuga anasema hawakuitwa na kuandikwa wanaweza kuandikwa baadae hakuna tatizo. There is no prejudice.
Wakili Mrema pia alisema Mshitakiwa alishauriwa kuwa majina ya mashahidi atakuja kuwasema mahakama kuu. That one was premature kwahiyo hamna shida.
Waheshimiwa majaji naomba niwaonyeshe jinsi ambayo hii nayo ni shida kubwa.
Mashahidi kutokuandikwa kwenye commitall proceedings.
Ipo hivi Waheshimiwa majaji, Mshitakiwa ana haki ya kutamka majina na anuani ya mashahidi wake wakati wa committal maana asipoitumia inabaki fadhila ya mahakama.
Kwenye committal nilikuwa na haki ya kusema mashahidi wangu na anuani zao. Kwenye mahakama hii ni descretion yenu sio haki yangu tena.
Mnaweza kuamua au msiamue sasa niwapeleke kwenye sheria.
Kifungu cha 264 cha CPA ndo kinatoa haki kwa mshitakiwa kutaja majina ya mashahidi wake wote.
Nikisema nina mashahidi wewe Hakimu KISWAGA huwezi sema nitawasemea mahakama kuu, unapaswa kuandika.
Hilo halikufanyika.
Mawakili wa serikali wanasema ni premature, unaweza kuita baadae, sasa hiyo baadae iko kifungu cha 281 na 314 ya CPA. (Kumbukeni CPA ni Criminal Procedure Act - Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
S. 281 inasema hivi msajili wa mahakama kuu ataandaa wito kwa mashahidi wote ambao orodha yao ipo. Registrar/ msajili anatoa summons/wito kwa hao uliowataja. Kinasema hivyo.
Sasa kama hujataja nini kinapaswa kufanyika ndio S. 314 inaingia hapo. Kinasema hivyo mtuhumiwa hawezi kuwa na haki ya kuita mashahidi wake ambao hawakuwa kwenye orodha yake labda mahakama ijiridhishe kuwa kuna umuhimu wa mashahidi hao kuitwa.
Sasa hii ni fadhira ya majaji haki yangu nimesema ilikuwa Kisutu.
The accused person shall not be entitled to call witness without approval au consent ya majaji sasa kuna prejudice kubwa kuliko hiyo kunyang'anywa mashahidi wangu.
Haya maneno ya kwamba naweza kuwaita baadae ni maneno ya watu wenye nia mbaya sana na mimi.
Wanasema mambo ambayo sheria haiyatambui na kuyakubali, naomba waheshimiwa majaji msikubali jambo hili.
Sasa Job Mrema alisema majaji mnapaswa mjiulize hili pingamizi kama liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Na alilisema jambo hili kwa mbewembwe kabisa.
George Abdon Kilinga na wenzake vs Anna na wenzake ni mashauri ambayo aliyaleta hapa.
Kwanza hii ni kesi ya mirathi ilianzia mahakama ya mwanzo, ikaenda mahakama ya wilaya ya Babati ambayo iliamua kwamba wadaaawa wataamua watumie sheria gani? Mahakama kuu rufaa ya pili sasa Madam Justice alisema parties can not by agreement confer jurisdiction to a Court.
Wadaawa hawawezi jiamulia kuipa mamlaka mahakama hii kwasababu suala la jurisdiction (mamlaka) ni suala la Jaji.
Kwenye kesi yangu sasa Mshitakiwa anasema alikuwa committed na mahakama ambayo haikuwa na mamlaka.
Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Serikali ya CCM itaendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi.kwa Kuunda Tume Maalum ya Maridhiano na Upatanishi.
Tume hii itaandaa maandalizi ya kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa njia shirikishi na jumuishi.
# Kazinaututunasongambele
Serikali ya CCM itaanzisha programu maalum ya ujenzi wa mitaa ya viwanda wilayani kwa lengo la Kuzalisha ajira kwa Watanzania
Hatua hii inalenga kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza kipato cha wananchi.
#kazinaututunasongambele#oktobatunatiki✅✅
Serikali ya CCM itaanzisha mifumo rafiki ya uwajibikaji ambapo: Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wengine wa Serikali
Watatoa taarifa na kujibu maswali ya wananchi.
Hiki ndicho kitakuwa kipimo cha utendaji wao kuhakikisha viongozi wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi
Leo ni Zamu ya Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Viunga Vyake! Kumpokea Mgombea Urais CCM- Dkt Samia Suluhu Hassan na Kusikiliza Sera bora za CCM .
#kazinaututunasongambele#oktobatunatiki
Impunity is not immunity.
Haki itatendeka tu, Rais @SuluhuSamia unatumia vyombo vyote vya dola dhidi ya chama chetu na kiongozi wetu. Kwasababu ya uoga wa kushindana, kwasababu mheharibu uchumi wa nchi yetu, kwasababu serikali yako haina majibu kuhusu usalama wa watu, vijana wanatekwa wanauwawa na kupotezwa. Wewe Rais na serikali yako hamna majibu kuhusu ajira kwa vijana wala hamna mpango na uwezo wa kuleta ajira.
Serikali yako inaongoza kwa ufisadi na rushwa za kutisha.
Mnaogopa hayo inabidi Mtumie mbinu ovu kumnyanyasa Lissu
Kitu muhimu cha kukumbuka ni kwamba hakuna kinga ya kutenda uovu.“impunity is not immunity “
Watanzania hawatakubali na bado tunasisitiza #NoReformsNoElections tutaenda hatua zaidi kuhakikisha madai yetu yanasikilizwa na yanafanyiwa kazi.
Hii ndio IMPACT ya CHUKI ambayo mmekuwa mkiipandikiza kwa jamii kwa muda sasa, na TULIWAONYA …Na bado tutaona mengi kama mkiendelea kuvimbisha MAFUVU kisa mna DOLA!
#NoReformsNoElection#FREELISSU