Hali ni mbaya ndani CHADEMA jahazi linazidi kuzama taratibu,Wakili wake amejitoa kwenye kesi kisa kuhujumiwa na viongozi wenzake ambao wanaitumia kesi ya Lissu kujinufaisha binafsi
RAIS SAMIA AIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI KUPITIA MAZUNGUMZO NA MTAWALA WA DUBAI
Rais Dkt Samia,amekutana na Kufanya mazungumzo na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mtawala wa Dubai, pembezoni mwa Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit) 2026 unaofanyika Dubai.
Katika mazungumzo yao,wamejadili fursa mbalimbali za ushirikiano katika sekta za uwekezaji,biashara,uchumi,maendeleo endelevu na mabadilishano ya kitamaduni. Aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto za pamoja zinazolikabili dunia,ikiwemo mabadiliko ya tabianchi,maendeleo ya teknolojia na ustawi wa jamii.
Rais Samia ameipongeza UAE kwa uongozi wake madhubuti katika mageuzi ya kiutawala na matumizi ya sera bunifu zinazolenga maendeleo ya muda mrefu. Vilevile, ameonesha dhamira ya Tanzania ya kuendelea kushirikiana na UAE ili kuchochea uwekezaji, kuongeza fursa za ajira na kuboresha maisha ya wananchi.
Mkutano huo unaakisi msimamo wa Tanzania katika kuimarisha diplomasia ya uchumi na kujenga ushirikiano wa kimkakati kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.
Kwa maelezo zaidi unaweza kutembeleaππΏ;
https://t.co/MW0DhjTcYe
https://t.co/MW0DhjTcYe
@barakawamb Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuithibitishia dunia kuwa Tanzania iko tayari kwa ushirikiano wa kimkakati unaochochea ukuaji wa uchumi kupitia diplomasia makini.
Rais Dkt .SSH ametajwa kwenye orodha ya Wanawake 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Afrika kwa mwaka 2025. Orodha hiyo imetolewa na Avance Media.Aidha, Rais Samia ametambuliwa kwa diplomasia ya kiuchumi kuimarisha nafasi ya Tanzania kimataifa, na kuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake.