Tafuta wimbo wa
Ambwene, unaitwa- Natamani sana.
Pata muda wa kuusikiliza kwa utulivu, uelewe neno kwa neno, baada ya kuusikiliza kwa mara nyingi, anza kuufwatisha, imba kama ombi lako kwa MUNGU, hata kama unaendelea na kazi zako, wewe imba kama ibada.
✓Shalom
Luke 4:13
[13] When the devil had finished all this tempting, he left him until an opportune time.
✓“An opportune time.”🤔
James 1:14
[14] but each person is tempted when they are dragged away by their own evil desire and enticed.
✓Katika ile biashara iliyokufa, nini tumejifunza.
✓Nini tulijifunza baada ya kuumizwa na rafiki au mchumba.
✓Nini tulijifunza baada ya kufukuzwa kazi.
✓Nini tulijifunza baada ya Baba na mama kuachana.
@Shalom
SHIDA/CHANGAMOTO zina mafunzo mengi sana ambayo RAHA haziwezi kutupatia. Badala ya kukumbuka namna tulivyoumia tulipopitia kipindi cha shida nyingi, tutafute nini tulijifunza katika hayo.
[9] Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa KINYWA chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini MOYONI mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. [10] Kwa maana kwa MOYO mtu huamini hata kupata HAKI, na kwa KINYWA hukiri hata kupata WOKOVU.
✓Rum 10:9-10
Kama tukifanyiwa ubaya na watu tutabadilika tabia ya kufanya wema, tafsiri yake ni kwamba hatukuwahi kua wema wala tabia ya kufanya wema haikua asili yetu (tuliigiza..!!), Mtu mwema habadiliki kwa kufanyiwa ubaya, kama ilivyo kwa mwovu habadiliki kwa kufanyiwa wema.
Upo ugonjwa wa kutafsiri maandiko kwa namna ya kuvutia utaratibu wa kule tunakokusanyikia, huu ni UDINI. Neno la MUNGU halina udini, wala si shabiki wa kanisa fulani. Neno la MUNGU, lina nguvu ya kumkaripia yeyote na kudai matengenezo hata kwa sisi tunaofikiri tuko sahihi.
Wanadamu tunafahamu kuku huatamia mayai siku 21. Hii ni tofauti sana kwa kuku mwenyewe, yeye hafahamu hizo siku 21, anachojua ni kuyaatamia mayai mpaka vifaranga vitakapoanguliwa. Maombi si jambo lenye ukomo, kwamba utamaliza usubiri majibu. Omba mpaka utakapojibiwa.
✓1Thes 5:17
Toba haiondoi madhara ya dhambi. Ukiiba mali ya mtu wakakukamata, wakakupiga mpaka ukang'ooka meno. Baadae ukitubia dhambi ya wizi na ukaokoka, meno yako hayata ota tena, utakua mlokole mwenye mapengo. Kuna hali ngumu unaipitia leo, huenda ni madhara ya dhambi uliyowahi kuitubia.
Maisha humgusa kila mmoja kwa namna tofauti, ukilia wewe katika nyanja fulani ya maisha, haina maana wengine wote wanalia. Ni vizuri zaidi tukafikiri ikiwa mahali tulipo ndipo ambapo MUNGU alitaka tuwepo🤔.
Usimkatishe tamaa yeyote kwa sababu ya historia za maumivu ulizowahi kupitia. ¹MUNGU YUPO, na ni halisi. ²kufanya kazi kwa bidii kuna faida. ³Ndoa zinadumu, na upendo wa kweli bado upo sana. ⁴Elimu bado ni muhimu na ndoto za wengi zinatimia kupitia elimu.
Many of the things that you think are evil, might not be evil to GOD. Because they drew you to the place of prayer and even when you pray GOD will delay answers, until the spirit of prayer and supplication rest upon you, when HE knows even if HE answers you will not stop praying.
Kwa bahati mbaya hakutakua na ushahidi wowote kwa kizazi kijacho, kwamba Baba au Mama aliwahi kupambana kwa juhudi zote ila “akashindwa”. Fursa pekee tuliyo nayo ni kuhakikisha tunapambana mpaka tunafanikisha japo kwa udogo🤏,hata kama hatukufikia ukuu, lakini hatukuishia patupu.