Jioni hii, ibada fupi ya kumwombea marehemu Suez Dani Maradufu imefanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, kabla ya mwili wake kuondoka na kuanza safari kuelekea Tarime, mkoani Mara, kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Leo Jumanne, tarehe 30 Juni 2026, Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imekutana katika kikao chake cha kawaida mjini Kigoma, Kanda ya Magharibi. Kikao hicho kinaongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. @HecheJohn.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi Mhe. Rhoda Kunchela akizungumza katika mkutano wa hadhara wa operesheni #KatibaMpya#FreeTunduLissu uliofanyika Mpanda Mjini, Mkoa wa Katavi, katika uwanja wa Kashaulili leo tarehe 25 Juni 2026.
Hii inaitwa IGA UFE, JARIBU UFILISIKE.
1. Mbarali, Mbeya
2. Makambako, Njombe
3. Songea Mjini, Songea
4. Masasi, Mtwara
Hii ni mikutano ya hadhara katika mikoa minne tofauti kanda ya kusini na Nyasa. Mikutano mingine imefanyika asubuhi. Watu ni wengi kama mchanga.
Wananchi wamekuja wenyewe bila kusombwa na kulipwa na wamechangia TONE TONE kuendesha chama chao. Wananchi wanaipenda CHADEMA.
Mashosti wa mbogamboga, wao hadi bajeti itoke kwa MaCCM na msimu wa uchaguzi ufike ndio unaweza kuwaona majukwaani. Siasa za posho. Shensisana.
#KatibaMpya #FreeTunduLissu
Katibu wa Chadema Kanda ya Kusini Mhe. @ShijaShibeshi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa operesheni #KatibaMpya#FreeTunduLissu uliofanyika Mbeya Mjini, uwanja wa Stendi ya Kabwe leo tarehe 23 Juni 2026.
"Leo CCM ukimkosoa @SuluhuSamia wanasema unamtukana, nchi gani hii watu wamejaa hofu, watu wanaiba rasiliamali za nchi, mbuga za wanyama zinauzwa, madini yetu yanaondoka kinyume na utaratibu wa sheria. Hata ndani ya CCM kumwambia @SuluhuSamia unapeleka nchi shimoni hawawezi kusema." Mhe. @HecheJohn
SINGIDA, jiandaeni! Baada ya Kamati Kuu tunamalizia majimbo mawili ya Mkoa wa Morogoro, halafu tunahamia kwenu, kijiji kwa kijiji, mkoa mzima. Mood iko Top Class! Walisema CHADEMA itakufa, lakini muda unaendelea kuthibitisha tofauti. We are here to stay, and to conquer.
Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. @HecheJohn akizungumza katika mkutano wa hadhara wa operesheni #KatibaMpya#FreeTunduLissu uliofanyika Mbeya Mjini, uwanja wa Stendi ya Kabwe leo tarehe 23 Juni 2026.
Leo, tarehe 23 Juni 2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. @HecheJohn, akiwa wilayani Mbarali kuendeleza Operesheni "Katiba Mpya, Free Tundu Lissu", ameshiriki zoezi la kupandisha bendera kwenye vizimba mbalimbali vya chama katika Kata ya Chimala, Kijiji cha Rimbogo, Jimbo la Mbarali.
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini Mhe. Belchomas Ponera akizungumza katika mkutano wa hadhara wa operesheni #KatibaMpya#FreeTunduLissu uliofanyika Mbeya Mjini, uwanja wa Stendi ya Kabwe leo tarehe 23 Juni 2026.
Katibu wa CHAUMMA Mkoa wa Mbeya, Protas Mgimbila, leo tarehe 23 Juni 2026 ametangaza kukihama chama hicho na kurejea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mgimbila alikuwa mwanachama wa CHADEMA kabla ya kuhama mwaka 2015. Amepokelewa rasmi kurejea CHADEMA katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stendi ya Kabwe, mjini Mbeya, ambapo viongozi na wanachama walimkaribisha.
Makamu Mwenyekiti wa Bara, Mhe. @HecheJohn, usiku huu amefanya kikao na wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa Chadema (CHASO) Mkoa wa Mbeya, hii ni baada ya mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo jijini Mbeya.