Ahsanteni sana wana Bahi kwa kujitokeza kwa wingi na kwa dua na maombi leo asubuhi nilipokuwa nikihitimisha kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Urais kwa Mkoa wa Dodoma, kabla ya kuelekea Mkoa wa Singida. Ninawashukuru sana.
Hii ni kielelezo tosha kwamba Dkt Samia anapendwa sana, hili nyomi limetuma ujumbe kwa watu wote wasiomtakia mema Samia na nyomi hili pia linawaita wote waliokigeuka Chama waje tuungane sisi ni ndugu wa baba mmoja na mama mmoja Chama Cha Mapinduzi.
Tutailinda amani ya Nchi yetu kwa wivu mkubwa, wala hatutakuwa tayari kuruhsu migawanyiko ya kisiasa kwakuwa Ardhi ya Tanzania imekuwepo kabla ya kuwepo vyama vya siasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Comoro kwenye Sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika katika uwanja wa Malouzini Jijini Moroni tarehe 06 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Waumini wa kanisa la Arise and Shine alipowasili katika hafla ya Ufunguzi wa Kanisa la Arise and Shine, Kawe Jijini Dar es salaam.
Haya ni Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita mkoani Katavi kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025 ambapo Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali zimeongezeka mkoani humo.
Kwa kipindi hicho, Zahanati zimeongezeka kutoka 80 hadi 127 ikiwa ni ongezeko la zahanati 47
Vituo vya Afya vimeongezeka kutoka 17 hadi 28 ikiwa ni ongezeko la vituo 11 sawa na asilimia 39.
Aidha hospitali 4 za Wilaya zimekamilika huku Hospitali ya Manispaa ya Mpanda imekarabatiwa
Imani yetu ni kwamba Dkt Samia Suluhu Hassani atatuvusha kwa kishindo 2025-2030.
Wako watu walikaa mtaani na degree zao zaidi ya miaka mitano hasa walimu lakini leo wanashukuru sana ujio wa awamu ya sita, wapo kwenye vituo vya kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma leo tarehe 26 Juni, 2025. Pamoja na mambo mengine kesho Mhe. Rais Dkt. Samia atahutubia na kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya kufanikisha jawabu la changamoto ya maji kwa wananchi 450,000 kwa kuzindua Mradi wa Maji wa Butimba, nilipata wasaa kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kirumba.
Imekuwa jioni nzuri Jijini Mwanza, tukimshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hatua kubwa za maendeleo tunazoendelea kupiga kwa pamoja. Tumezungumza na kukumbushana umuhimu wa ushiriki wa kila mwananchi na makundi yote ya kijamii katika kulinda amani na utulivu wa nchi yetu. Usalama wa nchi yetu ndio msingi wa maendeleo na mshikamano wa kitaifa.
Leo Juni 19, 2025 nchi imepata historia nyingine kubwa, daraja la JP Magufuli leo limeziduliwa rasmi na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Hii ni hatua kubwa sana, tunaipongeza Serikali kwa kulikamilisha hili daraja.
Leo imekuwa siku ya kihistoria kwa nchi yetu na ukanda wa Afrika Mashariki ambapo tumefungua ukurasa mpya katika sekta ya usafiri na usafirishaji kwa kuzindua Daraja la JP Magufuli. Daraja hili ni uthibitisho mwingine kuwa nchi yetu inakua kiuchumi na tunaweza kupanga na kutekeleza mambo makubwa. Pongezi kwa kila Mtanzania. Haya ni matunda ya nguvu zetu sote.
Tulitumie daraja hili kama nyenzo ya kujiletea maendeleo na tulitunze ili lidumu. Daraja hili ni sehemu ya miundombinu na miradi ya kimkakati tuliyoikamilisha, hivyo, nimeiagiza Wizara ya Ujenzi na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha linalindwa na kutunzwa kwa uzito huo kwa niaba ya Watanzania wote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Hospitali ya Wilaya ya Itilima katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.