Meta who also owns WhatsApp, banned my number 424-537-3057 from WhatsApp because this is the number Tanzanians were using to send me the photos and videos of the October 29 killings committed by Samia Suluhu which I then posted on this X page.
It’s clear meta has decided to de platform anyone opposing the illegitimate and brutal Tanzania government. Just sad.
🔵🇧🇷 Maresca: “I’m just trying to help Estevão, to not put pressure on him, to use him in the right way”.
“This is only reason why he doesn’t play from the start every game”.
Many Tanzanians want an international independent investigation into the killings.
Three weeks after the election, there are many families still searching for their loved ones
Bro to Bro
Chochote unachopoteza kama mwanaume, ilimradi si uhai wako, unaweza kukirudisha na hata kwa ukubwa zaidi.
Unaweza kuinuka tena kutoka kwenye chochote. Mshirikishe Mungu kwenye mipango yako, weka Juhudi na usikate tamaa.
Ulishawahi kufanya, unaweza kufanya tena!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 41
Wanaendelea Upande wa Jamhuri
Sasa anasimama Thawabu Issa Wakili wa Serikali kusoma PH.
Anasema majina ni Tundu Lissu, Mwanasiasa na Kiongozi wa Chadema.
Anashitakiwa kwa kosa moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39 cha Penal Code.
Mshitakiwa ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na ana utii na anamiliki hati ya kusafiria na anaitaja.
Kwamba Mshitakiwa alidahiliwa na kuorodheshwa miongoni mwa maafisa wa/askari wa akiba mwaka 1989 na kumaliza 1990. Alianza Mafinga JKT na baadae Mbeya.
Tarehe 03/05 akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA aliitisha mkutano kuongea na watia nia waliokuwa wanakusudiwa kugombea uchaguzi mkuu 2025 pale Mikocheni Makao makuu ya Chama.
Kupitia mkutano huo alitengeneza nia ya kuushwishi umma kuzuia uchaguzi mkuu kwa lengo la kuitishia serikali. Na katika kuidhihirisha nia hiyo alichapisha maneno yafuatayo.
"Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi ni kweli kwasababu tunasema tutazuia uchaguzi. Tutaenda kukinukisha vibaya sana huu uchaguzi tutaenda kuuharibu"
Mkutano huo ulikuwa unarushwa na Jambo TV.
Maneno yake yalichochea sehemu ya umma na wachochewa hao walianza kujikusanya maeneno mbalimbali na wakawa wamekubaliana kuzuia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025.
Wengine walikamatwa wakati wakiendelea kutekeleza nia yao hiyo kwamba maneno hayo yaliyosemwa yamepelekea kuwa ni kosa la jinai na yakawa yamewasilishwa kwa mkuu wa upelelezi kanda maalumu ya Dar.
Mshitakiwa alikamatwa huko Ruvuma na kufikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es salaam inayoketi Kisutu Tarehe 10/04/2025 na hadi sasa amesimama mbele ya Mahakama hii kujibu mashtaka yake na huo ndio mwisho wa hoja hizo.
Jaji anasema Mahakama itakusomea na wewe utajibu.
Nitakupitisha kila aya baada ya nyingine.
1. Anamuuliza kuhusu majina yake na kuwa ni mwanasiasa.
Mhe. Lissu anasema ongeza kuwa ni mwanasheria na wakili wa Mahakama hii. Msiishie hapo.
2. Pia unashitakiwa na uhaini kwa mujibu wa sheria
Mhe Lissu : Ndivyo ninavyoshitakiwa Mh. Jaji.
3. Wanasema ukiwa mtii kwa JMT kwa kuwa Mtanzania wa kuzaliwa una hati ya kusafiria yenye namba TAE458265 iliyotolewa na Uhamiaji.
Mhe. Lissu : Hilo ni kweli kabisa Mhe. Jaji
4. Pia wanasema ulisajiliwa na kuwa recruited katika jeshi la kujenga taifa mwaka 1989 katika kikosi cha 841 Kj Mafinga na ulimaliza kikosi cha 844 Kj Mbeya na ulitunukiwa Cheti.
Mhe. Lissu : Mhe Jaji kama lengo ni kuonesha mimi ni mwanajeshi basi hawajielewi na mimi sio mwanajeshi ni kweli nilienda JKT ila mimi sio mwanajeshi, anayesema hayo hajui alisemalo.
Jaji naomba urudie hatujaelewa. Anarudia kusema tena.
Hayo maneno kama anadhani mimi ni mwanajeshi hajui asemalo na Mungu amsaidie kwamba mimi nina uaminifu wa JMT hilo sasa nawasubiri wawalete hao wanajeshi wao. Tutakutana.
5. Uliitisha mkutano na ukazungumza na ....... jaji kasita Mhe. Lissu amesema nikusaidie nilizungumza na watia nia.
Mhe. Lissu : mimi sikuitisha huo mkutano. Uliitishwa na viongozi wa Chama wa Chini yangu na niliuhutubia ni kweli.
Watiania niliwahutubia ila mkutano sikuuitisha Mimi.
6. Katika mkutano huo ulihudhuriwa na Media Personnel wa Mwananchi, Jambo TV na nafasi Media ni miongoni mwa walioalikwa.
Mhe. Lissu : Nafahamu walikuwepo waandishi wengi kuhusu vyombo gani walioleta mashitaka wanafahamu mimi siwezi kufahamu vyombo gani vililuwepo.
7. Hoja nyingine wanasema kupitia mkutano huo ulitengeneza nia ya kushawishi umma kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuwatisha Executive yaani serikali.
Mhe. Lissu : Nilitengeneza nia ya kuwashawishi watanzania na wanachama wenzangu kuzuia uchaguzi mkuu na kwa vile sio kosa kwenye sheria zetu maneno hayo ni bure kabisa kuwa nilifanya kosa.
Part 42 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.