TUJADILI:
Kwa nini ABIRIA alipie huduma ya Choo Stand Kubwa (fenced)..?
Ukiingia getini unalipia
Tiketi umelipia
-Kwanini na huduma ya choo ulipie?
-Kwanini wamiliki wa mabasi wasilipie management costs za choo?
-Kwanini pesa za getini zisitoshe to cover management cost?
Bedriya kutoka Ethiopia alitafuta mtoto kwa miaka 12 ndani ya ndoa, hatimaye amejifungua mapacha Watano. Bedriya mwenye miaka 35 anasema alimuomba Mungu ampe mtoto, alipopata ujauzito aliambiwa amebeba 4 ila siku ya kujifungua amepata 5, wakiume 4 na wakike 1. Wanaendelea vizuri.
𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀 𝐅𝐎𝐑 𝐅𝐈𝐅𝐀 𝐏𝐔𝐒𝐊Á𝐒 𝐀𝐖𝐀𝐑𝐃.
Dunia imeona bao bora zaidi mwaka huu ni kutoka kwa Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama. Utamu wa bao hili zaidi ni kumfunga mtani na kuchangia mtu kuliwa kichwa.
Jambo la kufanya kwa Mwanasimba ni kutag akaunti ya @FIFAcom ujumbe uwafikie mapemaaaaa!!! #NguvuMoja
Jana tulikuwa na mazungumzo kuhusu Siku ya historia ya VALANTINE DAY.
Mke wangu aliniuliza, Hivi Godbless , ungependa Brilliant (Binti yetu) aolewe na mume mwenye tabia kama zako ?
Nikajibu faster , aolewe na mtu kama Yesu !!
Akacheka 😂😂😂Bro, acha kurukaruka, Yesu hakuoa!!’ Nakuuliza wewe !!
Mbona jibu rahisi sana ?
Nikajibu, nahitaji marekebisho kidogo na maombi kwa sasa kwanza!!
Akasema, Awake your spirit Godbless, ikiwa wewe ni baba na hauwezi ku recommend mtoto wako aolewe na mwanaume mwenye tabia kama zako basi iko shida!! Bahati nzuri wakati stori zinaendela , Bon Yai alipiga simu , nikaenda pembeni nikasema naona kuna simu ya kikao, nikawa nimepita hivii , nikamwambia Ney , unajua Lissu kanyimwa chakula huku nikiwa nimekunja uso !! Ney , hawa CCM ni sadist sana!! Nikajiongelesha !!
Okay !! Sasa na wewe mwanaume mwenzangu nakuuliza kama nilivyo ulizwa? Je , ungependa binti yako aolewe na jamaa mwenye tabia kama zako ?
Kama jibu ni hapana !! Badilika !! Tubadilike!!
Unajua sisi wanaume tunapenda sana kulaumu wanawake kwa kuchagua mwanaume asiye sahihi, lakini kamwe hatumlaumu mwanaume aliyeficha utu wake wa kweli na kujifanya mtu mwingine ili ampate mwanamke mwema. Hatari kubwa sana hii.
Nawatakia Siku Njema ya Wapendanao.
TAARIFA KWA UMMA.
KESI YA UHAINI DHIDI YA Mhe LISSU KUENDELEA.
Nawafahamisha kwamba kesi ya uhaini dhidi ya Mhe Lissu, Criminal session case No. 19605/2025 imepangwa kuendelea Mahakama kuu, Kanda ya Dar Es Salaam kuanzia tarehe 09 February 2026 hadi tarehe 06 March 2026.
Ikumbukwe kwamba kesi hiyo inasikilizwa na Majaji watatu, Mhe Jaji D. Ndunguru, Mhe Jaji J. Karayemaha na Mhe Jaji Kiwonde.
Tayari Mhe Lissu jana alipokea taarifa rasmi kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama kuu.
Tukutane Mahakamani.
Gaston Galubindi
Mkurungenzi wa Sheria CHADEMA Taifa,
Umeona inavyouma eee??
Sasa hayo ndio maumivu ya dhuluma!!
Hayo ndio maumivu anayopata mtu anayenyimwa haki!!
Imagine hiyo ni haki kwenye mpira tu inauma hivyo!!
Sisi tunaonnyimwa haki za kuishi tunaumia vipi!??
Unang’ang’ania madaraka, unaua watu, unazuia wapinzani wako kushindana na wewe, unateka watu, unapoteza na kuua kikatili kama. Alivyofanyiwa mzee Kibao.
Unafanya yote hayo ili iweje, Kama maji tu yamewashinda miaka 64 iliyopita?
Sisi ni Nchi ya tatu kwa vyanzo vingi bora vya maji safi na baridi Duniani. Nchi ambayo mvua zinanyesha kila mwaka.
Asilimia 60 ya madawa yanayonunuliwa kwenye hospital zetu ni kwasababu ya magonjwa yanatokana na kutumia maji machafu.
Kwahiyo ukiwapa watu maji safi na salama ya bomba, utakua umeokoa 60% ya bajeti ya dawa zielekezwe kwenye mambo mengine. Pia utakua umeokoa maisha ya watu wengi sana.
Miaka 64 bado eti tuna wizara ya maji na watu wanatembea Nchi nzima, kuahidi kwamba tutaleta maji..
Ndio maana watanzania wanataka uchaguzi huru na haki waweke watu wanaoweza kuondoa kero hizi, lakini poa hao watu wakishindwa Watanzania wawe na uwezo wa kuwaondoa na kuweka wengine.
Unatumia mabilioni ya shiling kununua silaha, kulipana posho, kuua na kutisha watu kulinda madaraka uliyojipa mwenyewe bila ridhaa ya watu.
Ungewapa watu vitu wanavyohitaji wao wenyewe wangekutetea, matendo yako na uongozi wako ungekutetea sio silaha wala polisi.
Kufikiria vijana Watanzania ni wajinga ni kujidanganya….
Mnatakiwa kutoka kwenye denial, hiki sio kizazi cha kuambiwa mambo ya uongo.
Mnaiba pesa za umma, mnaiba rasimali za vijana wa Nchi hii mnakabidhi wageni.
Vijana wanataka uchaguzi huru ufanyike ili wapate viongozi watakaosikiliza sauti yao na kuwaheshimu, watu wataoweka maslahi ya Taifa mbele sio maslahi ya familia zao na vikundi.
Leo mnapora uchaguzi kwa mtutu wa bunduki, mnataka nini?
Watu watakaopambana kuwaletea ajira na fursa za maisha bora.
Kudai haya sio kulipwa, wala kushawishi..
Vijana wa Tanzania sio wajinga, acheni kufikiri kwamba nyie na familia zenu ndio wenye akili.
Walijaribu kutugawa kwenye maandamano ya #MO29 kwa kutaka kuaminisha UMMA yale yalikuwa maandamano ya CHADEMA ikashindikana.
Sasa wanajaribu kutugawa Kwenye maandmaano ya #D9 kwa njia ya DINI ZETU. Hili pia tumekataa na litashindikana maana GEN Z , hatuna DINI wala CHAMA.
Dini yetu sisi NI MUNGU MMOJA.
Chama Chetu sisi ni HAKI.
Kesho fanya vyote usikose BANDO.
Kesho dunia inaenda kuona kwa kina yote yaliyofanyika GIZANI kupitia kituo kikubwa cha habari cha CNN.
Kumbuka Hii imewezekana kwa nguvu ya UMMA. Page zetu wananchi ziligeuka Media kuihabarisha Dunia wakati Media zimeingia MITINI.
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵😎