Kioo kinachomsaidia dereva kutazama mbele ni kikubwa kuliko vioo viwili vya pembeni vinavyomsaidia kuangalia nyuma..
Tutumie nguvu nyingi kuangalia tunakokwenda kuliko tulikotoka
Nyuma pangekuwa muhimu Mungu angetuwekea macho kisogoni.
Wanawake Hawapendi Kabisa Mwanaume Awe Na Mahusiano Na Mwanamke Mwingine.
Ila Wanapenda Mwanaume Awe Na Uwezo Wa Kuvutia na Kupata Mwanamke Mwingine.
All Women Are Attracted With A Man Whom Other Women Wants And Admires.
Kuna nyakati kwenye maisha huna budi kupukutisha baadhi ya watu katika maisha yako ili upate fursa ya kuwapanga upya waendane na muelekeo wa maisha yako. Kupangua nako pia ni kupanga.
Kama tunao uwezo wa kuiona nia njema tunapokosewa na wale tunaowapenda, basi tunao uwezo pia wa kuiona nia njema tunapokosewa na wale tusiowapenda au wasiotupenda. Tukibadili mtazamo wetu na vile tunavyovitazama hubadilika pia.
Katika kujirekebisha kwangu kunaweza kusababisha mtikisiko na hata kwako. Si kwamba nimedhamiria kukutikisa bali ni kwasababu uko karibu sana na mimi. Ungekuwa mbali nisingekufikia. Ndio ilivyo kwenye maisha, ukiona unakereka na mtu huenda tatizo ni wewe umemsogelea sana."