Baada ya mechi mbili za maelezo mijadala ambayo mwanzo walikuwa hawataki wao kuisikia wameirudisha mezani.
Toka mechi ya kwanza anicet oura anaanza kuvaa uzi wa simba kila mtu alikubali kuwa jamaa anajua boli hata wao walikiri ndani ya nafsi zao na toka hapo anicet ameendelea kuwa wa moto.
Baada ya wachezaji wao kushindwa kuwa na form mzuri kwenye mechi za ushindani haswaa walikuwa hawataki hata wachezaji wao wafananishwe na oura kwakuwa walijua jamaa kawaacha mbali sana ila ghafla baada ya mechi mbili zao za maelezo na mipango mingi (mbeya city na pamba) ghafla wametoka mafichoni na kuanza kumfananisha anicet oura na wachezaji wao wa mechi za mipango.
Guys anicet oura huyu sio tu anajua boli ila ndo mchezaji pekee aliyefunga kwenye mashindano yote msimu huu akianza na klabu bingwa tena hatua ngumu ya makundi ana chuma mbili swaaafiii na ligi ya NBC ameshafunga huku kombe la CRDB confederation akifunga pia na sio kufunga tu ila amekuwa pia mshereheshaji na kila mtazamaji ajutii kulipia kiingilio kumuangalia akifanya ngono na boli.
Kwahyo wakati munajaribu kusifia wachezaji wenu wanaoonekana kwenye mechi za maelezo tangulizeni heshima kwanza kwa ivorian boy Ancient oura.