Uongozi wa Simba Sc umefikia makubaliano ya kumsajili Mchezaji mzawa wa Tanzania akitokea Kagera Sugar Nassoro Kapama ambaye tayari amekuwa mali halali ya Simba Sc kwa mkataba wa miaka miwili.
@Simbasportsclub
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Victoria Kwakwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2022.
Wananchi wa kaya 104 kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro waliohamia Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni wameanza kupewa elimu ya kujikinga na malaria baada ya kuhamia katika mazingira hayo mapya.
“Mimi nilitoka Kijiji cha Esere Ngorongoro, kule ni mazingira ya baridi na hakuna mmbu. Msomera ni mazingira tofauti na baridi ni ya kawaida na wakati mwingine joto hivyo elimu hii ni muhimu sana kwetu ili tujikinge pamoja na Watoto wetu” aliongeza Laizer.
HATIMAYE!! Eng.Hersi Ally Said ashinda kuwa rais wa Yanga kwa kupigiwa kura za Ndiyo na wanachama waliowengi wa timu hiyo zoezi ambalo limefanyika kwenye ukumbi mikutano wa kimataifa wa Julius International Conference Centre Jijini Dar es salaam leo tarehe 9 Julai,2022
@yangasc
Kenya imetangaza kwamba siku ya Jumatatu ya tarehe 12 Julai,2022 itakuwa siku ya Mapumziko kupisha Waislamu kusherehekea sherehe ya Eid Al Adha.Huku Tanzania ikiwa siku ya Jumapili ya tarehe 10 Julai,2022.
#DicksonUPDATES
Rais Mstaafu wa Angola Jose Eduado Dos Santos Afariki Dunia
Dos Santos ambaye ameliongoza taifa hilo kwa kuwa wa pili kwa uzalishaji wa mafuta amefariki jijini Barcelona ambapo alikuwa hospitalini akipatiwa matibabu.
Mchezaji Bora wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa wanawake Clara Luvanga amepokea tuzo ndani ya ukumbi wa Johari Rotana Jijini Dar es salaam leo tarehe 7/7/2022.