Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona (Uviko-19) kama tunavyoelekezwa na wataalamu wetu wa afya. Tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni, tutumie vitakasa mikono, tuvae barakoa na tusigusanegusane. Ugonjwa wa Korona upo.