"Msiogope kwenda kupiga kura kwani kila mwenye mahitaji maalumu atapewa kipaumbele kupiga kura bila kukaa kwenye foleni na kuhakikisha anakuwa salama. Nendeni Mkachague viongozi mnaowataka ambao watakuwa wazuri kuwaongoza na kuwatatulia changamoto zenu za kijamii” RC. Senyamule
“Wajibu wa kulea Makundi haya yenye uhitaji ni wa jamii nzima ikiwa ni pamoja na Wazazi, Walezi, kijiji, Serikali kutokana na uwezo unaokuwepo kwa wakati huo, pia ni wajibu wa mtu mmoja mmoja atakayeguswa, hakuna mtu mmoja mwenye jukumu la kulea watu wenye ulemavu” RC Senyamule
“Serikali imeendelea kutatua kero za Walimu ikiwemo kupandishwa vyeo, nyongeza ya mshahara kila mwaka ambayo imeleta tija, kubadilishwa miundombinu ya Utumishi na kulipa madeni mbalimbali ikiwemo madeni ya likizo, uhamisho, fedha za kufunga mizigo kwa Wastaafu”. RC Senyamule
“Ukosefu wa Amani unajenga chuki, unaondoa mapatano, unapoteza haki, lakini pia unachelewesha maendeleo. Sisi Tanzania na hata maeneo mengi Duniani, tumeona nchi ambazo zimepoteza Amani, kuja kuirudisha si jambo rahisi sana na wakati fulani inachukua karne na miongo” RC Senyamule
“Mhe. Rais anafanya kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo katika nchi yetu hivyo niwapongeze kwa hatua nzuri ya kumsemea Mama kazi anayoifanya katika Mkoa wetu na kuona wajibu ambao tunaendelea kuufanya katika Mkoa”. RC Senyamule kwenye kikao na Wanawake waMkoa wa Dodoma.
“Vijana tunapaswa kujitambua, kujua haki zetu, kujua miili yetu, na kujua namna ya kufanya maamuzi sahihi yanayolinda afya zetu. Tusiogope kuuliza maswali. Tusiogope kutafuta msaada kutoka kwa Wazazi, Walimu, au Wataalamu wa Afya.” Mwl. Vicent Kayombo.
"Niwapongeze kwani Mbio hizo zimeunganishwa na ajenda za Kitaifa za kuunga Mkono Jitihada za Mhe. Rais za masuala ya Afya katika kuongeza zaidi bajeti ya afya na ununuzi wa Dawa na NBC Mmeunga Mkono katika masuala mazima ya usonji na kansa ya shingo ya kizazi” DC Jabir Shekimweri
“Kulingana na utafiti wa Kitaifa uliofanywa 2022 ushamiri wa maambukizi ya Homa ya Ini aina B ni 3.5% kwa watu wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 60. Tunaweza kuona ni tatizo kubwa kama ilivyo maambukizi ya Ukimwi Kitaifa ni 4.5% tunaweza kuona Homa ya Ini inakaribia hapo” Dr. Njau
“Mradi wa AHADI kwa kipindi cha miaka mitatu umekua na manufaa katika Mkoa kwa kuwafikia kwa elimu ya afya ya uzazi, kupinga ukatili wa kijinsia na stadi za maisha jumla ya vijana rika balehe 13218 ambapo 2639 ni wale walio nje ya shule huku 10,579 wakiwa shuleni”. CPA. Ntikahera
"Naamini kupitia mkutano huu tutaweka makubaliano ya utekelezaji wa pamoja katika vyanzo vya mapato, aina ya miradi, maudhui na uwajibikaji kwenye mipango inayotekelezwa kuanzia ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi Mkoa ili kurahisisha usimamizi na ufuatiliaji". Bi. Nyamkomora
Mkoa wa Dodoma unatarajia kuanza sehemu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa ushirikiano na Wawekezaji kutoka Kampuni ya LIFAN GROUP ya nchini China ambao wanatarajia kuwekeza kwenye kiwanda cha kuunganisha Pikipiki na Bajaji katika Wilaya ya Chamwino.
“Kufika kwenu katika kikao hiki si kwa bahati mbaya, ninyi nyote ndio kisima cha maarifa ya mafanikio ya michezo kwenye Mkoa wetu. Natamani nyote mliopo hapa kila mmoja adhamirie kwenda kufanya jambo zuri litakaloacha alama mahali alipo kwenye sekta hii ya michezo". Mwl. Kayombo
“Malengo ya nchi ni kupunguza vifo wakati wa kujifungua kutoka 504 kwa vizazi hai 100,000 na hapa Dodoma tumeona mabadilikomakubwa, kwa mwaka uliopita, tulisajili vifo 75 kutoka vizazi hai 100,000 na 58 kutoka mwezi Januari mpaka sasa ambapo ni matokeo ya Mfuko huu” DC Shekimweri
"Aina nyingine ya utalii inayopatikana katika Mkoa wa Dodoma ni utalii wa kilimo hususan kilimo cha zao la zabibu, ambalo linalimwa kwa wingi na ni kivutio kinachopatikana katika Mkoa wa pekee ". RC Senyamule
“Mpango huu tayari unatuonesha mafanikio 60% ya utekelezaji wake, kazi tunayobaki nayo sasa ni 40% kwa kazi kubwa na nzuri ambayo umeifanya. Mhe. Rais umeonesha uzalendo mkubwa kwa kutekeleza mambo yaliyokuwepo na yaliyokua kwenye mipango ya miaka ya nyuma sana.” RC Senyamule
“Dira 2050 imeweka lengo na shabaha kufikia uchumi wa kati wa juu wa Dola Trilioni moja, naelekeza Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu waweze kuandaa nyenzo zitakazotumika kupima utendaji Serikalini kwa kuzingatia malengo na shabaha za Dira hii”. Rais Samia
"Nimpongeze Askofu ambaye leo amekua rasmi Askofu wa Kanda ya Kati. Tumekua tukishirikiana naye kwenye mambo mengi. Kwa heshima kubwa aliyokabidhiwa na Mungu, niendelee kukuahidi, tutatoa ushirikiano kuhakikisha Kanisa linaendelea kuwa na amani, utulivu, na kustawi". RC Senyamule
"Nawapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya —pamoja na huduma za kiroho, mmekuwa mkihudumia jamii kwa kuanzisha vyuo vya thiolojia, shule, zahanati na vituo vya afya. Mmeendeleza maisha ya watu kiakili, kimwili na kiroho. Hongereni sana". Prof. Kabudi.
“Wanawake waombolezao wana kina cha maombi. Kama mnavyojua kipindi hiki kuelekea uchaguzi kuna watoto, familia, uchumi na mambo mengine, tunawakutanisha kina Mama kuomba na kuomboleza kwa ajili ya kuweka hali nzuri ya Amani, nchi bila Amani hatuwezi kukaa”. Mch. Deborah Malassy
"Wafugaji wa Bahi, Dodoma na Tanzania, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatamani kuona tunaongeza thamani ya mifugo tunayofuga". Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ashatu Kijaji.