"Kwa niaba ya wachezaji wenzangu moja ya malengo yetu ni kuanza msimu vizuri kwa kushinda mechi hii muhimu ya kesho, naweza kusema tumejiandaa vizuri na sote tunafahamu umuhimu wa mchezo huu na tunatambua jukumu tulilonalo la kulinda na kulitetea taji letu.
Tutaingia uwanjani tukiwa na umoja, ari na kujiamini tukiamini kwamba tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri" @Hussein15Mo
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko