Akiwasilisha mitigating factors, Lissu anasema:
"Historia haijawahi kuwa nzuri kwa Majaji wanaofunga watu wasio na hatia ili wamridhishe mteule. Hilo kosa la uchochezi mmelitafuta wenyewe Majaji kumsaidia mteule wenu."
What a Man!
‼️UNVERIFIED TAARIFA‼️
Kwa mujibu wa vyanzo viwili (bado kimoja hatujathibitisha), Polepole anashikiliwa kituo cha Mabwepande na anajlhojiwa
Ushauri kwa ndugu na jamaa wafike hapo na mawakili!
Msiogope #Tutashinda ✊🏽 Wanataka kutusambazia hofu ila wana hofu zaidi yetu 😀
#TutaelewanaTu
Tatizo askari wetu wanahisi kama yakifanyika mabadiliko ya kiutawala au upinzani ukichukua nchi basi wote wataachishwa watakosa kazi!!
Upinzani hauji na askari wake jamani, upinzani hauna askari polisi wa kucover nchi nzima, askari mtaendelea kuwa nyie nyie na kazi yenu hamtapoteza.
Kinachopambaniwa hapo ni mabadiliko ya kimfumo, ili tuwe na mfumo bora unaosimamia na kutoa haki kwa raia na mali zake!!
Mfumo wenye maslahi na watanzania wote, watoto na wajukuu zenu na sio kikundi cha watu wachache!!
Ungeni mkono tulete mabadiliko na kwenu hamtapoteza ajira zenu!!
WANAOFAIDIKA NI MABOSS ZENU TU!!
SIO NYIE ASKARI WA CHINI, TENA NYIE NDIO MKO WENGI!
WAO NDIO WANALIPWA MISHAHARA MINONO!
WAO NDIO WATOTO WAO WANASOMA PRIVATE SCHOOL
WAO NDIO WAKIUGUA WANATIBIWA NJE AU AGAKHAN!
NA WANA BIMA KUBWA!!
WAO NDIO WAKISTAAFU WANAPEWA KIINUA MGONGO CHA MAANA!!
WAO NDIO WAKISTAAFU BADO WANAPEWA VYEO VYA UBALOZI AU UKUU WA MKOA!!
NYIE MNATESEKA TU KAMA SISI, TIA MCHUZI PANGU PAKAVU!!
NYIE NDIO WATOTO WENU NA WATOTO WETU WOTE WANASOMA KAYUMBA NA HAWAPATI ELIMU BORA!
NYIE NDIO WAKE ZENU NA WAKE ZETU WAKIWA WAJAWAZITO WANASHEA KITANDA KIMOJA MAHOSPITALINI!
NYIE NDIO HAMNA MAGARI KAMA SISI TU, WOTE TUNAGOMBANIA MWENDOKASI MKIWA OFF WORK!
NYIE NA SISI WOTE KIKOKOTOO KINATUHUSU!!
SASA TUNAPOUNGANA KUPIGANIA MABADILIKO YA KIUTAWALA, NI TUNAPIGANIA NA MAISHA YENU PIA!
TUNAPIGANIA KESHO BORA YA WATOTO NA WAJUKUU ZENU!!
TUNAPIGANIA WATOTO WENU NA WETU WASIJE KURITHI HIVI VIBARUA VYETU VYA UWINGA, AU HIZO KAZI ZENU!
AMBAZO HATA NYIE TUNAJUA HAMZIPENDI NI VILE HAKUNA ALTERNATIVE TU!
JE UNAPENDA MTOTO WAKO AJE AFANYE KAZI HIYO!?🤷🏿
SASA KWANINI NIKIPIGANIA MABADILIKO HAYO, UNANIPIGA RISASI, UNANIPIGA MABOMU,UNANIPIGA VIRUNGU, UNANITEKA NA KUNIUA?🤷🏿
NIUNGE MKONO TUIKOMBOE NCHI TUZIKOMBOE FAMILIA ZETU MIMI NA WEWE AFANDE!!
Mwenyekiti CHADEMA jimbo la Kibamba, Ubungo, Dar es Salaam, Ernest Mgawe jioni ya siku ya jana, 01.10.2025 alihitajika kituo cha Polisi Gogoni, alipofika, wakaelekea kituo cha polisi Oysterbay, Kinondoni.
Tangu majira ya saa tatu usiku 01.10.2025 katika kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni alikuwa akiandika maelezo, ilipofika majira ya saa sita na nusu usiku 02.10.2025 walielekea nyumbani kwake Kibamba
Baadae, Polisi Oysterbay walielekea nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya upekuzi katika makazi yake. Saa 11:20 alafajiri wakamaliza kufanya upekuzi katika makazi yake Kibamba na kurudi Oysterbay Police Post.
Walirejea katika kituo cha polisi Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam baada ya kumaliza zoezi la upekuzi ambalo hawakupata kitu chochote ambacho kinahusiana na tuhuma zinazomkabili ndugu Ernest Mgawe.
Zoezi la upekuzi lilikuwa linasimamiwa na Mkuu wa kituo cha polisi Gogoni Wilaya ya Ubungo, ASP Yahaya M. Omary aliyekuwa akitekeleza maelekezo yaliyotoka katika ofisi ya RCO mkoa wa kipolisi Kinondoni.
Jeshi la Polisi linamtuhumu na kumshikilia ndugu Ernest Mgawe kwa makosa mawili (1) kuhamasisha maandamano. (2) kuhamasisha watu kufanya vurugu katika vituo na magari yanayokwenda kasi (BRT)
NB; kwa kuwa Ernest Mgawe alirejeshwa alfajiri ya saa 11 kituo cha polisi Oysterbay, mawakili wa CHADEMA wamesubiri asubuhi kuendelea na mchakato wa dhamana yake kwa kuwa tuhuma hizo zinadhaminika.
Ile chuki mbaya dhidi ya Chadema hadi kubambikia kesi, kuteka na kuua viongozi, wanachama na wafuasi wake, imewasaidia nini?
Sasa wapinzani ni wananchi, na hasa vijana. Mtateka na kuua wangapi?
Actually, narudia kusema wazo la kuteka na kuua wapinzani ni la KIPUMBAVU sana.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 36
Anaendelea Mhe. Lissu
Wakili wa serikali alisema utaratibu upi unapaswa kutumika? Na Jaji Nyalali akamjibu na makubaliano yakawa utaratibu huo utumike hadi utakapokuja kubadilishwa.
Sasa hadi leo hakuna kilichobadilishwa, hizi kesi zote mbili ni za kwao hawa ma DPP sasa leo wanasema tuendeleee. HAIWEZEKANI.
Mahakama hii isiwaruhusu kuleta mambo ambayo yalishawekwa sawa na watu waliowatangulia kwenye maofisi yao.
Mwisho naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo.
1. Je makosa haya yote yanarekebishika? Kama hujataja kosa unarekebishaje? Hiyo maana yake ni hakuna.
Mahakama ya rufani inasema hiyo ni sifuri. Unarekebishaje sifuri kwahiyo hayarekebishiki na kama hayarekebishiki the information must be quashed.
2. Maneno sio kosa ila nia ya kuitisha serikali juu ya kuzuia uchaguzi.
Hayo maneno ya kuitisha serikali yako wapi kwenye hiyo charge sheet? Wapi serikali imetajwa? Wapo viongozi wake wametajwa? Haipo kabisa.
Habari ya kuitisha serikali kwenye maneno haya haipo kabisa ni maneno matupu haya. Tufuate msimamo wa Khatibu Gandi kuwa maneno matupu hayafui dafu katika hili.
Naomba waheshimiwa majaji hati hii ya mashitaka ifutwe mara baada ya mawasilisho hayo.
Amemaliza Mhe. Lissu.
Naona Majaji wanaandika kidogo naona pia wananong'onezana wote watatu. wanaandika tena.
Ngoja tusubiri watasema uamuzi ni lini?
Naona majaji wanacheka kimya kimya. hawataki tuwaone wanacheka.
Si unajua zile style za vicheko vya majaji ni kama hawacheki hivi.
Wanacheka na kujikausha kama hawajacheka vile.😂😂😂
Jaji Nduguru amesema Mahakama itatoa uamuzi siku ya Jumatatu saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 35
Anaendelea Mhe. Lissu
Hizo nyaraka baada kusomewa kule chini vyote kwa pamoja vinaletwa huku.
Sasa ukileta kimojawapo bila kingine ujue hapo hakuna kesi yani ulete information bila witness statement. Kwamba taarifa inaweza kusimama peke yake.
Naomba hili Waheshimiwa majaji mumuachie Katuga abaki nalo yeye na kikundi cha wenzake hapo maana hakuna information without witness statement. They go together.
Sasa mmeambiwa hivi walijiandikia au waliandika hayo ni maswala ya ushahidi.
Sasa hilo sio suala la ushahidi maana it is on the face of records, nyaraka mnazo hapo na mnaona mkiangalia.
Sasa anasema wakija watasema wameandika kwa mamlaka gani?
Hatuhitaji kuwasubiri waje waseme walishaandika tayari na mamlaka hayo wameshayasema sasa S. 10(3) ya CPA inaruhusu wajiandikie wenyewe maelezo?
Hilo ndio swali sasa.
Sheria imesema nani anayepaswa kuandika maelezo ya mashahidi ni police officer anayechunguza yeye ndio anawakanya, anawaonya, anasign na kumuandika mashahidi.
Hili limefanywa na mapolisi wengine kwenye kesi hii hii hawajaandika wenyewe. Wameandikiwa na mapolisi wengine kama sheria inavyotaka.
Kwanini kuwe na mapolisi waliojiandika na wawepo walio andikiwa? Unaelewa nini hapo.
Kwanini vyote viwe sahihi? Wasituchezee akili hapa wajifunze sheria.
Hakuna mtu anayeweza kujionya mwenyewe na kujiapisha mwenyewe.
Haya yote yapo on face of records. Tusipeleke kesi mbele wakati haipo wako polisi wanne wamepatia utaratibu.
Shida ya mapolisi huwa hawasomi sheria eti wameandika kwa mujibu wa kifungu cha 10(3) ambacho kinasema wanapaswa kuandikiwa maelezo na sio kujiandika wenyewe.
Lipo lile lingine la hawa Mawakili wa serikali waliomba mashahidi wao wasijulikane wafichwe na jaji akawapa alichowaomba. Kusiwepo na anuani, majina, kazi zao, makazi yao, majina ya ndugu zao na hakikisheni mnawapa majina bandia na mfute hayo ambayo hayatakiwi.
Wakaondoka na hiyo amri wakafuta futa majina mengine wakaacha,
Amesimama Katuga anasema Mheshimiwa ameanza tena kwenda mbali huko hatukufika. Naombeni mwongozo sisi tulielewa hivyo. Mtoe guidance.
Jaji: Lissu unasemaje?
Lissu: hicho anachopinga sio sahihi na amesema haya mambo hata yeye leo hapa.
Majaji wanateta kidogo hapa.
Wanasema tuendelee hebu achanana na Katuga.😂
Sasa kwenye ile kesi ya Felius Mulokozi kesi ya armed robbery aliyenyooshewa silaha hakutajwa. Mahakama ya rufani ikasema hilo shitaka na hati yake ni batili.
Isdory Patrice kesi ya attempted rape waendesha mashitaka kwenye hati ya mashitaka hawakuweka neno attempted mahakama ya rufani ikasema hilo sio shitaka ikafuta.
Waheshimiwa Majaji kwenye kesi ya Uhaini usipotaja kulikuwa na nia ya kutenda kosa la uhaini na ukasema kulikuwa na nia ya watu kuzuia uchaguzi mkuu.
Hiyo hati ya mashitaka inasalimika vipi?
Kama kutokutaja nani aliyenyooshewa silaha imefuta kesi ya armed robbery na kutotaja neno attempted kesi ilifutwa. Huku kutokutaja kabisa kosa la uhaini kunabakije?
Kwa maoni yangu kosa hili ni kubwa zaidi kuliko kutokuandika attempted au kutokusema nani alinyooshewa silaha.
Hili la uhaini mambo yanabaki vipi yalivyo kwa maoni yangu hati ya mashitaka haibaki kabisa na kama nilivyosema.
Haiwezi kubaki hii hati ya mashitaka.
Naomba waheshimiwa majaji wala msiicheleweshe kabisa, ifutilieni mbali huko.
Wakili wa Serikali Mkuu amesema pia kuhusiana na Grey Likungu Mataka na Khatibu Gandi kwamba yale yote niliyosema kuhusu namna ya kuandika charge sheet au information hayakuamuliwa kwenye objection yaliamuliwa kwenye hukumu ya kesi kwahiyo na hii twende tutaamua mbele kwa mbele.
Waheshimiwa Majaji ni kweli hayo yaliamuliwa kwenye Judgement yaani yalisemwa kwenye trial kwasababu mawakili wa mashitaka hawakukosea waliandika hati zao sawasawa.
Hivyo ndio maana yaliibuka huko mbele. Kwenye hii kesi yangu wao wamekosea kuandika hii information yao.
Part 36 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 34
Anaendelea Mhe.
Kwahiyo kusema tusubiri ushahidi hakuna cha kusubiri ushahidi hapa maana hakithibitishiki na hakipo kabisa.
Na nimalizie hoja hii kwa kusema hivi Mahakama ya rufani kuanzia ile ya Afrika Mashariki na muhimu zaidi hii ya Tanzania. Zote zimesema "usipoweka haya mambo ya lazima kwenye hati ya mashitaka hakuna uhaini na shitaka hilo halipo." Hakuna nafasi ya kwenda nje ya msimamo wa mahakama ya rufani.
Sasa waheshimiwa majaji wakili wa serikali amezungumzia vilevile juu ya utaratibu wa kuandika hati za mashitaka za uhaini.
Ameenda kwenye Sect. 138 ya CPA na amesema haijatoa utaratibu wa namna ya kuandika mashitaka ya uhaini.
Angalau amekubali hilo sasa kama hakuna utaratibu tunaishia kwenye maelekezo ya kifungu hicho cha 138 cha CPA.
Sasa Majaji utaratibu wa kuandika hati za mashitaka haupo kwenye sheria za Tanzania ila upo kwenye maamuzi ya mahakama za Tanzania.
Usipokuwepo kwenye CPA sio kwamba haupo bali Mahakama ya rufani kwenye Khatibu Gandi ukurasa wa 22 na 23 ilisema kwa vile utaratibu huo haupo kwenye CPA utaratibu tutakaoutumia ni utaratibu uliotumika na mahakama ya rufani ya afrika mashariki kwenye Grey Likungu Mataka utaratibu huo uliowekwa kwenye Grey Likungu unasemaje?
1. Hati yamashitaka ya uhaini ionyeshe statement ya kosa.
2. Ionyeshe maelezo ya kosa la uhaini.
3. Lazima matendo ya kuthibitisha (overt act must be pleaded)
Hati ya uhaini ni LAZIMA iwe na mambo hayo matatu haipaswi kuwa kama hati ya mashitaka ya kosa la kuiba kuku.
Hii taarifa imetengenezwa na ofisi ya DPP iliyotengeneza hati ya mashitaka iliyotengeneza kwenye Grey Likungu Mataka na Khatibu Gandi.
Jaji Mkuu nyalali alisema niliulizwa na wakili wa serikali kulwa Masaba nieleze utaratibu ukoje...
Hivyo huu utaratibu unafahamika kwenye ofisi ya DPP. halafu kwenye hii ya kwangu wameleta kwa mujibu wa sheria ambazo hazipo maana utaratibu wanaufahamu na upo maofisini kwao wanachopatwa kukisubiria hapa ni HATI KUFUTWA.
Sasa Waheshimiwa majaji naomba kuzungumzia hicho kinachoitwa Amendment ya hati ya Mashitaka, kifungu cha 295 cha CPA, tumezungumza sana.
Kifungu kinafanya reference ya amendment ya hati ya mashitaka under s. 294 and the accused is not aware/ there must be notice.
Kwa kifupi ni kwamba lazima notice iwepo, kuhusu amendment ya Charge. Na s. 294 inasema mahakama kutoa amri ya kufanya amendment ya Charge.
Hivyo ukitaka kufanya marekebisho ya hati ya mashitaka, tumeambiwa tuende kwenye 294(2) na mahakama ndio inaleekeza hapo nini cha kufanya.
Sasa Mashitaka yalisomwa tar. 10/04 haya ya uhaini. Mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka ya kufanya chochote ni kweli.
Sasa kifungu cha 295 kinaposema notice ambayo mshitakiwa amepatiwa hiyo notice ni nini?
Hiyo offence ambayo mshitakiwa amepewa nayo kuhusu kosa lake ni ipi kama sio Charge sheet? Hiyo ndio taarifa niliyopewa.
Sasa hiyo taarifa haiwezi rekebishwa kienyeji enyeji kupitia 294 yaani Mahakama lazima itoe ruhusa sio kujifanyia.
Hawajaomba ruhusa wamejifanyia inatakiwa ifutwe.
Na hayo marekebisho waliyofanya sio madogo, wanataka kurekebisha makosa yaliyokuwa kwenye Charge sheet wanafikiri yatawaokoa.
Hata baada ya hayo marekebisho hii hati ya mashitaka bado haiwaokoi wala kuwafikisha kokote.
Kuhusu maelezo ya mashahidi tuendelee hapo sasa.
Waheshimiwa Majaji wakili wa serikali amesema jambo moja kubwa sana.
Amesema kwamba taarifa ya kosa haina uhusiano wowote na maelezo ya mashahidi.
Kwamba taarifa inaweza kusimama yenyewe bila maelezo ya mashahidi. Akatoa ule mfano wa Chamber summons supported by affidavit.
Kwahiyo information sio lazima iwe na maelezo ya mashahidi.
Sasa Lengo kuu la Committal proceedings ni kukusanya maelezo ya mashahidi. Yakikamilika maelezo hayo basi 262(6) of CPA DPP anaandaa tarifa pamoja na maelezo ya mashahidi mahakama inayarudisha committal Court ili mshitakiwa akasomewe huko mahakama ya chini.
Part 35 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 33
Anaendelea Mh. Lissu.
Watu wanafurahi kumsikiliza.
Mawakili wa serikali wamesema hati ya mashitaka kuhusu publication na kifungu cha 39(2) cha Penal Code.
Publication maana yake maneno yaliyochapishwa kwenye karatasi yaani writing au printing.
Nilimsikia anasema nilichapisha na nikaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Angalieni kwenye hati ya mashitaka kuwa nilichapisha kwenye mitandao ya Kijamii.
Sasa angalieni hayo maneno kama yapo kwenye hati ya mashitaka kuwa nilichapisha hayo maneno kwenye mitandao ya kijamii.
Kama yapo niambieni ili nikae chini kama maneno hayo hayapo hawawezi kuja kusema wakati wa ushahidi.
Hivyo basi publication by writing or printing haipo kokote sasa Waheshimiwa Majaji kuna kitu nimesikia kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.
Kwamba maneno ni matendo. The deed of uttering words. Waheshimiwa majaji maneno sio matendo ieleweke vizuri.
Huyu Katuga ni mtu mwema sana alituletea maana ya deed kutoka Black's law dictionary anaisoma hapa.
Deed sio maneno, something that is done or carried out na sio kusema, kuongea. Hiyo ndio Deed.
😂😂😂😂Katuga alisoma maana ya Deed kwenye blacks law dictionary hakuelewa.
Anaendelea Lissu.
Kwa mara ya kwanza nimesikia kwa Katuga kuwa maneno ni matendo hiyo tafsiri tumuachie Katuga akae nayo mwenyewe ni yake.
Amegundua hili yeye.
Mahakama ya rufani ya Tanzania ilisemaje juu ya maneno na uhaini, nafikiri hata hili Katuga hajalielewa na halifahamu kabisa.
Tutaelekezana pia katika hili.
Mahakama ya rufani ya Tanzania ilisema hivi ...... Kwenye uhaini maneno ni nini?
Ukurasa wa 55 mere words do not amount to overt act on a treason charge na ikasema maneno matupu haitengenezi kosa la uhaini isipokuwa hayo maneno yanaelezea kitendo cha uhaini.
Maana yake ni kwamba wanaopanga uhaini wanakaa vikao na kupeana maelekezo hapo utasema maneno hayo ni vitendo vya uhaini eti kuhamasisha wananchi kuzuia uchaguzi. Hii ni kesi ya Khatibu Gandi.
Sasa kama Mahakama ya Rufani imesema Maneno hayatengenezi matendo ya uhaini nani anayeweza kubisha?
Ni huyu Katuga?
Pia ukurasa wa 67 inasema hivi Francis Nyalali Jaji mkuu anasema kanuni kuu maneno hayatengenezi matendo ya uhaini lakini wakiwa wengi inaweza kuwa vinginevyo na isipokuwa mshitakiwa akiwa mmoja huwezi kusema maneno yake yanatengeneza uhaini.
Kwa kifupi akisema mtu mmoja kama nilivyosema mimi na nikashitakiwa mtu mmoja kama nilivyoshitakiwa mimi basi hakuwezi kuwa na uhaini ndio msimamo wa sheria ya uhaini as we speak today.
Hajalijibia hili amekimbia kimbia tu sasa kwahiyo nimesema hakuna nia ya kufanya kosa na hakuna publication na maneno matupu hayavunji mfupa kwenye uhaini.
Kuna kitu hapa amekisema sana katuga, umma, umma, umma.
Hivi UMMA ni nini? Anaongea ongea tu umma. Umma ni watanzania milioni 63+ hayo majina yanapaswa kuwepo kwenye hati yaje kuwa pleaded nimezungumza na watu fulani usipowataja ni kosa, umekosea kuandaa hati ya mashitaka.
Haya hayahitaji ushahidi, hati ikiwa mbovu inafutwa kabla mshitakiwa hajajibu shitaka, inafutwa kabla ya ushahidi ieleweke hivyo.
Anaendelea Lissu.
Waheshimiwa Majaji kabla sijaondoka kwenye habari ya publishing kwasababu sheria inasema publishing by writing or printing sasa hiyo writing or printing ni lazima iwe pleaded.
Mtakaposoma Grey Likungu mtaona hao waliopanga kupindua serikali walikuwa wanaandikiana baru na kulikuwa na chapisho linaloitwa Ukweli na hayo yote yalikuwa set out kwenye hati ya mashitaka.
Waheshimiwa majaji mkiangalia kwenye kesi hiyo hiyo kwenye ukurasa wa mwisho kabisa, ameainisha hizo overt act zaidi ya 34 because the were pleaded ziliwekwa kwenye hati ya mashitaka.
Huwezi ukasema alichapisha halafu ukaishia hapo, unapaswa kusema alichapisha nini, wapi, akapeleka wapi? Hata walete mashahidi hayapo kwenye information.
Part 34 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 32
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa Waheshimiwa Majaji wakili wa serikali akaenda kwenye kifungu cha 39(d) cha Penal Code yaani Kanuni ya Adhabu juu ya Uhaini na akarudi kesi za Grey Likungu Mataka.
Na akasema kwa Mujibu wa Grey Likungu Mataka kwamba mambo yanayofanya kosa la uhaini ni matatu makuu ndio alivyosema Katuga.
1. Utiifu kwa jamhuri ya muungano
2. Kutengeneza nia yaani nia ya kutenda kosa la uhaini.
3. Uthibitisho wa kutenda hiyo nia ya kosa la uhaini. Manifestation.
Wakili wa serikali amesema hayo masharti matatu sio pekeee.
Sasa mimi namuuliza so what?
Hayo masharti mengine mimi sijalalamikia.
Utiifu kwa jamhuri mimi sina shida na sharti hilo na hoja yangu haipo hapo.
Hoja yangu ni kwamba kulikuwa na nia ya kuunda kosa la uhaini.
Na pili hiyo nia ilithibitishwa kama inavyotakiwa?
Sharti la pili la hicho kifungu cha 39(2) cha Penal Code. Hati ya mashitaka inapaswa kuonyesha ulitengeneza nia ya kutenda kosa la uhaini.
Taarifa iliyoko mbele yenu waheshimiwa majaji inasema nilitengeneza nia ya kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi mkuu.
Anaisoma hapo hiyo taarifa yaani Charge sheet ile hati ya mashitaka.
Wakili wa serikali hajagusa hilo hata kidogo kwamba nilihamasisha watu kuzuia uchaguzi sio kosa la uhaini wala kosa lolote la jinai.
Amekimbia kwenye hili
Hajagusa hata kidogo. Hakuna nia na sijatengeneza nia ya kutenda uhaini.
Ila nimetengeneza nia ya kufanya watu kuzuia uchaguzi wa Tanzania na hiyo sio kosa la uhaini.
Huwezi kuelewa mambo haya kama hujui sheria.
Nilisema mambo yako zaidi ya 10 yanayotengeneza kosa la uhaini wakili wa serikali akasema yako 13 sasa naomba kumuuliza kwenye hayo 13 je ni kitendo gani kinasema kuzuia uchaguzi ndio uhaini? Hakipo na hajasema hapa.
Wakili wa serikali Mkuu alivyokimbia kwenye hoja hiyo akasema kwamba.
Hii taarifa iko sawa sawa kwasababu imetaja jina langu, tarehe, kwamba mimi ni mtiifu wa jamhuri hayo yote wapi nilisema yana shida?
Anasema alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025. Kama nilivyosema Waheshimiwa Majaji hilo sio kosa wala sio inshu kabisa.
Infact kwa kusema hayo anathibitisha niliyosema nia ni kuzuia uchaguzi. YES. That is not an offence under the laws of the National Republic of Tanzania.
Anasema kwa lengo la kuitisha serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Watu wazuie itishike Serikali. Waheshimiwa majaji naomba angalieni hiyo information kuna mahali nimetaja serikali? Huwezi kusema ana lengo la kuitaja serikali wakati hajaitaja serikali sikutaja hata MWENYEKITI WA KIJIJI sio serikali tu.
Sasa hayo anayosema yalipaswa kuwepo kwenye taarifa yanapaswa kuwepo kwenye hati ya mashitaka.
Iseme ulitisha serikali yenyewe inasema nilikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi, hakuna kosa la kumshitakia mtu hapa labda uwe hujitambui.
Akasema haya mambo ni ya ushahidi. Sasa watambue kuwa tukienda kwenye ushahidi hawatakuja kusema ilitishwa serikali wakati humu wamesema walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi.
Wasifikiri tukienda kwenye ushahidi wasifikiri wataenda kwenye UVUVI WA USHAHIDI kwamba waseme lolote.
Na facts zako kwenye Charge sheet hazioneshi chochote kuhusu kutisha serikali na kosa la uhaini.
Hawatatengeneza kosa la uhaini kwenye ushahidi kosa linatengenezwa kwenye hati ya mashitaka.
Part 33 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 30
Anaendelea Katuga,
Mshitakiwa anapaswa kupewa nyaraka hizo lakini sio kwamba nyaraka hizo unaweza kutumia moja dhidi ya nyingine.
Maelezo ya mashahidi hayawezi kutumia hati ya mashitaka kuondoa uhalali wa hati ya mashitaka.
Kutafsiri vifungu vya sheria unaweza kwenda kwenye vifungu vingine kupata maana.
Maombi yoyote chini ya sheria hii ni lazima kuwepo na Chamber summons na affidavit sasa hakuna kifungu kinasema mashitaka haya yanafunguliwa kwa hatinya mashitaka yakiwa yamesupportiwa na maelezo ya mashahidi.
Natamani siku moja binti yangu Kylie aje kuwa Wakili lakini sitaki awe kama Katuga 😂 kiukweli napata wakati mgumu hata kumsikiliza anachosema.
Anaendelea Katuga.
Hii hoja tunaona ilitakiwa kuja mwanzoni na sio muda huu.
Sasa hivi ni afterthought kwamba witness statement ilipaswa kupingwa wakati ule wa awali na sio pingamizi la leo.
Tunaomba jambo hilo lisiruhusiwe muda huu.
Kifungu cha 11 cha CPA kinasema Police officer afanye nini anapomuhoji nani? Kinachosema hicho kifungu ni kumtenganisha police officer na shahidi mwingine wa kawaida.
Na hayo yote yanahitaji ushahidi kwahiyo tunapaswa kusubiri wakati wa ushahidi.
Sasa kesi ya Jamhuri vs Mbenga Seif Kasanwa, Abdu Masibu, Abdu Rajab.
Sasa stare decis hii ni persuasive kwenu ni kesi ya mahakama kuu hii. Haiwafungi mikono.
Ni kesi pia inayozungumziwa mazingira tofauti kabisa.
Sasa kuna kesi ya Silius Mlokozi vs Jamhuri nayo haiungi mkono chochote kuhusu madai ya mshitakiwa hapa mahakamani.
Katuga anasema hata mshitakiwa alikubali kusema haya maneno.
Amesimama Lissu anasema mheshimiwa huko hatujafika bado kwamba nimekubali kuwa nilisema au sijasema.
Nilichokuwa nakiongea mimi ni kuwa hayo maneno kwa mujibu wa katiba ibara ya 18 na kifungu cha 52 cha Penal Code na sheria ya vyombo vya habari ni maoni tu na sio kwamba nilikubali.
Jaji Ndunguru anasema sasa mjielekeze msiseme vitu ambavyo havipo hakusema hivyo labda useme maneno yanayoonekana kwenye hati ya shitaka ni haya hapa.
Imeita simu ya Polisi mara mbili inapiga kelele.
Mahakama imesimama lakini hawajachukuliwa hatua yoyote.
Angekuwa mwanaChadema hapa sijui Kama hili jambo lingepita kimya kimya maana huyu askari sijui anashida gani mara ya nne simu yake inatusumbua hapa.
Anaendelea Katuga na kusema Mheshimiwa Jaji hati ya mashitaka haina shida yoyote kwasababu imejengwa kwenye kifungu cha 138 cha CPA hivyo huwezi kuweka pingamizi.
Tunaomba kumalizia kuwa tunaomba mapingamizi hayo yatupiliwe mbali na upande wetu ni hayo tu hatuna kingine..
Majaji wanaandika kidogo na kuulizana mawili matatu.
Tunasubiri sasa Rejoinder ya Mh. Lissu sijui ataifanya Leo au na yeye atahitaji muda arudi geto huko Magereza akaandae nondo za kuwajibu hawa jamaaa.
Binafsi sijaelewa Katuga alikuwa anasema nini kwa kiwango kikubwa sana.
Ngoja tuone ngoma bado ni mbichi.
Mahakama imemuuliza Mhe. Lissu amesema anaomba health break kidogo na azungumze na mawakili pia.
Mahakama imesema turudi saa saba na nusu kwa ajili ya rejoinder kutoka kwa Mh. Lissu.
Askari Magereza wameamuriwa wasije kumzuia Lissu kuonana na Mawakili kwasababu Lissu amelalamika kuwa Mawakili wanazuiwa kule lockup.
Tunatoka muda huu kwa ajili ya Break.
Tukutane saa saba na nusu mchana.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 29
Katuga anaendelea hapa.
Tumemsikia kwenye hati ya mashitaka anasema amemtaja Rais au Serikali au Makam au Waziri Mkuu. Anawataja katuga kama waheshimiwa kwa unyenyekevu sana.🤣🤣🤣
Sasa akisema kuwa hatujawataja hao watu ndio hati ya mashitaka haijaeleweka kwa mashitakiwa. Kuwataja au kutowataja ni suala la ushahidi.
Mahakama itakaposikiliza ushahidi ndio itajua hayo mengine yote.
Waheshimiwa mlikuwa mnaambiwa msema kuna uhaini hapa. Katika hatua hii mahakama haiwezi kujibu kuna uhaini au hakuna.
Haya maneno yanaleta uhaini au hayaleti ni suala la ushahidi.
Taarifa ya mashitaka inaweza kuwa na dosari either kwa muundo au kwa maudhui.
Sasa kuhusu hati ya mashitaka kutokuwataja watu sisi tumesema ali instigate public kwahiyo hapo public ilikuwepo na yeye alikuwepo mtoa maneno.
Hatuwezi kutaja public huyu na yule kwa sasa.
Nimewaona Wazee akina Nshala na Mpoki ni kama wamekasirika hivi wanaona kuna ujinga mkubwa sana unazungumzwa na huyu Bwana Katuga.
Katuga aninipa uvivu mpaka kuandika.😤
Anaendelea Katuga
Naomba tuijibie hoja nyingine alisema kwenye kesi ya Mataka mahakama ilisema kwa kuwa hakuna sheria iliyowekwa ya namna ya kuandaa mashitaka ya uhaini na ilishauri kufuata English Procedure.
Kwenye hili tunasema kifungu cha 138 cha CPA sura ya 20. Kinazungumzia jinsi ya kuandaa hati ya mashitaka kwenye makosa ya jinai.
Ingawa ukisoma kifungu hiki kinasema jinsi ya kuandaa hati ya mashitaka na pia kinashauri waandaaji wa hati za mashitaka kuandaa hati zinazoendana na second schedule ya sheria hii.
Hakuna mfano wa hati ya mashitaka ya kosa la treason na kutokuwepo na hati ya mfano haipekekei mtu atoke alipotoka aseme kwamba hakuna sheria mahsusi inayoeleza hati ya mashitaka inavyopaswa kuandaliwa.
Kifungu 138 ni kifungu mahsusi kinachoelezea kosa hili la uhaini.
Pia kuhusu Hati aliyosomewa tar. 10/05 na hii aliyosomewa juzi kuna maneno yameongezwa.
Ametumia maneno kuwa imekuwa amended na akasema kuwa hawa jamaa hawa hawajaonesha mamlaka ya kurekebisha hati ya mashitaka.
Hawajasema mahakama iliyowapa hayo mamlaka.
Hati ya mashitaka iliyopelekwa mahakama kabidhi ni hati inayopelekwa chini ya kifungu cha 262 cha CPA.
Kifungu kinasema mshitakiwa anapokuwa amekamatwa apelekwe mahakama ya chini akiwa na hati ya mashitaka inayopendekeza kosa lake.
Kwa tafsiri halisi hii sio actual hati ya mashitaka hii ni holding charge.
Hii sio hati halisi ni proposed charge. Kule chini ilikuwa ni uhaini na mbele yenu anashitakiwa na uhaini.
Anaendelea Katuga:
DPP atakapojirishisha ushahidi upo wa kutosha ataandaa au atalazimisha kuandaliwa hati ya mashitaka na ataiwasilisha Mahakama kuu pamoja na mashahidi.
Hajasema huruhusiwi kubadilisha hati ya mashitaka kwa mujibu wa kifungu gani na ingawa nikikumbuka alisema yeye ni Wakili wa miaka 23.
Pingamizi la pili alisema hati ya mashitaka haiwezi kutibika kwasababu viambata vyake havijachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Hati ya mashitaka inampa taarifa ya kosa lake na kuwapa jukumu upande wa mashitaka kuthibitisha pasipo kuacha shaka hiyo hati waliyomsomea mshitakiwa.
Kwenye hoja hiyo mshitakiwa hakuiambia mahakama kuwa hati ya mashitaka ili iwe valid lazima iambatane na orodha ya mashahidi.
Kwa vile hakusema ni wasilisho letu kuwa alikuwa sahihi kabisa kutokusema.
Upande wa jamhuri tunasema kuwa hati ya mashitaka ni nyaraka inayojitegemea na imetengenezwa kwa mujibu wa kifungu cha 138 cha CPA na hakuna mahali inaposema hati ya mashitaka itakuwa pamoja na hayo maelezo ya mashahidi. Hili ni jambo jipya.
Waheshimiwa majaji suala la maelezo ya mashahidi kuambatana na hati ya amshitaja ya mahakama kuu imeanza kuonekana kwenye kifungu cha 262(6), 263(2).
Part 30 itanendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.