THE EMBASSY ENGAGES AMDA INTERNATIONAL MEDICAL INFORMATION CENTER ON HEALTHCARE SUPPORT SERVICES
The Embassy held a meeting with representatives of AMDA International Medical Information Center. The discussions focused on the organization’s work in providing free medical consultation, interpretation, and appointment support services to foreign residents in Japan, particularly those facing language barriers in accessing healthcare.
The Embassy welcomed the initiative and acknowledged its importance in supporting the welfare of Tanzanian nationals and other foreign communities living in Japan. In this regard, the Embassy agreed to disseminate information about AMDA’s services to the Tanzanian diaspora to enhance awareness and access to these important services.
The Embassy also looks forward to continued engagement with the organization in promoting the well-being of Tanzanians residing in Japan.
AMBASSADOR MUTATEMBWA VISITS SOKA UNIVERSITY TO STRENGTHEN ACADEMIC COOPERATION
Ambassador Anderson Mutatembwa visited Soka University, where he held discussions with Vice President Professor Akio Nishiura. The purpose of the meeting was to strengthen existing cooperation and explore new areas of collaboration.
Soka University, established in 1971 by Daisaku Ikeda, currently hosts over 6,000 students. The university has been teaching Swahili and, since 1991, has organized annual Swahili speech contests, significantly contributing to the global promotion of the language.
The Ambassador commended the university for its efforts in promoting Kiswahili through educational initiatives, speech competitions, participation in World Kiswahili Language Day 2025, and collaboration with the Embassy, including the SADC Lecture Series. He also proposed establishing formal academic partnerships between Soka University and Tanzanian universities, particularly in the fields of language and cultural studies. This proposal was well received, with the university expressing its readiness to collaborate.
FOLLOW-UP DISCUSSIONS WITH FUJITA CORPORATION ON TANZANIA’S REAL ESTATE AND INFRASTRUCTURE OPPORTUNITIES
The Embassy held a meeting at the Chancery with representatives of Fujita Corporation, a Japanese company specializing in construction, housing, and urban development. Discussions focused on follow-up to the mission of Japan International Association for the Industry of Urban Development, Building and Housing (JUBH) member companies to Tanzania in July 2025, particularly in relation to opportunities in real estate and housing development.
The company informed that its planned follow-up visits to Tanzania, which had been scheduled for November 2025 to engage further with the National Housing Corporation (NHC), was postponed. However, it expressed continued interest in undertaking the visit in the near future.
In addition, Fujita Corporation highlighted its ongoing involvement in infrastructure development in Tanzania, including the construction of the Dodoma Inner Ring Road, underscoring its continued commitment to supporting the country’s infrastructure and urban development agenda.
The Embassy encouraged the company to sustain its engagement in Tanzania, particularly in affordable housing and integrated urban development projects, and reaffirmed its readiness to facilitate coordination with relevant institutions to support the realization of these initiatives.
DIPLOMATIC ENGAGEMENT ON JAPAN’S CANDIDATURE TO THE UN HUMAN RIGHTS COMMITTEE (2026–2030)
The Embassy welcomed a delegation from the Ministry of Foreign Affairs of Japan; and shared information regarding Japan’s candidate, Prof. Teraya Koji, who is seeking re-election to the United Nations Human Rights Committee (CCPR) for the 2026–2030 term.
The Embassy received the request and has taken it forward for consideration in line with established procedures. The election is scheduled to take place in New York, United States of America, in June 2026. Representing the Embassy was Ms. Edna Dioniz Chuku, Counsellor of Economic Affairs, and Mr. Hosea Chikolongo, Political and Cultural Attaché.
H.E. Ambassador of the United Republic of Tanzania, Anderson Mutatembwa, met with President Kyosuke Nagata of the University of Tsukuba to strengthen academic collaboration and bilateral ties.
🇹🇿🇯🇵
UBALOZI WAPOKEA UJUMBE WA KAMPUNI YA SPRIX KUJADILI PROGRAMU ZA ELIMU YA TEHAMA
Ubalozi ulipokea ujumbe wa wawakilishi kutoka SPRIX, ambapo mazungumzo yalijikita katika programu za elimu ya TEHAMA kwa shule za msingi na sekondari. Katika mazungumzo hayo, kampuni hiyo ilieleza dhamira yake ya kuanzisha programu hizo nchini Tanzania, kwa lengo la kuchangia maendeleo ya elimu ya kidijitali na ujuzi kwa wanafunzi.
UBALOZI WATEMBELEA TAMA ZOO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UTALII
Ubalozi ulitembelea Tama Zoological Park iliyopo jijini Tokyo, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya utalii na uhifadhi wa wanyamapori. Katika ziara hiyo, pande zote mbili zilijadiliana kuhusu uwezekano wa kushirikiana katika kubadilishana uzoefu na utaalamu, hususan katika maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori, utalii wa ikolojia (eco-tourism), pamoja na programu za elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira na viumbe hai.
UBALOZI WAPOKEA MWAKILISHI WA KAMPUNI YA SUMITOMO KUJADILI USHIRIKIANO NA TANZANIA
Ubalozi wapokea mwakilishi kutoka Sumitomo Corporation aliyefanya ziara Ubalozini kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano kati ya kampuni hiyo na Tanzania. Mazungumzo yalijikita katika fursa mbalimbali za uwekezaji na ushirikiano, hususan sekta za maendeleo ya uchumi, biashara na miundombinu.
UBALOZI WAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA PHOENIX YA JAPAN WANAOJISHUGHULISHA NA BIASHARA YA MAGARI
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan ulifanya mazungumzo na Phoenix, kampuni inayojihusisha na uuzaji na usafirishaji wa magari.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili fursa za biashara na ushirikiano katika sekta ya magari, hususan usafirishaji wa magari kwenda Tanzania. Aidha, ilielezwa kuwa kampuni hiyo tayari inafanya biashara zake nchini Tanzania na ni miongoni mwa wanachama wa Japan Used Motor Vehicle Exporters Association (JUMVEA).
Ubalozi uliwahakikishia kuwa Tanzania inaendelea kutoa mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji, na kuonesha utayari wa kuendelea kushirikiana na kampuni hiyo katika kukuza biashara yenye manufaa kwa pande zote mbili.
UBALOZI WAPOKEA UJUMBE WA JAPAN INTERNATIONAL COOPERATION AGENCY KUMTAMBULISHA MSHAURI WA UTALII ZANZIBAR (JICA TOURISM ADVISOR)
Ubalozi ulipokea wawakilishi watatu kutoka Japan International Cooperation Agency (JICA) waliomtambulisha Bi. Kana Matsuzaki, Afisa Mshauri wa JICA wa masuala ya utalii endelevu ambaye ataanza rasmi majukumu yake mwezi Mei 2026 katika Wizara ya Utalii na Urithi ya Zanzibar kwa kipindi cha miaka miwili.
Katika mazungumzo hayo, ujumbe wa JICA ulieleza kuwa jukumu la mtaalamu huyo litajikita katika kuimarisha uwezo wa taasisi za utalii Zanzibar, kukuza ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, pamoja na kusaidia kuandaa mikakati na ramani ya utekelezaji wa miradi ya muda mfupi itakayochochea maendeleo ya utalii endelevu. Aidha, alieleza dhamira yake ya kujifunza kwa kina mazingira ya sekta ya utalii Zanzibar ili kubaini maeneo ya kipaumbele yatakayohitaji maboresho na kuanzisha programu za mafunzo kwa wadau husika.
Ubalozi uliukaribisha ujio wa mtaalamu huyo na kueleza matarajio makubwa kuwa uwepo wake utaongeza nguvu katika kuimarisha ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Japan, hususan katika sekta ya utalii Zanzibar. Ubalozi ulisisitiza umuhimu wa kuzingatia utalii endelevu sambamba na fursa zilizopo katika uchumi wa buluu, ikiwemo uvuvi wa bahari kuu, maendeleo ya bandari, pamoja na uwekezaji wa kimkakati unaohusiana na sekta ya utalii.
BALOZI ANDERSON MUTATEMBWA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA CHUO KIKUU CHA KILIMO TOKYO (TOKYO NODAI)
🇹🇿🇯🇵
Balozi Anderson Mutatembwa alifanya mazungumzo na Rais wa Tokyo University of Agriculture (Tokyo NODAI), Dkt. Fumio Eguchi, wakati wa ziara yake ya kikazi katika chuo hicho.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Eguchi alieleza shukrani zake za dhati kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tokyo NODAI na Sokoine University of Agriculture (SUA), hususan kufuatia makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa mwaka 2009. Alibainisha kuwa ushirikiano huo umeendelea kuzaa matunda kupitia programu za kubadilishana wanafunzi, utoaji wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka SUA, pamoja na ushiriki endelevu wa wanafunzi hao katika mkutano wa kimataifa wa wanafunzi kuhusu chakula, kilimo na mazingira unaofanyika kila mwaka.
Aidha, Dkt. Eguchi alielezea muhimu wa programu ya Global Agri-Nutrition Leaders Programme katika kukuza wataalamu wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za kimataifa katika sekta ya kilimo na lishe. Alieleza kuwa chuo hicho kimejikita katika dhana ya “Practical Science,” inayolenga kuunganisha nadharia na vitendo katika kujenga ujuzi wa wahitimu.
Kwa upande wake, Balozi Mutatembwa alishukuru kwa ushirikiano huo na kupongeza mchango wa Tokyo NODAI katika kukuza rasilimali watu wa Tanzania kupitia elimu ya kilimo. Alibainisha umuhimu wa kuendeleza na kupanua zaidi ushirikiano huo, hususan katika maeneo ya utafiti, ubunifu na mafunzo ya vitendo yatakayochangia maendeleo ya sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Mazungumzo hayo yalihitimishwa kwa pande zote mbili kueleza nia ya kuendeleza ushirikiano huo wa muda mrefu kwa manufaa ya pande zote mbili.
BALOZI ANDERSON MUTATEMBWA AFANYA ZIARA CHUO KIKUU CHA SOPHIA KILICHOPO TOKYO NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS WA CHUO HICHO
Mheshimiwa Anderson Mutatembwa alifanya ziara katika Sophia University kilichopo Tokyo, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa chuo hicho, Profesa Mariko Iijima.
Katika mazungumzo hayo, Balozi alieleza kuwa madhumuni ya ziara hiyo yalikuwa ni kujitambulisha pamoja na kukishukuru chuo hicho kwa ushirikiano wake mzuri na Sokoine University of Agriculture (SUA). Aidha, alipongeza juhudi za chuo hicho katika kufundisha lugha ya Kiswahili pamoja na ushiriki wake katika maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani mwaka 2025.
Balozi Mutatembwa alitumia fursa hiyo kuomba kuimarishwa zaidi kwa ushirikiano uliopo, ikiwemo kupanua wigo wa ushirikiano kwa kushirikisha vyuo vingine vya Tanzania, hususan vilivyopo Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar. Alisisitiza umuhimu wa kuendeleza ufundishaji wa lugha ya Kiswahili pamoja na kufanya tafiti za pamoja katika masuala ya lugha na utamaduni.
Kwa upande wake, Profesa Iijima alipokea mapendekezo hayo na kuonesha utayari wa Sophia University kuanzisha ushirikiano na vyuo vingine vya Tanzania katika programu za lugha ya Kiswahili. Aidha, alieleza kuwa kuna fursa ya kupanua ushirikiano katika mafunzo ya lugha ya Kijapani kupitia ubadilishanaji wa wahadhiri na wanafunzi, pamoja na kufanya tafiti za pamoja zinazohusu lugha na utamaduni.
UBALOZI WAPOKEA MKURUGENZI WA JIJI LA YOKOHAMA NA UJUMBE WAKE KUJADILI USHIRIKIANO NA JIJI LA DAR ES SALAAM 🇹🇿🇯🇵
Ubalozi ulipokea ujumbe wa wawakilishi watatu kutoka Yokohama, ulioongozwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa wa jiji hilo, Bi. Maruyama Akiko. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuendeleza majadiliano kuhusu kuanzisha ushirikiano kati ya Jiji la Yokohama na Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, ujumbe wa Yokohama ulikumbushia maendeleo yaliyofikiwa katika rasimu ya Hati ya Ushirikiano (Memorandum of Understanding – MoU) kati ya majiji hayo mawili. Aidha, waliwasilisha ombi la kuandaliwa kwa mazungumzo ya awali kati ya wataalamu wa Dar es Salaam na Yokohama, kwa lengo la kujitambulisha, kubadilishana uzoefu, pamoja na kubaini maeneo ya kipaumbele kwa ajili ya ushirikiano huo.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuweka msingi imara wa ushirikiano wa muda mrefu kati ya majiji hayo mawili, hususan katika maeneo ya maendeleo ya miji, miundombinu, mazingira na huduma za jamii.
Ubalozi ulieleza utayari wake wa kuendelea kuratibu na kusaidia juhudi hizo ili kuhakikisha ushirikiano huo unatekelezwa kwa mafanikio na kuleta manufaa kwa pande zote mbili.
UBALOZI WAPOKEA UJUMBE WA ASASI YA CMC KUJADILI USHIRIKIANO WA KUELIMISHA WANAFUNZI MASHULENI KUHUSU MASUALA YA KIMATAIFA
Tarehe 27 Aprili 2026, Ubalozi ulipokea ujumbe kutoka Children Meet Countries (CMC) yenye makao makuu jijini Tokyo. Taasisi hiyo imekuwa ikiandaa warsha na semina maalum mashuleni kwa lengo la kuwapa wanafunzi wa Japan uelewa kuhusu masuala ya kimataifa na tamaduni za nchi mbalimbali.
Akipokea ujumbe huo kwa niaba ya Mheshimiwa Balozi Anderson Mutatembwa, Bi. Edna Dioniz Chuku, Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi (Counselor Economic Affairs), aliipongeza taasisi ya CMC kwa jitihada zake za kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa uelewa wa kimataifa. Aidha, alieleza utayari wa Ubalozi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kuandaa programu zitakazosaidia kuitangaza Tanzania, hususan katika maeneo ya utalii, utamaduni, elimu na fursa za biashara kwa bidhaa za Tanzania nchini Japan.
Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilikubaliana kuendelea kushirikiana katika kuandaa warsha na semina zitakazohusisha wanafunzi wa Japan, kwa kuzingatia mada mbalimbali zinazohusu Tanzania, ikiwemo historia, utamaduni, lugha ya Kiswahili pamoja na vivutio vya utalii. Lengo ni kuongeza uelewa na kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Japan.
BALOZI ANDERSON MUTATEMBWA AFANYA ZIARA KWENYE TAASISI YA UTAFITI WA ANGA ZA JUU YA JAPAN (JAXA) INAYOTARAJIWA KURUSHA SATELITE YA KWANZA YA TANZANIA
Tarehe 30 Aprili 2026, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan, Mheshimiwa Anderson Mutatembwa, alifanya ziara kwenye Taasisi ya Utafiti wa Anga za Juu ya Japan, (Japan Aerospace Exploration Agency - JAXA). Lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta ya anga za juu, hususan katika utekelezaji wa mradi wa kurusha satelaiti ya kwanza ya Tanzania (TanzaniteSat-1).
Mheshimiwa Balozi alipokelewa na viongozi wa JAXA wakiongozwa na Makamu wa Rais wa taasisi hiyo, Bw. ISHII Yasuo.
Pande zote zilijadili maendeleo ya Mradi wa Satelaiti ya Tanzania (TanzaniteSat-1); JAXA ikieleza kuwa inaendelea kushirikiana kwa karibu na timu ya Tanzania kupitia mikutano ya mara kwa mara ya kiufundi, na kubainisha kuwa uzinduzi wa satelaiti unatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ujao, kwa kutegemea ukamilishaji wa hatua za mwisho za maandalizi.
Makamu wa Rais wa JAXA alieleza historia na mafanikio ya Japan kwenye sekta ya anga za juu, pamoja na nafasi yao katika kuratibu na kutekeleza miradi ya sekta hiyo; na mchango wa JAXA katika kukuza ubunifu na ushirikiano wa kimataifa katika sekta hiyo. Aidha, alibainisha fursa mbalimbali za ushirikiano kwa nchi zinazoendelea kupitia Programu ya KiboCube, inayolenga kusaidia nchi zisizo na uwezo wa kurusha satelaiti kupata uzoefu wa vitendo katika teknolojia hiyo.
Kwa upande wake, Balozi Mutatembwa alielezea dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na Japan katika teknolojia ya anga za juu na kufuatilia maendeleo ya Mradi wa TanzaniteSat-1. Alieleza kuwa mradi huo ni wa kimkakati kwa maendeleo ya Taifa, hususan katika ufuatiliaji wa mazingira na majanga, ukusanyaji wa taarifa kupitia earth observation, pamoja na kuimarisha sekta za kilimo, mawasiliano na usimamizi wa rasilimali. Aidha, alitoa rai kwa JAXA kuendelea kuwajengea uwezo wa wataalamu wa Tanzania kupitia mafunzo ya kisayansi na kiufundi.
Baada ya mazungumzo, Mheshimiwa Balozi alipata fursa ya kutembelea Kituo cha Anga cha Tsukuba, ambapo alijionea miundombinu ya kisasa ya uendeshaji wa Moduli ya Kibo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (International Space Station - ISS), maabara za majaribio ya satelaiti pamoja na maonesho ya teknolojia za anga za juu.
H.E. ANDERSON MUTATEMBWA HELD DISCUSSIONS ON SAMURAI BOND WITH THE CEO OF INTERCONTINENTAL TRADING COMPANY LTD. (GLOBAL FINANCE)
H.E. Ambassador Anderson Mutatembwa received a delegation from Intercontinental Trading Company Ltd. (Global Finance), led by its Chief Executive Officer, Mr. Takahiro Hosojima.
The delegation introduced their company as a Tokyo-based financial advisory firm working closely with African governments and institutions. Mr. Hosojima, who brings over 30 years of experience including previous service with the Japan Bank for International Cooperation (JBIC), provided an overview of their expertise in structuring and facilitating sovereign financing.
Discussions centered on the potential issuance of a Samurai Bond for Tanzania as an innovative mechanism to access financing from the Japanese capital market. The delegation shared recent examples of Samurai Bond issuances by some African countries highlighting the role of Japanese financial institutions and credit enhancement mechanisms, including guarantees from entities such as JBIC, Nippon Export and Investment Insurance (NEXI), and the Africa Finance Corporation, in attracting Japanese investors.
The meeting provided an opportunity to exchange views on the feasibility, structure, and potential benefits of such financing for Tanzania, particularly in supporting infrastructure development and sustainable economic growth.
@mfa_tanzania@mofURT
THE EMBASSY PARTICIPATES IN THE JICA KIZUNA PROGRAM - FINAL PRESENTATION ON HUMAN RESOURCES DEVELOPMENT IN THE MINING SECTOR
🇹🇿🇯🇵
The Embassy participated in the Final Presentation of the Japan International Cooperation Agency Program for Human Resources Development in the Mining Sector (KIZUNA Program), during which 20 participants presented their research findings and shared their academic and professional experiences gained during their studies in Japan.
Among the presenters were three participants from Tanzania, including two PhD candidates who studied at Kyushu University and Kyoto University, and one Master’s degree graduate from Hokkaido University.
The Embassy was represented at the event by Ms. Edna Dioniz Chuku, Counsellor for Economic Affairs, who attended the session and engaged with the participants and organizers on areas of mutual interest, particularly in strengthening Tanzania’s human resource capacity in the mining sector through continued collaboration with Japan International Cooperation Agency.
@mfa_tanzania@jica_direct_en
BALOZI ANDERSON MUTATEMBWA AKUTANA NA JUMUIYA YA WAJITOLEA WA JAPAN NCHINI TANZANIA (JAPAN OVERSEAS COOPERATION VOLUNTEERS – JOCV)
🇹🇿🇯🇵
Mheshimiwa Balozi Anderson Mutatembwa alikutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wajapani waliojitolea nchini Tanzania (Japan Overseas Cooperation Volunteers - JOCV). Jumuiya hiyo inayojulikana, Waswahili No Kai, ilianzishwa mwaka 1986 kwa lengo la kuwakutanisha marafiki wa Tanzania waliopo Japan, hususan Wajapani waliowahi kuishi, kufanya kazi au kushiriki shughuli mbalimbali nchini Tanzania.
Waswahili No Kai ni jumuiya inayojumuisha wanachama wanaotoka katika nyanja mbalimbali, wakiwemo washiriki wa programu ya kujitolea ya Japan International Cooperation Agency (JICA) ijulikanayo kama Japan Overseas Cooperation Volunteers - JOCV, pamoja na wadau wa biashara, elimu, utamaduni na miradi ya maendeleo inayohusiana na Tanzania. Kundi hili lina wanachama takribani 400 na linaendelea kuwa daraja muhimu la kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Kundi hili pia lina mchango mkubwa katika kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Kitanzania, kuwezesha kubadilishana uzoefu na maarifa, pamoja na kuunga mkono shughuli za maendeleo na ushirikiano wa kijamii kati ya mataifa haya mawili.
Akizungumza katika mkutano huo, Mheshimiwa Balozi Anderson Mutatembwa alitoa shukrani na pongezi za dhati kwa viongozi wa Waswahili No Kai kwa juhudi zao za kuanzisha na kuratibu kundi hilo muhimu. Alisisitiza kuwa kupitia uongozi wao mahiri, wamefanikiwa kuwaleta pamoja watu wenye mapenzi ya dhati kwa Tanzania na kuunda jukwaa lenye mchango mkubwa katika kuimarisha mahusiano ya watu kwa watu (people-to-people relations).
Aidha, aliwapongeza kwa kuendeleza ari ya kujitolea na ushirikiano unaochangia maendeleo ya Tanzania, akibainisha kuwa mchango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers unaendelea kuwa nguzo muhimu katika kuimarisha urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Japan na unastahili kuthaminiwa kwa kiwango cha juu.
@mfa_tanzania@jica_direct_en@jica_direct
BALOZI ANDERSON MUTATEMBWA ATEMBELEA SHIRIKA LA TAIFA LA UTANGAZAJI LA JAPAN (NHK WORLD) NA KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA HABARI 🇹🇿🇯🇵
Balozi Anderson Mutatembwa alitembelea Makao Makuu ya Shirika la Taifa la Utangazaji la Japan (NHK World) jijini Tokyo, ambapo alifanya mazungumzo na Makamu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano katika sekta ya habari kati ya Tanzania na Japan, pamoja na kuangazia fursa zilizopo katika kukuza uelewa wa kimataifa kuhusu Tanzania kupitia vyombo vya habari vya Japan.
Baada ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi alipata wasaa wa kutembezwa katika ofisi za Shirika hilo na kujionea shughuli mbalimbali za uendeshaji na uzalishaji wa vipindi. Aidha, alipata fursa ya kufanya mahojiano maalum, ambapo alizungumzia uhusiano wa Tanzania na Japan, fursa za uwekezaji na biashara, uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili nchini Japan, pamoja na manufaa ya kuendeleza ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
@mfa_tanzania@TBConlineTZ@WizaraSanaa