Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini, amesema Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, anapaswa kuachiwa huru, lakini hatua hiyo isitokane na mashinikizo ya jumuiya za kimataifa bali iwe uamuzi unaotokana na busara, maridhiano na mifumo ya Tanzania yenyewe.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 14, 2026 Jijini Dar Es Salaam, Selasini amesema Tanzania imejijengea sifa ya kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo na amani, hivyo haipaswi kufikia hatua ya kuonekana inalazimishwa na mataifa au taasisi za nje katika kushughulikia suala la Lissu.
"Sisi tunamuona mwenzetu ni shujaa sana, lakini ndani ya moyo kuna maumivu. Fikiria familia yake, mke na watoto. Sisi tunafurahia yeye kuwa ndani lakini yale maumivu hatuyahisi. Mimi namuomba Rais Samia hili suala la Lissu lifike mwisho, sio kwa sababu tumeambiwa na Jumuiya ya Madola, bali kwa sababu Tanzania imejengwa katika kusuluhisha mambo kwa amani. Lissu kuwa magerezani sio sifa kwa nchi," amesema.
Kauli hiyo inakuja wakati kumekuwa na wito unaoongezeka kutoka kwa jumuiya mbalimbali za kimataifa kuhusu hatima ya kesi ya Lissu, ivi karibuni, Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ikiungana na Taasisi na Jumuiya nyingine za Kimataifa ikiwemo Bunge la Ulaya, ikitoa tamko la kutaka Lissu kuachiwa ndani ya siku 30 na kueleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa kesi hiyo na kutoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu, utawala wa sheria na mchakato wa haki.
Kwa upande wake, Serikali ya Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa kesi ya Lissu ipo mikononi mwa vyombo vya sheria na kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria. Serikali imekuwa ikieleza mara kwa mara kuwa haiwezi kuingilia mchakato wa mahakama, huku ikitaja kuwa nchi ina mfumo huru wa utoaji haki ambao unapaswa kuheshimiwa bila kuingiliwa na shinikizo la kisiasa.
CHADEMA, kwa upande wake, imeendelea kushikilia msimamo wake kwamba Lissu hana hatia na inataka aachiwe huru mara moja. Chama hicho kimekuwa kikieleza kuwa mashtaka yanayomkabili yana mwelekeo wa kisiasa na kimekuwa kikitoa wito kwa Serikali kumaliza suala hilo kwa njia itakayorejesha maridhiano, kuheshimu haki za binadamu na kulinda misingi ya demokrasia nchini.
🚨 EXCLUSIVE: Manchester United in advanced talks to sign Youri Tielemans from Aston Villa. All parties in contact as #MUFC try to finalise - 29yo midfielder keen on move. Ederson deal off for now; #MUFC may look to revisit later this summer @TheAthleticFC https://t.co/KbWwD1jxov
🚨⚠️ EXCL: Éderson to Manchester United, deal OFF and considered as collapsed as Man Utd informed Atalanta.
Atalanta believe Éderson is 100% fit and will welcome the midfielder back as part of their squad, as Man United changed their plans.
Éderson won’t join #MUFC.