The only time you are sure to lose is when you quit. No aspirations to quit the game . Haijalishi itakuwa ngumu kiasi gani lakini bado tutaishi kwenye ndoto zetu, wakati wetu ukifika na sisi tutafika tu.
Hakikisha unapoondoka kwa mtu au unapoondoka kwenye taasisi fulani usibamize milango, wakati mwengine maisha yana siri kubwa sana. Mambo yakiwa magumu viporo havitupwi bali vinapashwa 😂
“Stay humble even when you’re are at the top, because you’re one step away from being back to the bottom. Never forget where you started “Christopher Wallace (The Notorious B.I.G)
Kulalamika sana ni njia nyengine ya kulia, kaza firigisi mwanetu…maisha sio lelemama na lawama kwetu cheo, maana hata ufanyaje huwezi kumridhisha kila mmoja. Dunia uwanja wa fujo hata usipofanya fujo basi utafanyiwa 😂😂
“Walinifungulia mlango katika career yangu, kitu ambacho sikufanyiwa nchini kwetu Ufaransa. Nahisi nina deni kubwa kwao “ Antoine Griezman 🇫🇷(Kuelekea fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Sociedad)
Kukata tamaa ni kosa la jinai kwa sababu hata jua linapozama kesho huchomoza tena. Licha ya wengi kumkatia tamaa baada ya kuchemka Chelsea na Everton lakini Super Frank amekuwa mkombozi wa Ng’ambo pale Coventry City kwa kufanikiwa kuirudisha EPL baada ya miaka 25 .