"Uchumi wetu unakua kwa kasi, biashara zinazidi kufunguka kwa namna hiyo hiyo mfumo wetu wa kodi hauna budi kukamilika kuendana na wakati tulio nao. Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka" Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"Wafanyabiashara wanaotekeleza wajibu wao wa kisheria na kizalendo wa kulipa kodi kwa uaminifu na kwa wakati wamejijengea heshima hii, na sina budi kuwapa heshima hii (Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora)" Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya picha aliposhiriki tukio la utoaji wa Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora sambamba na Maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam Leo Julai 01,206.
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel:
Ikulu Tanzania na Tovuti: https://t.co/f1VkCZ78Xo
#TanzaniaYetuSote#NchiYetuKwanza
*KIFO CHA DEREVA WA HECHE NI MWENDELEZO WA CHADEMA KUUA ILI KUPATA HURUMA*
Anaandika Dkt. Silaa juu ya utata wa matukio ya utekaji na mauaji ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo yanayopangwa na kuratibiwa kwa siri kubwa.*
TUACHE VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA IFANYE KAZI YAKE ....
Ila Ushauri Muhimu haikubariki Dereva wa VIP kwenye Chama akalale Gesti za Vichochoroni hata akipata shida ya kiafya anapataje huduma kwa haraka..Tupunguze Pombe tukiwa Field.
@godbless_lema@MariaSTsehai@HecheJohn
Viongozi na wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam,tarehe 30 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mfanyabiashara kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group,Alhaji Aliko Dangote pamoja na Ujumbe wake, Ikulu Jijini Dar es Salaam,tarehe 28 Juni, 2026
Umoja wa Mabunge Duniani @ipu inaenda kubadilishana uongozi wa Katibu Mkuu wa Umoja huo ambapo Bwana Martin Chungong anamaliza muda wake wa uongozi na atamkabidhi Balozi Anda Filip mwisho wa mwezi June. Rais wa IPU @TuliaAckson anatarajiwa kuendesha kikao cha Kamati ya uongozi na atashuhudia mabadilishano haya ya kihistoria ya uongozi ambapo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 130 Katibu Mkuu ni mwanamke. Pamoja na hayo, Tanzania 🇹🇿 itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa IPU Mkoani Arusha mwezi Oktoba na katika ajenda za mkutano huo ni pamoja na uchaguzi wa Rais wa IPU atakayemrithi Dr Tulia ambaye pia ni Mtanzania wa kwanza kushika nafasi ya Urais wa IPU. Historia inaenda kuandikwa Tanzania 🇹🇿 ambapo wanawake watatu (the triple three) wataongoza Mkutano huu ambapo Mheshimiwa Rais wa JMT Dkt. Samia Suluhu Hassan ndio mwenyeji wa Mkutano huu unaotarajiwa kuleta Maspika na wabunge wa Dunia zaidi ya Elfu Mbili. Balozi Anda Filip ataongoza Mkutano wake wa kwanza kama Katibu Mkuu huku Mhe. Dkt Tulia akiongoza kikao chake cha mwisho kama Rais wa IPU. #ipu153arusha🇹🇿 #thetriplethree🇹🇿 #womenleaders
ZIARA YA MWENEZI CCM TAIFA MKOANI PWANI.
Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Ndg KENANI LABAN KIHONGOSI Mkoani Pwani:-
👇🏿
✅KIBAHA
Tarehe 01 Julai 2026
✅RUFIJI
Tarehe 02 Julai 2026
✅MKURANGA
Tarehe 03 Julai 2026
MTUMISHI WA WOTE💪🏿
#ChamaKipoKazini
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Dkt, Netumbo Nandi-Ndaitwah baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa, tarehe 20 Juni, 2026.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Mhe. Petro Magoti amesema vikosi vya ulinzi na usalama Wilayani humo vimejipanga kudhibiti maandamano yanayotajwa, kuratibiwa na kuhamasishwa kufanyika Julai 07, 2026.
Dc Magoti amwsema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge katika baraza maalumu la Madiwani wa Halmashauri hiyo, wakijadili kuhusu ripoti ya mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka 2024/25.
"Nikuhakikishie Mkuu wa Mkoa, hakuna hata mmbu atakayeandamana hiyo tarehe saba." Amesema Dc Magoti.
SGR IMESAFIRISHA ZAIDI YA ABIRIA MILIONI 6, TAKRIBANI ABIRIA 11,000 KWA SIKU - PROF. MBARAWA
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu ya usafiri inayolenga kuimarisha huduma za usafirishaji katika Ushoroba wa Kati (Central Corridor), huku mafanikio makubwa yakionekana katika reli ya kisasa ya SGR, Bandari ya Dar es Salaam na usafiri wa majini.
Akizungumza katika Mkutano wa 15 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ushoroba wa Kati (ICM) unaofanyika Dar es Salaam leo Juni 18, 2026, Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR katika sehemu mbalimbali za Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kigoma pamoja na Uvinza hadi Musongati nchini Burundi utaongeza kwa kiasi kikubwa muunganiko wa kikanda, biashara na ushirikiano wa kiuchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema tangu kuanza kwa huduma za usafiri wa abiria wa SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma mwezi Juni 2024, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanikiwa kusafirisha zaidi ya abiria milioni sita.
Kwa sasa, safari nane hufanyika kila siku kati ya Dar es Salaam na Dodoma, huku safari tatu zikifanyika kati ya Dar es Salaam na Morogoro, zikisafirisha wastani wa abiria kati ya 8,000 na 11,000 kwa siku.
Prof. Mbarawa ameeleza kuwa mafanikio hayo yanaonesha wazi kuwa SGR imekuwa chachu ya mageuzi katika sekta ya usafiri nchini Tanzania kwa kuwavutia wananchi wengi kutumia reli badala ya usafiri wa barabara na anga.
Aidha, amesema TRC ilianza rasmi huduma za usafirishaji mizigo kupitia SGR mwezi Juni 2025 kutoka Dar es Salaam hadi Ihumwa mkoani Dodoma.
Pia, shirika hilo liko katika hatua za mwisho za ujenzi wa kituo cha kubadilishia mizigo cha Bahi, ambacho kitaiwezesha mizigo kuhamishwa kwa urahisi kutoka reli ya kisasa kwenda reli ya zamani kwa usafirishaji kuelekea Isaka na maeneo mengine.
Kuhusu Reli ya TAZARA, Prof. Mbarawa amesema Tanzania na Zambia zilitia saini makubaliano mwezi Septemba 2025 ya kuikabidhi reli hiyo kwa mwekezaji kutoka China kwa mfumo wa ubia, hatua inayotarajiwa kuifufua reli hiyo kupitia ukarabati mkubwa wa miundombinu na ununuzi wa vichwa na mabehewa mapya.
Katika sekta ya bandari, Waziri huyo amesema ushirikishwaji wa kampuni za DP World na Tanzania East Africa Gateway Limited katika usimamizi wa shughuli za makontena umeongeza ufanisi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam.
Amebainisha kuwa hadi Machi 2026, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imehudumia tani milioni 29.66 za mizigo ikilinganishwa na tani milioni 23.18 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita, sawa na ongezeko la asilimia 27.96.
Amesema Serikali inaendelea kuboresha mfumo wa uhamishaji mizigo kutoka bandarini kwa kuendeleza bandari kavu katika maeneo ya Kwala, Morogoro, Ihumwa, Isaka, Fela na Katosho ili kupunguza msongamano na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo.
Katika usafiri wa majini, Prof. Mbarawa amesema Serikali inaendelea na ukarabati wa meli za MV Mwongozo na MV Liemba katika Ziwa Tanganyika pamoja na ujenzi wa karakana ya kisasa ya meli na meli mpya ya mizigo aina ya Roll-on/Roll-off (Ro-Ro).
Kwa upande wa Ziwa Victoria, amesema Serikali inaendelea na ukarabati wa meli za MV Nyangumi na MV Clarias pamoja na ujenzi wa meli mpya ya MV New Mwanza na meli nyingine ya Ro-Ro kwa lengo la kuimarisha huduma za usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi katika ukanda huo.
Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ufanisi wa usafiri na kupunguza gharama za usafirishaji katika Ushoroba wa Kati ili kuongeza biashara, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi wanachama.