Saizi nikiongea kuna namna Mdomo unajivuta pembeni kwasababu ya MAPENGO niliyopata ukubwani.
Hii ni hali mpya inanikosesha raha, ila haitaweza kunizuia kuyaishi maisha yangu niliyozoea.
Naamini na nyie wanangu mtazoea kuniona kwenye hali hiyo. Hata mkinitainia kwa hilo pia mimi kwangu UNYAMA.
Hili kwangu ni dogo sana, wapo watu wamekatwa Miguu baada ya kukutana na wakoloni weusi kama mimi, leo mimi meno tuu mawili yamepotea niogope?
Maisha yataendelea kama KAWA. Hili jaribu Mungu alinipa akijua naliweza na kweli NITAISHI NALO mwanzo mwisho.🙏
Watanzania achaneni na Majizzo na wapuuzi wengine. Kwa hali ya sasa sio Majizzo tu hata Kusaga wiki ijayo atawaombea msamaha wasanii. Kwa sababu hizi
1. Radio & Tv zinakufa pia sio wasanii pekee
2. Serikali batili inahitaji Watanzania mrudi kuwa busy na wasanii ili wao waendelee na unyonyaji na uuaji.
3. Wasanii ndio tegemezi la CCM katika kuhamasisha Jamii, so wananchi mkiwapuuzia na kuwapotezea wasanii na serikali batili imepoteza nguvu juu ya wananchi.
4. Wanataka nchi irudi kwenye hali ya zamani, yani wananchi mko busy na wasanii na sio seriajli.