‼️IKITOKEA NIMETEKWA/KUPOTEZWA AU KUUWAWA, KINGAI NDO ATAKUWA MUHUSIKA NO. 1‼️
Nimepewa taarifa kwamba Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya jinai nchini (DCI) Ramadhan Kingai ametuma Team ya maofisa wa Polisi wanitafute popote nilipo, wanifikishe kwake nikiwa hai au maiti,
Kingai anadai nimedharau na kukejeli wito wa Jeshi la Polisi ambao waliutoa siku kadhaa zilizopita.
Team hiyo aliyoituma inaongozwa na ofisa wa Polisi Kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma jina lake ni Edward Pius Soteli wengine ni
1. Detective Juma Sadick Bahat, huyu Katolewa ofisi ya RPC wa Mtwara,
2. Detective David Edward Mabula huyu katolewa ofisi ya RPC wa Ruvuma.
3. Detective Eliud Peter Kivuyo, huyu katolewa ofisi ya RPC wa Iringa
4. Detective Ally Jamal Mganzo huyu katolewa ofisi ya RPC wa Kigoma
5. Detective David Sailevo Lukumay, huyu Katolewa ofisi ya RPC wa Tabora.
Serikali haram iko na mambo ya hovyo sana yani pesa kwa ajili ya kufanya maendeleo hakuna lakin pesa za kulipa watu ili watutafute na kututeka zipo za kutosha.🚮
YUKO WAPII?
2 Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI UTALIPONYA TAIFA.
BAK MWABUKUSI.
Ukitaka kujua hakuna Nchi Sikiliza mambo kama haya.
Watu walikua wnashangaa kwanini Bashite anaendesha gari mabilioni na misafara ya kutisha.
Watu walikua wanashangaa kwanini anaapa hata kudhuru au kuumiza watu aliosema “wanacheza na Urais wa mama”
Ukisikia wanasema tutamlinda kwa gharama yoyote unaelewa nini? Wataua. Watadhuru kumlinda ili na yeye awalinde katika uchafu huu.. you scratch my back i scratch yours.
Watu wanasema na kusikia utajiri mkubwa wa ghafla wa bwana Gerson, akiongea kwa kufoka kana kwamba Nchi ni yake.. kiburi kinatoka huku.
Yaani uwanja ulikadiriwa ujengwe kwa Tsh bilioni 187 alafu mkataba ukasainiwa wa Tsh bilioni 338!!!!
Alafu mzabuni alipatikana bila kushindanishwa au tenda kutangazwa!!!! Sijui Kama wengi tunaelewa maana ya hili jambo.
Tenda ikitangazwa makampuni ya ujenzi yakashindana bei ingekua chini zaidi, licha ya kwamba sheria ya manunuzi inakataza kutoa tenda bila ushindani, mtu mmoja au kikundi cha watu wachache wakaamua kuipa kampuni moja hiyo kazi bila ushindani!!! Hakuna anaejua kama kweli ni kampuni au ni wao wamechukua vibarua wanawalipa per day au ni kampuni ya mmoja wao ya mfukoni.
Yaani bei mara mbili ya ile iliyokadiriwa!!! Watanzania wanakufa mafuriko, hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme, hakuna shule bora wala hospital! Watu wanachezea fedha za wananchi kiasi hiki!!!
Morocco imejanga viwanja vya kisasa na vyenye ubora wa Kimataifa, viwanja hivyo vimetumika kwenye Afcon 2025 na vitatumika kwenye Kombe la dunia 2030. Bei ya chini kuliko hicho cha mafisadi na bora zaidi.
1.Khouribga stadium billioni 150
2.Stade Municipal de Nador & Shabiba Bilioni 200
3.Prince Moulay Abdellah Stadium USD 75 m sawa na bilioni 187.
Unaweza kutaja na vingine na vingine kwa mamia.
Huu ni ujambazi kwa Nchi yetu, na vijana mpo hamna kazi, ajira wala matumaini mnasema tunamuachia Mungu!!!!
Ukijiari iwe shamba au hata kwenye mtandao wanakuja kuchukua fedha yako kama kodi, ukinunua gari au bodaboda kodi ni mara mbili ya kununulia.. alafu pesa inachezewa hivi.
MPANGO NA SHERIA YEYOTE INAYOTUNGWA KWANJIA NA SABABU ZA KIBAGUZI NI UVUNJAJI WA SHERIA ,KATIBA NA MIKATABA YA KIMATAIFA.
Huwezi kuzungumzia kupatanisha kampuni mbili za kigeni ili zibaki kufaidi Ngorongoro halafu wakati huohuo ufikirie eti kutafuta suluhisho la kisheria kwa kuwaondoa wamasai Ngorongoro.
Hiyo itakuwa sheria ya kibaguzi na Kikaburu.
Hata ukitunga sheria itakuwa sheria haramu ya kibaguzi nankikaburu inayokiuka Haki ya Wamasai katika Ardhi yao.
Kipaumbele cha kwanza kwa ngorongoro ni kulinda haki na hadhi ya Wamasai katika Ardhi yao ya Asili.
Tunaweza kuweka utaratibu bora wa Ufugaji na Matumizi rafiki ya Ardhi. Ngorongoro is for Maasai .Siyo kwa ajili ya Mahotel na Wawindaji wa Kigeni.
Haki,Ukweli na Uwajibikaji vitaliponya Taifa.
BAK Mwabukusi.
Nduli Idd Amin Mama alituma wasaidizi wake Gereza la Ukonga.
Wakamwambia Mhe. Lissu kwamba limama lao lipo tayari kumsamehe Mhe. Lissu ila sharti lake ni moja akubali kuipeleka CHADEMA kwenye maridhiano.
Mhe. Lissu aliwauliza anisamehe kwa kosa gani wakati yeye ndo aliyenibambika hii kesi ya uwongo?
Mhe. Lissu aliwambia sihitaji anisamehe wala kupewa masharti kwamba ukitoka ufanye hivi ila nataka afute hii kesi kwasababu ni ya uwongo na yeye anajua na Dunia inajua kwamba mimi sio Muharifu.
So Nduli Idd Amin Mama anatumia kesi ya mchongo ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu ili kumkomoa ndo maana mpaka leo Mahakama ya Rufani haijapanga tarehe ya kuanza kusikiliza Rufaa ambayo imekatwa na Mawakili wa Serikali.
Nduli Idd Amin mama anadhan kwa kufanya hivi itafika muda Mhe. Lissu atampigia magoti na kukubali kuipeleka CHADEMA kwenye maridhiano uzuri Mhe. Lissu alishasema kama wanataka kumnyonga kwa hii kesi ya uwongo yupo tayari ila hatompigia magoti mtu yeyote.
Halafu hata hiyo kesi ya Mgawanyo wa mali za CHAMA na mazuio ya CHAMA kufanya shughuli zake za kisiasa ni muendelezo huo huo wa kublackmail Viongozi kwamba mkikubali kuingia kwenye maridhiano basi hizi kesi zote zitafutwa.
Nakumbuka wakati wa Uchaguzi Nduli Idd Amin mama na vibaraka wake walikuwa wanasema kwamba “CHADEMA wanajiona wao ni special sana wakati Tanzania Vyama vya upinzani viko vingi”
Sasa kama Vyama vya upinzani nchini viko vingi sana kwanini yupo Desperate, anahangaika na kutumia nguvu kubwa kiasi hiki kutaka CHADEMA ikubali kuingia kwenye maridhiano si akaridhiane na hivyo Vyama walivosema ni vingi???😂😂😂😂
Labda tumkumbushe tu Nduli Idd Amin Mama kwamba CHADEMA ni CHAMA CHA WANANCHI WA TANZANIA, IKO MIOYONI MWA WATU.
CHADEMA IMEBEBA MATUMAINI YA WATANZANIA WENGI.
CHADEMA NDO CHAMA PEKEE CHENYE LEGITIMACY KWENYE NCHI HII SO TUTAILINDA LEGITIMACY YETU KWA WIVU MKUBWA.