Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimiwatu, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Teddy Njau akielezea Muundo wa Taasisi kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi tarehe 17 Oktoba, 2025.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Teddy Njau akitoa neno la utangulizi kwa washiriki wa mafunzo ya awali kwa watumishi wapya wa ofisi hiyo. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Dodoma tarehe 6 Oktoba, 2025.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi akitoa hotuba kwa washiriki wa mafunzo ya awali kwa watumishi wapya wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 6 Oktoba ,2025.
S/SGT. Mussa Ntimizi akichangia Mada kuhusu changamoto za kimaadili kwa wanafunzi na ufumbuzi wake Mdahalo uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru tarehe 26 Agosti, 2025.
Bi. Florah Msilu ambaye ni mdau wa masuala ya maadili akichangia mada kuhusu Changamoto za kimaadili kwa Wanafunzi na ufumbuzi wake. Mdahalo huo ulifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru tarehe 26 Agosti, 2025.
Bi. Salama Ally ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha akichangia Mada katika Mdahalo kuhusu changamoto za kimaadili kwa Wanafunzi na ufumbuzi wake. Mdahalo huo umefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru tarehe 26 Agosti, 2025.
Bw. Gerald Mwaitebele Katibu Msaidizi , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini akifungua Mdahalo kuhusu changamoto za kimaaadili kwa Wanafunzi na ufumbuzi wake. Mdahalo huo umefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru tarehe 26 Agosti, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt. Vicent Mashinji akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa klabu ya Maadili ambao ni wanafunzi wa Shule Msingi Dodoma Makulu wakati alipotembelea Banda la Sekretarieti ya Maadili katika Maonesho ya Nanenane jijini Dodoma tarehe 4 Agosti 2025
NANE NANE 2025
Picha za matukio mbali mbali Wananchi wakiendelea kupata elimu na huduma katika banda la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati Dodoma Bi. Jasmin Awadhi akitoa elimu ya Maadili kwa Wananchi katika banda la ofisi hiyo kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma tarehe 3 Agosti, 2025.
Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili Bw. Waziri Kipacha akiteta jambo na viongozi wa kimila kutoka mikoa ya kusini waliofanya ziara Maadili kwa lengo la kushirikiana katika kukuza Maadlili nchini. Viongozi hao wamekutana tarehe 10 Julai, 2025 jijini Dodoma katika Ofisi za Maadili.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Kaskazini , Bw.Gerald Mwaitebele akitoa mada kuhusu Maadili kwa watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) Mafunzo yalifanyika katika ukumbi wa TAWIRI Arusha tarehe 20 Juni, 2025.