Nyota wa zamani wa England David Beckham amesaini mkataba wa miaka 10 wa kuwa Balozi wa Utalii wa nchi ya Qatar. Mkataba huo utamlipa takribani paundi milioni 15 kwa mwaka. Pembeni ya kutangaza utalii na utamaduni wa Qatar nyota huyo atakuwa uso wa Kombe la Dunia 2022.