Jumapili 5 Julai 2026 itanza raundi ya pili mkondo wa Pili wa Fahari Super Cup 2026 katika uwanja wa Red Cross Ngomeni Kisesa Magu Mwanza.
Mkurugenzi wa Mweta Sports Club ambao ndio waratibu wa Michuano hiyo anaelezea kwa undani kuhusu mechi ya kesho na ratiba inayofuata.
M/Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Bara, @HecheJohn, pamoja na N/ Katibu Mkuu wa Bar @amanigolugwa, na wengine, wamewasili katika mortuary ya Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, kushiriki uchunguzi wa mwili wa marehemu Suez Dani Maradufu ili kubaini chanzo cha kifuo chake.
Akizungumzia maandalizi na malengo ya kliniki hiyo, Kocha Kessy Mziray, ambaye ni Mwalimu wa Michezo wa Karume Day & Boarding School, ameeleza kuwa mpango huo unalenga kuwapa watoto nafasi ya kuonesha vipaji vyao chini ya mazingira bora na ya kitaalamu.
Shule ya Karume Day & Boarding School, iliyopo Nshambya, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, imekamilisha maandalizi ya kuendesha kliniki maalum ya kusaka na kuendeleza vipaji vya michezo kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 6 hadi 13, wavulana na wasichana.
Kwa mujibu wa waandaaji, watoto watakaoonyesha uwezo wa hali ya juu watapata nafasi ya kuendelea na hatua zinazoweza kuwafungulia milango ya kujiunga na akademi kubwa ya soka nchini Uhispania, hatua inayoweza kuwa mwanzo wa safari yao kuelekea soka la kimataifa.
Uongozi wa shule umetoa wito kwa wazazi na walezi kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kushiriki katika zoezi hilo, ambalo linalenga kubaini, kukuza na kufungua fursa za kimichezo kwa vijana wenye vipaji.
Kliniki hiyo inatarajiwa kufanyika mara baada ya kumalizika kwa likizo ya shule, ikianzia takribani Julai 8 hadi 12, 2026, katika viwanja vya shule hiyo.
Feyfay Investment inakutakia mwanzo mwema wa mwezi. Mwezi huu uwe wa fursa mpya, mafanikio makubwa na hatua mpya za maendeleo.
Usikate tamaa kwa changamoto za jana. Anza upya ukiwa na imani, bidii na uthubutu, kwani kila siku mpya ni nafasi ya kujenga kesho iliyo bora.
Jiandae kwa matukio muhimu, fursa za kipekee na programu mbalimbali kutoka FEYFAY INVESTMENT. Tunaendelea kukuandalia shughuli zenye lengo la kuibua vipaji, kuwawezesha watu na kuleta burudani yenye tija.
Tunaamini katika vipaji, tunawezesha ndoto na tunajenga mafanikio.
#MCHEZAJIBORA | THAPELO MASEKO.
Thapelo Maseko ameibuka Mchezaji Bora wa Mechi baada ya kuiongoza Afrika Kusini kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini, akifunga bao pekee la ushindi.
Viongozi @ChademaTZ2 wako ziara ya kitaifa ya Operation FreeLissu na Katiba Mpya kusini mwa Tanzania. Wanasafiri maelfu ya kilomita kupitia barabara za vumbi na lami, wakianzia Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Tabora, Kigoma na kurejea Dar es Salaam.
🚨 Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Kanda ya Pwani, Boniface Jacob @ExMayorUbungo leo amefika Kituo cha Polisi Oysterbay baada ya kuitwa jana akiwa safarini kuelekea Morogoro kwa shughuli za mikutano ya hadhara.
Kupitia visa hivi utajifunza, utapata nguvu mpya ya kupambana na hali unayopitia, na kugundua kuwa nyuma ya kila maumivu kuna somo, na nyuma ya kila changamoto kuna njia ya ushindi.
🎙️ SIMULIZI HOUR | MAISHA NI SAFARI, KILA MTU ANA KISA CHAKE.
Je, umewahi kupitia maumivu yaliyokufanya ukate tamaa? Umewahi kusalitiwa, kudhulumiwa, kupoteza kila kitu au kupambana kimya kimya huku ukitafuta mwanga wa maisha!