Walioachwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, Hussein Bashe (Kilimo), Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani), Jenista (Afya), Dk Seleman Jafo (Viwanda na Biashara), Dk Pindi Chana (Maliasili na Utalii) na Dk Damas Ndumbaro wa Katiba na Sheria.
#FlowUpdates
Mahakama nchini Bangladesh imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani, Sheikh Hasina, adhabu ya kifo Nov 17,2025 kufuatia kesi ambayo ilimkuta na hatia ya kuagiza ukandamizaji mkali dhidi ya uasiulioongozwa na wanafunzi mwaka uliopita.
Chanzo @Reuters
✍️Flowin Vitus
#FlowUpdates#News
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo huku Hamis Mwinjuma (FA) kuwa Naibu Waziri na Paul Makonda akiwa kama Naibu wa pili wa Wizara hiyo.
#FlowUpdates#news#ikulu
Rais Samia Suluhu amemteua George Boniface Simbachawane kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi huku Dennis Lazaro Londo akiwa Naibu Waziri.
#FlowUpdates#news#ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Dorothy Gwajima kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu.
Dkt. Samia Amemteua pia Maryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo.
#FlowUpdates#news#ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Hamis Mussa Omary kuwa Waziri wa Fedha.
Balozi Omar ameteuliwa akichukua nafasi ya Dr. Mwigulu Nchemba ambaye aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
#FlowUpdates#ikulu
Kufuatia teuzi zilizofanywa hii leo Ikulu Chamwino, Dodoma Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
#FlowUpdates#news
Katika uteuzi uliofanywa leo Ikulu Chamwino, Dodoma Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Wanu Hafidh Ameir kuwa Naibu Waziri wa Eimu, Sayansi na Teknolojia.
#FlowUpdates,#News,#Ikulu
Kufuatia Teuzi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mohamed Mchengerwa ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya.
Uteuzi huo umetangazwa leo Novemba 17, 2025 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
#FlowUpdates#news#ikulu
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amemteua William Lukuvi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), huku Naibu Waziri akiwa Ummy Hamis Nderiananga.
#FlowUpdates,#Ikulu
Rais Donald Trump amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni Linalojihusisha na Habari la BBC kufuatia jinsi uhariri wa hotuba yake na kipindi cha Panorama.
Trump alisema: “Tutawashtaki kwa chochote kati ya dola bilioni 1 hadi 5, pengine wiki ijayo.”
@FlowUpdates,@News
Rais Trump amesema atakuwa akiomba A.G. Pam Bondi, na Idara ya Haki, pamoja na mashujaa wakubwa katika FBI, kuchunguza uhusiano na ushiriki wa Jeffrey Epstein na Bill Clinton, Larry Summers, Reid Hoffman, J.P. Morgan, Chase, na watu na taasisi nyingine nyingi.
#FlowUpdates,#News
kifuatiliaji cha taarifa za safari za ndege nchini marekani kimethibitisha kuwa leo Nov 11,2025 safari 1,100 za ndege zimefutwa kutokana na Hali ya hewa na udhibiti wa idadi unaofanywa na mamlaka nchini humo.
Chanzo @ABCNewsLive
✍️Flowin Vitus
#FlowUpdates#News
Mbunge Mteule wa Ilala, Musa Azzan Zungu amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania baada ya kupata kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa.
Zungu amelitumikia bunge kwa takribani miaka 20 pia amewahi kuhudumu kama Mwenyekiti wa Bunge na Naibu Spika.
#FlowUpdates#news