Vijana mjifunze kutoka historia ya Maumau na freedom fighters wengine
Mnatakiwa kuwa kama Mmasai
Msilale comfortably majumbani na simu zenu mzitumie kwa akili
Hakuna kukaa kinyonge
Nadhani tumeelewana -maana hawa wamepanic kwa sasa 🙄
#SaveTanzania
Breaking News:
Inaelezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara John Heche amekamatwa muda mfupi uliopita leo, Jumatano Oktoba 22.2025 akiwa anaingia kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam
Akizungumza na Wanahabari kuhusiana na hilo, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amedai kuwa Heche amekamatwa ghafla alipokuwa anaingia Mahakamani hapo lakini hadi sasa uongozi wa chama hicho haujui sababu ya kukamatwa kwake,
Amesema amepokea simu kutoka kwa mmoja wa wasaidizi wa Makamu Mwenyekiti huyo na kumueleza kuwa Heche amepelekwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) Dar es Salaam, na kwamba kwa sasa Mawakili wanaelekea kituoni hapo kufuatilia sababu za kukamatwa kwake,
Jambo TV itakuletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Furaha ya kufahamu kuwa TAL hajauza game amidst a massive storm is insane.. Mungu wetu aliye mwaminifu akuhifadhi na akuangazie nuru za uso wa macho yake, my brother.
Tunajenga taifa la namna gani?
24hrs baada ya kukamatwa
1. Hajapewa access ya kukutana na ndugu au mawakili wake
2. Hatujui kosa lake
3. Hajapewa dhamana
4. Hatujui usalama,food, water na mengine haijulikani.
5. Hajulikani yuko wapi?
Kinyume na CPA, 🍌Rep.
@HecheJohn Stay safe!
Afande IGP, Sasa ni saa 12:30 mchana wakati ninaandika ujumbe huu. Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA alichukuliwa na askari polisi mjini Dar es Salaam. Tulipofika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, tuliambiwa amepelekwa Tarime, kwa sababu ya shauri lake. Nasi tulifurahi kwa sababu alikamatwa hadharani. Hata hivyo, hadi sasa viongozi wetu pamoja na wale walioko Mara hawajui mahali alipo. Hili si tu ni chanzo cha taharuki bali ni utovu mkubwa wa nidhamu dhidi ya haki za binadamu.
Mnataka kufanikisha nini? Nina wasiwasi mkubwa kwamba siku moja jamii inaweza kupuuza hofu, uoga na Nchi yetu itapotea kwenye mwelekeo mbaya. Kama ilivyoandikwa “Mshahara wa dhambi ni mauti”
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 139
Mhe. Lissu: Kati ya Mwaka 2021 na 2022 ulihudhuria mafunzo ya Assistant Inspector of Police kule Moshi, sasa kwenye maelezo yako Polisi mambo hayo yapo?
Samuel Kaaya : Sikuyasema.
Mhe. Lissu: Ulisema umesomea medani za kivita na masomo mengine mengi hayo nayo umesema kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Sikusema.
Kwa kifupi huyu shahidi amesema mambo mengi sana hapa Mahakamani ambayo siku anaandika maelezo yake Polisi kuhusu kesi hii hakuyaandika ila hapa Mahakamani ameyasema.
Ndio yale maeneo 75 ambayo Mhe. Lissu ameyasema hapo awali na anaendelea kumuuliza.
Kila kitu anachomuuliza shahidi kwamba ulisema hivi hapa Mahakamani je kwenye maelezo yako yapo? JIBU LA SHAHIDI NI HAPANA, HAYAPO NA SIKUANDIKA.
Yataulizwa maswali mengine ya utofauti wa statement mfano alisema hapa Mahakamani hivi na kwenye maelezo alisema tofauti tutafikia pia hatua hiyo.
Lengo la zoezi hili ni kuonesha shahidi ni muongo na hapaswi kuaminika.
Mhe. Lissu: Je ulisema sana hapa Mahakamani kuhusu mafunzo uliyopata South Africa, Je kwenye maelezo yako yapo?
Samuel Kaaya: Sikuandika kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : Ulisoma miezi sita chuoni hapo?
Samuel Kaaya : Sikuandika na hilo pia.
Mhe. Lissu: Anauliza kuhusu chuo cha IFM na Masomo aliyosoma ya kuhusu Uhasibu na Data Management anayosema alisomea na kuzawadiwa shahada ya Sayansi ya Tehama kwenye vyuo mbalimbali je yako wapi kwenye maelezo yake?
Samuel Kaaya : Sikusema.
Mhe. Lissu: Mwaka 2024 ulipata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Sayansi ya Jinai. Kule India, Je yako wapi hayo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : sikuandika kwenye maelezo yangu, hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema mambo mengi ikiwemo utaratibu wa kuchunguza vielelezo ikiwemo ile kanuni yenu ya first inn first out kama umeuelezea kwenye maelezo yako ya pale Polisi?
Samuel Kaaya : Sikuelezea kabisa.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu kuwepo na Police Notebook muda wote ili kila unaloliona unarekodi kwenye Polisi Notebook, je hayo yapo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Hayapo
Mhe. Lissu: Hivi nyie Mapolisi nani huwa anawafundisha kuandika maelezo yenu?
Samuel Kaaya : Tunafundishana wenyewe.
Mhe. Lissu: Neno Confimatory test ulifanya, sasa nionyeshe hapo kwenye maelezo yako hiyo confirmatory test ulipoandika.
Samuel Kaaya : Kiukweli Sijaandika hilo neno, halipo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa unafanya Chron analysis ili kugundua kama kuna Deep Fake yaani teknolojia ya AI imetumika katika video husika je hayo yapo kwenye maelezo yako uliyoandika Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo Sikuandika.
Mhe. Lissu: ulisema habari za kuangalia video kama iko compressed or decompressed nao upo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Haupo.
Mhe. Lissu: Ulisema kuhusu censor pattern analysis na non Uniformity je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema habari za kufanya noise analysis kwenye hiyo video sasa tueleze hayo mambo mengi na utaratibu wa kufanya noise analysis na unaweza kuona vichengachenga kwenye video kama yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo
Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi nikisema huu ushahidi wa maeneo niliyokupitisha ulikuwa ni wa muhimu kwenye kesi hii?
Samuel Kaaya : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na ni kweli ni muhimu kwasababu unaonesha maabara yenu inavyofanya kazi kitaalamu?
Samuel Kaaya : Ni kweli
Mhe. Lissu: kuhusu notebook ni muhimu askari awe nayo muda wote wa uchunguzi hilo nalo ni muhimu?
Samuel Kaaya : Ni muhimu.
Part 140 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.