Naogopa sana jamii ikichoka kusema….
“ TUNAMWACHIA MUNGU”
Kauli hii ichukuliwe kama kengele ya tahadhari. Kwa sababu jamii ikichoka kabisa, madhara yake si kwa wananchi pekee, bali kwa taifa zima. Uongozi makini husikia hata sauti iliyosemwa kwa upole na hasira kabla haijageuka ukimya wa maumivu na fujo.
ningekuwa rais muislamu kutoka z'bar na nagundua kuna harakati kuifanya serikali yangu ionekane ina vita na kanisa katoliki, ningefanya kila linalowezekana kampeni hiyo kukoma. uwezo huo uko ndani yangu. kumbuka, mimi ni rais wa tanzania, nina nguvu zote:
Wakili Dkt. Rugemeleza Nshalla—> HONGERA. Miaka 30 tangu kuapishwa kuwa Wakili (15.12.1995–2025)! (2019–2021). U mwanzilishi mwenza wa LEAT, msomi wa Sheria wa Harvard, mtetezi shupavu wa haki za binadamu, utawala wa sheria na kuhifadhi mazingira, na kwa sasa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA. Uzalendo mkubwa kulitumikia Taifa. Mungu akulinde na kukuongoza.
30 years at the Bar (15.12.1995–2025)! Congratulations to Adv. Dr. Rugemeleza Nshalla—former TLS President (2019–2021), co-founder of LEAT, Harvard-trained advocate for human rights, rule of law & environmental justice, and current Director of Legal Affairs, CHADEMA. An outstanding legacy of service 🇹🇿👏
#30YearsAtTheBar #RuleOfLaw #HumanRights #EnvironmentalJustice #TLS #CHADEMA
Ni rahisi sana kuwaweka CHAWA straight bila fujo yoyote. Hii ni kwa Gen Z na watu wengine wote.
Hatupigi kelele, hatutukani , tunapiga BAN.
1️⃣ Wakisema kuna show → USIENDE kabisa. FULL BAN
2️⃣ Kampuni inayofadhili hiyo show~BAN bidhaa zao zote
3️⃣ Ukumbi uliotumika , USIWEKE MIGUU~BAN
4️⃣ Makampuni yanayowasponsor kupitia radio, TV, mabango~BAN huduma zao
5️⃣ Pages zao kwenye social media~UNFOLLOW WOTE NOW. BAN
6️⃣ Streams zao (YouTube, Spotify, Boomplay, Apple Music) → DON’T PLAY. BAN
7️⃣ Ringback / caller tunes → ONDOA. BAN
8️⃣ Events wanazohudhuria kama guests → IGNORE kabisa. BAN
9️⃣ Brands zinazowachukua kama ambassadors → BAN hiyo brand
🔟 Media interviews zao → USITAZAME, USISKILIZE. BAN
1️⃣1️⃣ Merchandise zao → USINUNUE. BAN
1️⃣2️⃣ Hashtags zao → USITUMIE, USITRENDSHE. BAN
1️⃣3️⃣ Fan pages zinazowapromote → MUTE / BLOCK. BAN
1️⃣4️⃣ Clubs & lounges zinazowaplay → USIENDE. BAN
1️⃣5️⃣ Award shows wanazoteuliwa → USIPIGE KURA. BAN
🧠 Kanuni ya Gen Z na wananchi wote, Hakuna fujo. Hakuna matusi.
Attention = currency.
Ukikata support → nguvu inaisha.
👉 No support. Full BAN.
#GenZ #WatuWote #BAN #NoSupportNoShow
Wewe mtu kachaguliwa na Somalia na Burundi na Mashekhe ubwbawa, unadhani atakuwa na akili ya kuwaza kwamba kafanya kosa?
Sambazeni Ujumbe Watanzania wote tuungane tarehe 9 Disemba. Hata ndani ya CCM hatumtaki huyu Jezabeli. Ana uwezo mdogo sana. #SamiaMustGo
Kila siku tunasikia kauli ileile ya kujifariji/kipumbavu kabisa, Etiii Mataifa mengine yanatuonea wivu wa maendeleo.” Wivu wa nini hasa? Wivu wa fedheha?
Maendeleo gani tunayojivunia wakati foleni ya kilomita 13 inatuadhibu kwa masaa matatu kana kwamba tunaendesha mikokoteni?
Maendeleo gani wakati taifa zima vijana wamegeuka kuwa madereva boda boda, si kama ubunifu, bali kwa kukosa ajira za maana? Maendeleo gani wakati kina mama wamejazana mitaani kuwa machinga, wakikimbizana na mgambo badala ya kuwa na mifumo rasmi ya biashara?
Maendeleo gani wakati vijana wa kiume wanaingia kwenye kutinda nyusi, kujiremba kupita kiasi, na wengine kusukumwa kwenye ngono za kulipwa kutokana na ukosefu wa fursa halali? Tunachojenga ni picha, si nchi. Tunapaka rangi juu ya ukuta uliochanika.
Hospitali hazina dawa. Shule hazina vifaa. Wakulima hawana masoko. Vijana hawana matumaini. Huku tukipewa maneno matupu ya kuaminishwa kwamba “Tunaonewa wivu kwa sababu ya maendeleo” Ikiwa haya ndiyo maendeleo tunayosema yanawafanya wengine watuonee wivu, basi huo si wivu ni huruma.
Hatuwezi kuendelea kuishi katika ndoto ambazo hazipo. Hatuwezi kuendelea kushangilia takwimu zisizogusa maisha ya mwananchi. Maendeleo hayajengwi kwa maneno, bali kwa kubadilisha hali halisi ya wananchi. Mpaka siku tutakapokubali ukweli ndipo tutaacha kujivunia hewa.
Hotuba ya Madam Samia imekuwa nzuri kwa sababu imebeba ishara za msaada wa Mwenyezi Mungu juu ya Nchi. Kama Mungu alivyofanya wakati akiwatoa Waisraeli Misri alipouacha moyo wa Farao uwe mgumu ili ajitukuze mbele ya watu wake, vivyo hivyo utukufu wa Mungu umeonekana Tanzania, tunahitaji mambo magumu ili kuthibitisha alama za nyakati na tujue tulikuwa na yeye ktk safari ya haki. Ninaiona kesho iliyo bora, yenye heshima na utukufu wa Mungu, maana dalili zote tayari zimekamilika. Basi tusifikiri mabaya juu ya mtu yeyote bali tuendelee kutafakari haki na wala tusichoke kutenda wema maana tutavuna pasipo kutarajia. Mtamshangaa sana Mwenyezi Mungu. Mimi, ingawa ni mdhaifu na sina uadilifu mbele zake, lakini ninautambua uwezo wake usio na kifani. Leo imekuwa siku ya ishara kubwa. Jipeni Moyo Mkuu. Tutavuka salama. Msizimie Moyo.
Utalii unachangia karibu 30% ya fedha za kigeni nchini, na kama mtu ninayetoka Arusha na kufahamu kwa undani tourism corridors, hali ilivyo sasa ni ya kutisha. Tour operators wamebaki na kazi moja, kupokea cancellations kila saa. Hawa tunaowaita ‘wafadhili’ si watu wa kutumiwa kama mifano ya majigambo ya kisiasa. Hao ndio wateja wetu wakuu, watoa huduma wa kimkakati, na sehemu ya mifumo inayolisha uchumi mzima na sekta ya utalii. Ni kosa la kimkakati, na kiukweli ni aibu ya kiwango cha taifa, kwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoa kauli ya kubeza kama hii. Katika mazingira haya, hatuhitaji kauli za kutengeneza headlines za kisiasa, tunahitaji uongozi unaofahamu geopolitics ya biashara, umuhimu wa foreign confidence, na athari za maneno ya juu juu kwenye sekta inayotegemewa na maelfu ya Watanzania. Huu si wakati wa kukwepa ukweli; ni wakati wa kufanyia kazi ukweli.
VIDEO:
Mazishi ya aliyekuwa Wakili mtetezi wa watuhumiwa wa vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu, Beatus Linda, yamefanyika jana katika makazi ya familia yao eneo la Nyamhongolo, Wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza.
Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyoongozwa na Paroko wa Parokia ya Nyamhongolo, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Padre George Nzungu. Katika mahubiri yake, Padre Nzungu alimpongeza marehemu kwa moyo wake wa kutetea haki za watu, hususan wananchi waliokamatwa kufuatia vurugu za maandamano ya Oktoba 29.
Alisema marehemu Linda alikuwa mfano wa wanasheria waliotumia taaluma yao kuweka mbele ustawi wa watu na kuwatumikia wenye uhitaji.
Akisoma historia ya marehemu, Makamu Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Mwanza, Erick Mutta, alisema kuwa Beatus Linda ameacha watoto watatu Lincoln, Kendrick na Eliah pamoja na mchumba wake, Ruth Mwakitalu, waliokuwa wakitarajia kufunga ndoa mapema mwaka 2026.
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma naye walieleza kushtushwa kwao na msiba huo, wakisema wamepoteza mtu muhimu kutokana na tabia yake ya ukarimu, upendo na ushirikiano katika masuala ya kijamii na ya kazi. Walisema marehemu alikuwa msaada mkubwa kwa wenzake na alijitahidi kila mara kuhakikisha kila mtu anasonga mbele.
Upande wa familia ya mchumba wake ulieleza kuwa msiba huo umewapiga butwaa kwa kuwa ulikuja ghafla wakati wakiwa na mipango mingi ya pamoja, ikiwemo kufunga ndoa ifikapo Juni 2026.
Wakili Beatus Linda alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 23, 2025, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Mwanza.