HERI YA SIKU YA MTOTO WA KIKE KIMATAIFA
Tunahitaji kuwawezesha wasichana kwa elimu inayohamishika na ujuzi wa muda mrefu kama vile Fikra, Ubunifu na Uelewa wa masuala ya kidijitali, na kuwa na watu ambao ni mfano wa kuigwa itakuwa muhimu sana hususani katika ulimwengu wa sayansi.
Tunaamini kuwa, kitabu ndio mwongozo na
mwanga kwa jamii hususani mabinti ktk kujikwamua kiuchumi. Ni imani yetu kuwa elimu iliyopo katika kitabu itasaidia kupunguza umaskini, kuimarisha usawa wa kijinsia na kumaliza kabisa utegemezi wa wanawake
na katika jamii
#GirlsInAction
Ni Siku Njema na Yenye Baraka katika Uso wa @miriammauki
.
Leo Tarehe 20 August Tunasherehekea miaka kadhaa ya kumbukumbuka ya kuzaliwa kwake Mama yetu, Mlezi, Mpambanaji Na Mtetezi wa Mabinti #MiriamMauki
Ikawe Heri, Baraka na Fanaka katika Safari ya maisha yake.#GirlsInActionTz
Hili ni moja ya Tamasha kubwa lililo wahi kufanywa nasi @girlsinactiontz miaka mitatu iliyo pita kwa ushirikiano mkubwa wa World Bank Tanzania 🇹🇿.
Nia na malengo yetu ni kuwajengea watoto wakike uwezo wa kujiamini, Kiutendaji, kifikra, Kiuchumi na kuchukua hatua.
Tunamaono ya kuwa na jamii ya Tz inayoheshimu haki za binadamu za wanawake. Na Dhima yake ni kujenga mtandao imara wa vyombo mbali mbali vya kitaifa na kimataifa pamoja na mpango wa dharura wa kuitikia ukatili wa kijinsia katika ngazi zote huku ikihusisha sheria na maendeleo.
.
Ni hatua madhubuti ya kujenga uwezo wa Mabinti waweze kujitegemea ili waweze kufanya maamuzi juu ya maisha yao na
kutekeleza maamuzi hayo kwa kutumia rasilimali zilizopo bila kuingiliwa au kubughudhiwa na mtu, taasisi au chombo chochote kwa sababu tu, wao ni wanawake.