@Sirajitz1 Huyo jamaa mara nyingi kanivamia sana hapo Karume.... kinachonisaidia siyo mpenzi wa majuisi ya barabarani... ila anakera kwa kiasi fulani mpaka ugundue kuwa ni mbinu yake ya biashara anakuwa amekupotezea muda mwingi, sababu lazima tu utamsikiliza...
@kizijr @Eric__Bernard Acha kinyongo huyu Binti mpe maua yake, hiyo ni hotuba halafu hasomi popote siyo kazi nyepesi hasa kwa mtoto mdogo huyo kusimama mbele ya Mh. Rais. Tujenge utamaduni wa kuwatia moyo mabint ambao wala hawapo kwenye ushindani na sisi. Kwani ukimpongeza hapo unapungukiwa nini jomba.
@Deo18Tarimo Tanzania Ina watu wema sana ila basi tu Kuna wachache wanachafua sifa za wakazi wa Tanzania.... @ayotv_ endeleeni kuibua watoto wengine wenye changamoto kama hizo, wengi huko vijijini wanazikwa na ndoto zao...
Shukrani ziende kwa mkuu wa wilaya Mh. Magoti hiyo ndiyo ibada nzuri
@RashdaZunde@rollymsouth@Mwabuk2Boniface Ujue Mimi nashindwa sana kuwaelewa baadhi ya Watanzania, hivi kwamba hii kasumba ya kumlaumu BAKM inatokana na nini... Ni msomi anayeongea kwa lugha inayoeleweka, kama vile anafundisha.. sasa kwenye ule mkutano na Mh Rais mlitaka amrukie Mh Rais mwilini ndiyo mridhike, nyie vipi?
@HKigwangalla Binafsi nimefurahishwa sana na hoja yako Bungeni... Wakati mwingine nafurahi pale ninapoona baadhi ya Wabunge mnakuwa Bungeni kwaajili ya kusemea shida ama walizonazo watu au wanazozitarajia kuzipata hapo mbeleni... Kila kitu kinatekelezwa Bungeni hivyo tunawategemea nyie.
@fatma_karume Hivi Mh. Mpina lini ana ugomvi na Mh. Rais mbona sijaelewa hapa dada Fatma ... Naona umekazana sana na sentensi hizo.. au ndiyo unachomchea kwa Mh. Rais makusudi?
Yani masuala ya Bungeni na akina Mwigulu ndiyo uanze kumwingiza Mh. Rais kweli.. tafadhali dada acha kabisa hizo.
@fumbokhanJr Hivi huyu @fumbokhanJr Huwa anaongeaga ukweli ni comedy za akina Stive mweusi, maana tusijeanza kutumia nguvu kujibu hapa kumbe anafanya masihala.