#TajiriLaKihaya
Ujue Serikali Nyingi Huwa inatumia kanuni ya ‘TENGA UTAWALE’
DIVIDE AND RULE…
Hii hurahisisha saana Utawala wao… na kutuweka busy na mambo yasio na muhimu wao wakiendelea kula mema ya nchi…
Tumejitahidi kwa kiasi chake kuDeal na Mambo ya Wasanii na Miziki yao…
Tumejitahidi kwa kiasi chake Kudeal na Mambo ya Simba na YANGA… mamipira..
Vile vile Naomba Saana Tujitahidi Kudeal na UDINI…
UDINI ndio silaha kubwa zaidi kuzidi zote… MAANA inashika Imani za watu- na waafrika wengi Huwaambii kitu kuhusu Dini…
Kama ambavyo kwenye Simba na Yanga Tumedeal na Viongozi wao, kwenye miziki tumedeal na Wasanii na kuacha kuwafuatilia ila MASHABIKI tumebaki kuwa wamoja … let the same Apply to Maswala ya DINI…
Masanja Mkandamizaji,Mwamposa,KKKT na wengineo Wakiharibu Tunadeal nao na Sio Wakristo wote wala wafuasi wao…
BAKWATA wakionekana wameramba Asali - tudeal nao wao… viongozi hao na wala sio waislamu wote au Masheikh wote…
Tutaacha mambo ya muhimu na kudeal na vitu ambavyo havifai mwisho wa siku Tunapoteza FOCUS.
Kama MUISLAMU nawaambia BAKWATA sio Taasisi ndogo kama tunavyoichukulia- Dar es salaam,Pwani,Tanga,Dodoma,Singida,
Tabora,Zanzibar NK- misikiti ya Bakwata ni asilimia 98% ya misikiti yote mnayoiona…Mikoa yote mikubwa na wilaya zote Tanzania nzima misikiti mikubwa ya IJUMAA ni ya Taasisi za BAKWATA.
Kiufupi asilimia 90% ya waislamu NCHI nzima viongozi wao ni BAKWATA na wanawafuata kweli kweli… mfano mzuri tu angalia - sikukuu za iddi… wengi huwafuata BAKWATA na wanaoswali siku tofauti ni wachache mno- hata kama zote zitaangukia weekend.
Ninataka kusema nini… tujichunge saana Tusipoteze FOCUS yetu mwisho wa siku tukapoteza nguvu na muda wetu kwenye maswala ya DINI…
Kama ambavyo BAKWATA walituamrisha TUFUNGE Jumatatu siku ambayo Raisi alikua anaapishwa na TUKAKAUSHA hakuna Aliefunga- tukaendelea na mambo yetu…
Tuendelee vivyo hivyo… maana Hatukuwatukana wala kuwavunjia heshima…
Hakuna ambae atapigana na Dini akashinda… hata msemaje hakuna muislamu ambae atahama awe mkatoliki na vivyo hivyo hakuna mkatoliki atahama awe muislamu…
Tuendelee kupigania tunachokiamini bila Kuvunjiana Heshima kwenye Dini… ADUI wetu ni mmoja tu… na atafurahia saana tukiingia kwenye huu mchezo wa UDINI.
Viongozi wakiongea ‘Pumba’ zao tuwakaushie infact hata Airtime hio ya kuwajadili tusiwape… lets FOCUS na mambo ya muhimu- Positive vibes only!
Hakuna kipindi inapaswa tuwe wamoja kama hiki…
Hakuna MUISLAMU KAMILI atafurahia unapowatukana MASHEIKH ZAO - hata mm sifurahii mnapowatusi masheikh hawana Elimu… mara sijui wanakula kitimoto… matusi ambayo hayana Tija kutafuta likes na engagement za kipuuzi.
Tofauti na mitazamo yetu kwenye siasa kuwa Tofauti…hawa ni Masheikh zetu kwenye Imani… ni waalimu wetu wa madrasa ni viongozi wetu wa Kiroho…
Lets maintain our FOCUS…
tukianza kujigawa kwenye UDINI… kuna wengi kimbilio lao litakua DINI KWANZA…and it will be worse!
Now Tunataka KATIBA MPYA, Tume ya UCHAGUZI IVUNJWE , waliouwa ndugu zetu WAWAJIBISHWE, Haki ipatikane kwa wote walioathirika, vijana wetu waliopotezwa wapatikane wakiwa Hai au miili yao, wafungwa wa Kisiasa wote waachiwe huru bila masharti, Kesi zote za CHADEMA mahakamani zitupiliwe mbali na waachwe waendelee na kazi zao!
Ikiwezekana UCHAGUZI MKUU URUDIWE…. Hata kama ni gharama tupo tayari kukaa miaka mitano bila maendeleo yoyote- ila viongozi tuwachague sisi kihalali💯
Lets maintain our FOCUS…
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Retweet yako.