VIDEO:
Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael George Mabuga Msonganzila, amewataka waumini na viongozi wa dini nchini kutokubeba jazba wala kujiingiza katika mijadala ya matusi, lawama na kejeli inayoibuka mitandaoni na kwenye mikutano ya kijamii, akisema kuwa njia ya Kristo ni ya upole, uvumilivu, huruma na kutanguliza haki.
Akizungumza kufuatia mfululizo wa matamko kutoka taasisi kadhaa za Kikristo na Kiislamu kuhusu matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu, huku baadhi ya kauli zikiishambulia Kanisa Katoliki kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uchochezi dhidi ya amani ya nchi, Askofu Msonganzila amesema kuwa migogoro na kejeli haviwezi kuizima nguvu ya ukweli.
“hamna sababu ya kuijibu, ni kuinyamazia tu wakati mwingine watu wakisema sisi tumeenda shule sio zamani, kwani kwenda shule ni shida? Shida ni kusoma, shida ni kuelimika, sasa kuzozanazozana katika misingi hiyo haina haja- ni kunyamaza kama Kristo aliyedhihakiwa: Wewe si ni mwana wa Mungu Jiokoe basi nafsi yako, Nyamaza kimya endelea kusali”, amesema.
Askofu Msonganzila amesisitiza kuwa nguvu ya maneno ya kupotosha haiwezi kuzidi uzito wa maadili, utu, na dhamira njema ya Kanisa, akionya kuwa matusi na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa haviwezi kubadilisha msingi wa imani wala wajibu wa viongozi wa dini kusimama katika kweli.
“Mahangaiko yakitokea ndugu zangu tusiogope kwa sababu ndio Kristo amepitia njia hiyo, Kanisa Katoliki linaweza likateseka kwa njia za namna hiyohiyo na matishio mbalimbali: umemwaga ugali tutamwaga mchuzi, tutawakatakata- tusiogope Mungu yupo”, ameeleza.
Ameongeza kuwa ufalme wa Mungu haujengwi kwa hasira, vitisho au ubabe, bali kwa misingi ya huruma, mapendo, upatanisho, haki, unyenyekevu na uvumilivu.
“Ufalme wa Mungu ni ufalme wa huruma na mapendo, haki, upole, upatanisho, tukiteseka kwa njia hiyo na tuteseke lakini haki na amani, upole na unyenyekevu na upatanisho ndio ziwe sare zetu, tumsifu Yesu Kristo”, ameeleza.
Kauli ya Askofu Msonganzila imekuja wakati ambapo mjadala kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kueleza ukweli wa kijamii na kisiasa umeendelea kushika kasi, huku baadhi ya taasisi za kiimani zikitoa matamko yanayopingana kuhusu misimamo ya Kanisa Katoliki na makundi mengine ya kijamii kuhusu mwenendo wa uchaguzi na matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
VIDEO:
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kwa Jimbo la Kigoma Mjini Wagombea Ubunge wa mwaka huu wa CCM Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Babalevo na Zitto Zubeir Kabwe wa Chama cha ACT Wazalendo wote ni wanae na wananchi ndio watakaoamua nani awaongoze.
Dkt. Samia ameyasema hayo Septemba 14, 2025 wakati wa Mkutano wake wa kampeni Kigoma Mjini, akilazimika kueleza hayo kutokana na ombi la Baba Levo aliyemuomba Dkt. Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kumtaja mgombea anayemuunga mkono kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
"Sina utani, nitampiga mtu saa tano asubuhi kwasababu ninayeshindana nayi mtu dhaifu sana, ni maarufu (gangwea) kwenye mitandao lakini ukimleta huku chini ni biskuti. Ni kama ameshahamia CCM maana leo alikuwa anasambaza vipeperushi vya Oktoba tunatiki akiwa amemuweka Mama na yeye pale chini, nakuomba Mama ni muda wa kumuambia ukweli unamsapoti nani hapa Kigoma Mjini." Amesema Baba Levo.
Katika majibu yake pamoja na mengine, Dkt. Samia amemjibu akisema ""Nataka kuwaambia wote ni watoto wangu kwasababu hata yule mwingine katoa vibao vya kijani na njano vinasema mpe Mama Samia, Ubunge nipe mimi sasa si unajua kwenye nyumba watoto wakiwa wawili watatu wanavutana sio ndio? Lakini wote ni wanangu."
Let us ask from the Holy Spirit the gift of #Peace. Peace begins in our hearts, for only a peaceful heart can spread peace in the family, society, and international relations. May the Spirit of the Risen Christ open paths of reconciliation wherever there is war. May He enlighten those who govern and give them the courage to take steps toward de-escalation and dialogue.