You gotta love Tundu Lissu, man.
His mitigation factors is that of a no nonsense lad.
“Sheria inapotaja adhabu ya faini au kifungo, ni lazima kwanza itoe adhabu ya faini. Huu ni msimamo wa kisheria.”
“Mkinipa maximum sentence itakuwa ni ushaidi kuwa mmeelekezwa.”
Oii🙌🏼🫡
“Waheshimiwa Majaji nashukuru kwa fursa ya kuzungumza. Naomba mnisikilize kwa makini kama ambavyo mmenisikiliza kwa makini mwaka mzima. Naomba pia m’rekodi proceedings kama mlivyo’rekodi vizuri mwaka mzima na nusu. Leo Waheshimiwa majaji ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kosa la uhaini. Ndiyo kosa kubwa Kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano. Ndiyo kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa la uhaini. Kwa siku 577 nimeitwa mhaini. Kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) ambapo adhabu yake inaeeza kuwa ni KIFO. Baada ya siku 577 baaada ya wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’inia juu ya kichwa changu. Leo Waheshimiwa Majaji mmeniita MCHOCHEZI. Kosa ambalo wala halijapangiwa adhabu. Unaona hapa, wakili mkuu wa serikali anahangaika kutafuta hii adhabu yake ni nini., anasema nipewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine, nihukumiwe kifungo cha miaka mitano gerezani. Hii maana yake ni nini Waheshimiwa Majaji? Waheshimiwa majaji mmesema wenyewe hakukuwa kosa. Kwa hiyo nimekaa gerezani siku 577 bila kosa lolote. Kuna kitu kimoja hamjakisema nitakisema kwa ajili ya kumbukumbu za Mahakama. Ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa kesi ya kisiasa. Kugeuza Mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, it’s an obvious political persecution. Kwa sababu ni political persecution inabidi vi’sababu vitangenezwe vya kumfunga huyu mgomvi wetu. Vi’sababu vya kumfunga huyu mpinzani wetu. Hili kosa la UCHOCHEZI ni kisa ambalo ninyi Waheshimiwa Majaji mmelitengeneza. Mimi nilishitakiwa kwa UHAINI na kusambaza taarifa za uongo. Mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, mmenipa. With all due respect mmefanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kwa maelekezo ya kisiasa tu. Ni kama mmeambiwa, huyu mtu hana kosa lakini tafuteni kosa lingine dogo, isije ikaonekana serikali imepata aibu. Mimi ninajua mtani’hukumu. Na mnaonekana tayari mnayo hukumu, l feel it in my heart.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, O6 November 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
“Sasa, Waheshimiwa Majaji, kuna maneno ambayo yamesemwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, ambapo amejigeuza kuwa shahidi badala ya kubaki kuwa Wakili wa Serikali. Amesema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba yalitokana na kauli zangu, kama nimemwelewa vizuri. Waheshimiwa Majaji, sina uhakika kama katika kesi hii mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Mkuu, Othman Chande. Hotuba hiyo haipo katika ushahidi wa kesi hii. Jaji Mkuu Othman Chande hajaja hapa kutoa ushahidi kuthibitisha kwamba kauli hizo zilitolewa na wanasiasa gani. Mnaombwa kutoa adhabu kwa kosa, kama kweli lipo, ambalo inadaiwa lilitokea miezi sita baada ya mimi kuwa tayari nimewekwa mahabusu. Mkikubaliana na mwaliko huo, Waheshimiwa Majaji, itakuwa ni uthibitisho kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo. Kesi nyingi kuhusu matukio mbalimbali ya uchochezi yamezungumziwa hapa. Lakini matukio hayo ni mangapi? Yametokea wapi? Na nani ameyafanya? Wakili Mkuu wa Serikali anataka muamini porojo za mitandaoni. Mkizikubali, Waheshimiwa Majaji, itakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maagizo.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
“Waheshimiwa Majaji, naomba nimalizie. Uamuzi wa kunitia hatiani kwa kosa ambalo sikushitakiwa nalo, na ambalo sikupata fursa ya kujitetea dhidi yake, kwa lengo la kubalansisha tu, una athari kubwa. Athari yake ni kwamba mmewapa kinga wale waliohusika na mauaji, kwa sababu watasema kwamba wale waliochochea wamekutwa na hatia. You are covering mass murderers. Serikali hii imeua watu wengi kuliko serikali zote zilizowahi kutawala nchi hii. Mara ya mwisho mauaji ya halaiki kutokea kwa kiwango hiki ilikuwa wakati wa Vita vya Majimaji. Mmewapa sababu ya kusema kwamba mkosaji aliyesababisha mauaji hayo amekutwa na hatia. Kama mnafikiria kwamba uamuzi huu utawasaidia, hautawasaidia. Watawajibishwa mahali pengine. Serikali ya Nyerere iliua watu 37. Wakati huo, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na alijiuzulu. Shahidi alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na alijiuzulu. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter, naye alijiuzulu. Leo hii, serikali imeua watu ambao idadi yao, kwa makadirio ya chini kabisa, ni 500, lakini hakuna aliyejiuzulu. Uamuzi wenu hautaficha ukweli huo. Nimewakumbusha, Waheshimiwa Majaji, kwamba katika Sentencing Guidelines, kipengele cha kwanza kinaelekeza kwamba adhabu ya faini itolewe isipokuwa pale ambapo kosa ni kubwa. Uchochezi, ambao sikushitakiwa nao, hauna adhabu maalumu. Ndiyo maana Wakili Mkuu wa Serikali anakwenda kwenye General Provisions. Waheshimiwa Majaji, namalizia kwa kusema: TOENI HUKUMU AMBAYO MNAYO, AMBAYO MMEAGIZWA KUITOA.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
Duh! Kama hawa ndo wanasiasa wetu, basi buana, tumeishiwa. Kweli, Lema ni wa kudogosha kazi za wanaharakati kama @MariaSTsehai, @mangekimambi na wengineo?!
Anyway, kwa kuwa kaonesha wazi kuwa yeye ni nani, ni kitu kizuri. We keep believing in you @HecheJohn na @TunduALissu.🤲
Unayeitwa Waziri mwenye dhamana ya kulinda raia na mali zao, unaweza kweli kuongea upumbavu kwa kiwango hiki na bado ukawa ofisini ? So sad.
Kwa kauli kama hii, hukupaswa kuwa ofisini hata kwa dakika moja. Dhamana ya kulinda maisha ya watu si mahali pa uzembe, dharau wala kauli zisizo na weledi.
Wakenya (Wenye NCHI) wametoa siku 7 Kizza Besigye (Uganda) na Tundu Lissu (Tanzania) waachiwe huru.
Kinyume na hapo BALOZI za "Tanzania & Uganda" zilizopo Kenya watazifunga.
Huu ndio undugu-asanteni Familia.🇰🇪
REPOST 200
On serious note : Chelsea wana vijana wengi wa kukabiliana na intensity ya ligi , ishu yao kubwa hawana calm heads mambo yakiyumba uwanjani . Unakuta asilimia kubwa wanapoteza kabisa umakini wao
Naelewa kwanini Alonso ana target wachezaji kama Welbeck , Hendo na Xhaka . You can banter all you want but kwangu mimi it make sense 100% .!
Inategemea tu na financial package inayohusika hapo. Ndio maana Chelsea waligoma kwenda zaidi kwa Xhaka . Fedha inayohusika kwa hao wachezaji ( transfer fee/ Salary ) inapaswa kuwa ya kawaida.