#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 319
Katuga: Kama Katibu Mkuu wa Chama chama chako kilishiriki uchaguzi?
Mnyika: Kilizuiwa Kushiriki?
Katuga: Kwenye hotuba ya Mwenyekiti ya Tar. 03/04 je ulisikia akisema kama unategemea kuwa mbunge sahau?
Mnyika: Aliwaambia uchaguzi utaahirishwa.
Katuga: Hotuba ya Mwenyekiti alisema na mimi nina nia ya kugombea katika kacheo fulani sahau?
Mnyika: Toa neno sahau weka neno utaahirishwa.
Katuga: Kama Chama cha siasa kama mlijiandaa kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025.
Mnyika: Tulijiandaa vizuri sana.
Katuga: Mlijiandaa kushiriki uchaguzi kwa mujibu wa Katiba?
Mnyika: Kwa mujibu wa Katiba iliyopo na marekebisho ya Katiba tuliyohitaji.
Katuga: Kwa haki hiyo hiyo ambayo Chadema alikuwa nayo na Vyama vingine vilikuwa na haki hiyo hiyo?
Mnyika: Haki ya kushiriki uchaguzi huru, wa haki na halali kila mtu anayo.
Katuga: Mwenyekiti alisema tutazuia uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia ulisema hivyo?
Mnyika: Sikutumia exactly maneno hayo Sikumbuki kama nilisema kama unavyotamka hapo. Mimi nilisema njia zilizotumika.
Katuga: Je hizo njia za kuzuia uchaguzi zilikuwa ni zipi?
Mnyika: Nilisema.
Katuga: Kuhamasisha uasi ni njia ya kidemokrasia.
Mnyika: Ndio
Katuga: Kuzuia uchaguzi usifanyike ni njia ya kidemokrasia kwa nguvu zote?
Mnyika: Kwa nguvu zote za kidemokrasia ni njia ya kidemokrasia.
Katuga: Kwahiyo ni maneno yako kuwa vyama vingine havikupaswa kushiriki?
Mnyika: Unasema wewe sio mimi.
Katuga: Uchaguzi huru, haki na halali je wa mwaka jana vyama vilikuwa na haki hiyo au havina?
Mnyika: Ni suala lao wenyewe kuitumia hiyo haki au la? Sijasema kama uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa huru na haki na halali.
Katuga: Kama Chama kimoja kinaenda kushiriki Uchaguzi ni demokrasia gani kwenda kuzuia?
Mnyika: Demokrasia ya kupinga na kuzuia uchaguzi au kuahirisha uchaguzi
Katuga: Njia gani itakayotumika ya kidemokrasia itakayotumika kumzuia mtu?
Mnyika: Ukienda kupiga kura peke yako wenzako wasiende hakutakuwa na uchaguzi hapo.
Katuga: Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema kila mtu anapaswa kuamini chochote ili mradi havunji sheria.
Mnyika: Inaruhusu.
Katuga: Je inaheshimu imani ya mtu ilimradi asivunje sheria?
Mnyika: Inaruhusu
Katuga: Je inaelekeza kumzuia mtu asiyeamini kitu fulani?
Mnyika: Inaelekeza kumueleimisha mtu.
Katuga: Sikiliza maswali kama mtu mwenye akili timamu.
Mnyika: Sikiliza Majibu yangu kama mtu mwenye akili timamu. Itakusaidia.
Katuga: Mwenyekiti kusema tutakinukisha, tutaenda kuzuia uchaguzi alilenga kunishikiza Serikali kufanyike mabadiliko ya sheria na Katiba?
Mnyika: Hapana. Hatukulenga Serikali. Maneno yetu tuliyaelekeza kwa umma na wananchi kwa ujumla.
Katuga: Huo msimamo wa No reforms No Election ulitekelezwa na nani?
Mnyika: Kamati Kuu.
Katuga: makamu mwenyekiti nae aliendeleza nia ya no reforms: No election?
Mnyika: Yupi huyo? Wako wawili.
Katuga: Bara?
Mnyika: Chama kilifungiwa kwa siku 309 kutokufanya hiyo mikutano.
Katuga: Viongozi waliendelea kuhamasisha umma kuhusu nia hiyo?
Mnyika: 09th June 2025 Chama kilifungiwa kufanya shughuli zake.
Part 320 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 320
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.
Katuga: Je huyu Heche katika kueneza hiyo nia alikuwa anaongea na waandishi wa habari?
Mnyika: Nimekwambia Tarehe 10/04 Chama kilifungiwa.
Katuga: Katuga una akili kweli?
Mnyika: Wewe unajiona una akili kweli?
Mhe. Lissu: Mheshimiwa haya maswali kila saa ya kwamba shahidi ana akili au vipi? Sheria inakataza. Kama hana maswali akae tu.
Katuga: Unajua au hujui Heche aliwahi kuongea East Africa radio kuhusu nia ya kuzuia uchaguzi?
Mnyika: Sijui
Katuga: Alitangaza kwamba uchaguzi wa 2025 hautakuwepo?
Mnyika: Sijui.
Katuga: Unajua au hujui kwamba katika uchaguzi wa 2025 kulikuwa na jaribio la kuuzuia huo uchaguzi, kufanya fujo.
Mnyika: Ninachojua kuna Mauaji yalifanyika.
Katuga: Je kulikuwa na jaribio la kuzuia uchaguzi kwa kuchoma vituo vya kura?
Mnyika: Sijui ndio maana tulitaka uchaguzi huru sisi.
Katuga: Ulikuwa nchini au haukuwa nchini?
Mnyika: Nilikuwa nchini?
Katuga: Ulijitokeza au hukujitokeza kwenye zoezi la uchaguzi?
Mnyika: Sikujitokeza kwasababu hakukuwa na uchaguzi.
Katuga: Kwa Msimamo wenu hakukuwa na uchaguzi?
Mnyika: Hakukuwa na uchaguzi huru, haki na halali.
Katuga: Ila nia ya kuzuia uchaguzi inadhihirika kwa maneno hayo?
Mnyika: Sio sahihi.
Katuga: Uchaguzi ule kuna mali za watu zilichomwa moto.
Mnyika: Nilijua kupitia hotuba ya Chande.
Katuga: Vilichomwa havikuchomwa?
Mnyika: Najua viliungua moto. Mambo ya kuchomwa sijui aliyechoma.
Katuga: Vituo vya mwendokasi je?
Mnyika: Nilipita na kuona vimeungua. Simjui aliyechoma.
Katuga: Maneno ya Mwenyekiti ya Tar. 03/04 kuwa tutakinukisha, tutazuia uchaguzi ni haki ya umma kutafsiri na kufanyia kazi?
Mnyika: Ni haki.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema ni haki pia umma kuchocheka na kukata wapiga kura vidole.
Mnyika: Sio haki.
Katuga: Mwenyekiti aliwaambia umma kuzuia uchaguzi zoezi hilo lifanyike lini?
Mnyika: Hakuwaambia.
Katuga: Ni haki au sio haki kuzuia uchaguzi sio ya kupiga kura?
Mnyika: Sio haki.
Katuga: Ulisema wewe ni accounting officer? Una elimu yoyote ya hesabu?
Mnyika: Nina elimu ya miaka 3 Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuhusu Bussiness Administration and Accounting sina Award yoyote.
Katuga: Ulisikiliza taarifa ya Chande yote au kipande?
Mnyika: Sio taarifa ni hotuba. Nilisikia yote.
Katuga: Ulisikia Chande akisema matukio ya Otober yalitokana kwasababu ya ushawishi wa wanasiasa kufanya machafuko?
Mnyika: Kwenye hotuba kuna vyanzo na viashiria
Katuga: una akili timamu kweli?
Mnyika: Nina akili timamu kuliko wewe na Maboss zako wote.
Katuga: Mimi ndio nimekuuliza una akili timamu?
Mnyika: Watu wasio na akili timamu mara nyingi huwa wanapenda kudhani wenye akili hawana akili. Sasa nina akili kuliko wewe.
Katuga: Mwenyekiti alikuwa anataka mabadiliko ya kisheria na kikatiba kwa njia zipi?
Mnyika: Alisema njia za kidemokrasia.
Katuga: Utofauti wa Chande na aliyosema mwenyekiti ni upi?
Mnyika: Chande alisema wakati Mwenyekiti yuko jela na Mwenyekiti alisema wakati Chande hajafanya kazi zote.
Katuga: Kwamba Kauli mbiu ni tumteteee kwa nguvu zote?
Mnyika: Kwamba Kauli Mbiu yenu huko Serikalini ni Tumfunge kwa Nguvu zote? Si ndio?
Katuga: Ulisema ulikuwa mbunge wa wapi na wapi?
Mnyika: Ubungo na Kibamba.
Katuga: Kwahiyo unauelewa kidogo wa masuala ya Sheria?
Mnyika: Nimetunga sheria nafahamu
Part 321 inaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 321
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika.
Katuga: Tanzania ni nchi huru na ina katiba yake?
Mnyika: Yes ina katiba yake na haiongozwi na Katiba pekee ipo Mikataba ya Kimataifa na Sheria zingine.
Katuga: Mahakama ndio chombo cha Mwisho kutamka mtu ana hatia au hana hatia?
Mnyika: Mahakama za Tanzania na Kimataifa.
Katuga: Mahakama ni Chombo cha Mwisho kwa mujibu wa Katiba kuamua kama mtu ana hatia au hana hatia?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Je ni kweli ni Mahakama itakayotamka ushahidi huu unatosha au hautoshi kumtia mtu hatiani?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Uliposema mshitakiwa aliposema kuwa mshitakiwa ameshitakiwa kuwa ni kesi ya uongo kwa majibu yako yaliyopita wambie Majaji kwamba kwenye hizo kesi ulizosema ni za uongo ni kesi gani uliitaja?
Mnyika: Zilifutwa zote kwasababu zilikuwa za uongo.
Katuga: DPP akifuta kesi anaweza kuirudisha au hawezi kuirudisha?
Mnyika: Anaweza kuirudisha.
Katuga: DPP akifuta kesi anasema kwa maslahi mapana ya Jamhuri?
Mnyika: Sio sababu pekee.
Katuga: Mihimili ya dola ya Tanzania unaijua?
Mnyika: Mitatu ipo, naijua
Katuga: Kwenye mambo ya kisheria unajua muhimili gani unahusika?
Mnyika: Ndio.
Katuga: Ni Bunge pekee lenye mamlaka ya kutunga sheria?
Mnyika: Sio Bunge pekeee.
Katuga: Mahakama ina jukumu la kutafsiri sheria?
Mnyika: Sio jukumu pekeee.
Katuga: Serikali kazi yake ni kusimamia sheria?
Mnyika: Sio kazi pekeee
Katuga: Hata Bunge linaweza kusimamia sheria pia. Wanaisimamia serikali pia.
Katuga: Vyombo vinavyotumika kulinda amani?
Mnyika: Vyombo vya serikali kama Polisi na pia mihimili yote pia.
Katuga: Vyombo ulivyotaja vyenye jukumu la kulinda Amani viko chini ya nani?
Mnyika: Vyombo gani?
Katuga: Polisi na Jeshi?
Mnyika: Chini ya Rais.
Katuga: Unapotishia kuvunja amani ni tishio la Rais na Vyombo vyake?
Mnyika: Sio kweli, sio kila tishio la Amani ni tishio kwa Rais na vyombo vyake.
Katuga: Siku ya Tarehe 29/10 Amani ilikuwepo au haikuwepo?
Mnyika: Kulikuwa na vurugu lakini Amani ilikuwepo si Serikali yenyewe imesema kulikuwa na Amani.
Katuga: IGP si alitangaza kukaa ndani tarehe 29/10?
Mnyika: Ndio
Katuga: Alisema IGP kuwa msitoke?
Mnyika: Hatuwezi kumuamini hata kama alisema.
Katuga: Kule Goba hukusikia mitutu ya Bunduki?
Mnyika: Nani amekwambia nilikuwa Dar es salaam? Nilisema nilikuwa Nchini.
Katuga: Vyombo vya Ulinzi vilikuwa na jukumu la kurudisha amani?
Mnyika: Sifahamu.
Katuga: Kuchoma mali za watu, miundombinu na kukata watjmu vidole ni uvunjifu wa Amani?
Mnyika: Ni uvunjifu wa Sheria.
Katuga: Unafahamu au hufahamu kuwa ni uvunjifu wa amani?
Mnyika: Ni uvunjifu wa sheria.
Katuga: Kutishia kuivunja amani ni kuitishia serikali yenye jukumu la kulinda hiyo amani? Unafahamu hilo?
Mnyika: Ndio nasikia kwako sifahamu mimi.
Katuga: Wambie Majaji kama unafahamu au hufahamu kwamba kila baada ya miaka mitano ni lazima kuwe na uchaguzi Mkuu?
Mnyika: Sio lazima.
Katuga: Ibara ya 65 kwamba Bunge litavunjwa kila baada ya miaka mitano.
Mnyika: Zipo ibara nyingi zinazosema extension ya Bunge na masharti mengine kuhusu Bunge.
Katuga: Kila Bunge linapovunjwa ndio ukomo wa Rais si ndio?
Mnyika: Sio kweli Bunge linavunjwa lakini Rais anaendelea kuwa Rais hadi atakapopatikana Rais mwingine.
Katuga: Ukomo wa term ya Urais unaisha Bunge likivunjwa si sahihi ibara ya 38?
Mnyika: Inasema kwa kuzingatia na taratibu zingine. Term inaisha lakini urais anaendelea nao hadi apatikane Rais mwingine ndio maana anaweza kuitisha tena Bunge.
Katuga: Mbona hujibu wewe unamuangalia jamaaa?
Mnyika: Namuangalia Jaji na wewe kati yenu nani ndio jamaaa?
Katuga: Kutishia kuivunja Sheria ni kuitisha Serikali?
Mnyika: Sio lazima.
Katuga: Serikali inaweza kutishika na tishio la kuvunja sheria?
Mnyika: Sio lazima.
Part 322 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 322
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika.
Katuga: Ulisema mlipokamatwa na Sugu wenzako walipelekwa kusikojulikana?
Mnyika: Ndio
Katuga: Kusikojulikana ni wapi?
Mnyika: Ndio maana hakujulikani
Katuga: Ni sehemu wewe usiyoijua au wewe usikokujua?
Mnyika: Nisipopajua na hapajulikani.
Katuga: Unajua ama hujui huyu aliyepelekwa kusikojulikana alipelekwa nyumbani kwake?
Mnyika: hata mimi nilisema hapa kuwa nilipelekwa central na baadae nyumbani.
Katuga: Yeye aliiambia Mahakama kuwa alipelekwa iringa kuna mbu wakubwa
Mhe. Lissu: Mimi sikusema mambo ya Iringa sijui ametoa wapi hili swali. Mimi sikupelekwa iringa na sikusema hivyo.
Jaji Ndunguru: Acha tu sisi tunaandika majibu yake. Maswali hatuna shida nayo.
Katuga: Kuonesha jinsi gani uanaharakati una malipo...
Mnyika: Nilisema Gharama hayo malipo unayatoa wapi?
Katuga: Milioni 350 ulisema hamjarudishiwa?
Mnyika: Hadi leo ndio Jamhuri walipaswa kutulipa hizo pesa.
Katuga: Ulitaja kesi nyingi sijui Nyamongo au wapi je umewatajia namba za hizo kesi?
Mnyika: Namba za nini nitaje? Sijataja.
Katuga: Je hati za mashitaka ulileta?
Mnyika: Sijaleta. Mimi sio shahidi wa Jamhuri.
Katuga: Je Mbowe nae alifunguliwa kesi ya Uongo ya ugaidi?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Ulisema alienda ikulu ilikuuma sana?
Mnyika: Inaniuma kumsingizia mtu ugaidi halafu mawakili wa serikali mmeshindwa kuthibitisha kesi inafutwa halafu gaidi anaenda kupokelewa ikulu. Hiki ndio kinaniuma na ni uongo huu.
Katuga: Unamjua Chura? Nitafute baadae nikusimulie kwanini ana mabaka. Unajua Chura ana mabaka..
Mnyika: Umesema nikutafute baadae. Kwahiyo kama unaendelea kumuhadisia hapa wahadisie majaji mimi nitakutafuta baadae. Sasa hivi sikusikilizi.
Watu wanacheka.😀😀😀😀
Katuga: Sasa Mbowe alishitakiwa na watu wengine ambao walikuwa wanajeshi?
Mnyika: Nilisikia Mahakamani.
Katuga: Wale Walinzi wake hawakuwa wanaharakati wa Katiba Mpya?
Mnyika: Kumlinda Mwenyekiti ni kuwa Mwanaharakati wa Katiba Mpya pia.
Katuga: Ulisema ulikuwa afisa maduhuri
Mnyika: Ni Masuhuli. Hiyo maduhuri kaitumie kwenye ofisini kwenu.
Katuga: Ulihusika kuwalipa posho?
Mnyika: Posho za Safari nilikuwa nawalipa.
Katuga: Je ulikuwa uanatembea nao mnalala pamoja na kula nao kujua yote?
Mnyika: Sikuwa natembea nao ili kujua yote.
Katuga: Ulikuwa pia hujui ushahidi wa tuhuma walizokuwa nazo kwasababu ulikuwa hutembei nao?
Mnyika: Nilisikia mahakamani wanayosema. Kwani mapolisi wakienda kutoa ushahidi walikuwepo?
Katuga: Ulisema kesi hii ni mwendelezo wa serikali kubambikiza kesi?
Mnyika: Ndio kupitia jeshi la polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zake. Lakini sio kubambikizia watu kesi.
Katuga: Ni sheria gani inayompa Mwenyekiti wa Chadema kinga?
Mnyika: Kama amefanya kosa hana kinga lakini hana kosa lolote.
Part 323 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 323
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea na maswali yake ya Kiwaki ila Mnyika anampa za uso.
Katuga: Unasema Msajili aliwaandikia barua kuhusu Kauli za Mwenyekiti?
Mnyika: Ndio
Katuga: Nae alimtuhumu Mwenyekiti?
Mnyika: Tuhuma za kisiasa ndio alituhumiwa nazo.
Katuga: Kuhusu kusaini au kutokusaini sheria hailazimishi?
Mnyika: Hailazimishi.
Katuga: Kushiriki uchaguzi ni haki ya Kikatiba?
Mnyika: Ndio ni kweli.
Katuga: Kunyimwa kutoshiriki uchaguzi kwa chama chenu na kuvunjwa kwa haki hiyo sheria inaruhusu kuidai Mahakamani haki hiyo?
Mnyika: Sio lazima uende mahakamani.
Katuga: Mlienda Mahakamani kudai haki yenu ya Kikatiba au hamkwenda?
Mnyika: Sio lazima twende Mahakamani soma kesi ya Kubenea Mahakama ilisema haki za kisiasa zinapaswa kutafutwa kwa njia za kisiasa pia.
Katuga: Wanasiasa wa Chadema ni dhumuni lao kushika nafasi ya uongozi kwenye hili Taifa?
Mnyika: Sio dhumuni pekee.
Katuga: Ulisema una akili nyingi sasa nikuulize swali...
Mnyika: Nilichosema nina akili nyingi kuliko wewe na Maboss zako. Sio nina akili kuliko watu wote Duniani. Ni muhimu ukaelewa ni akili nyingi kuliko wewe Katuga na Maboss zako.
Katuga: Kufanya mapinduzi ni njia mojawapo au sio njia ya kushika dola?
Mnyika: Ni njia lakini sio njia ya kidemokrasia.
Katuga: Uchaguzi wa Tanzania ulisema sio nini?
Mnyika: Sio huru, sio haki na sio halali.
Katuga: Ule uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wa nini?
Mnyika: Ulikuwa ni uporaji wa mamlaka ya wananchi wa kuchagua viongozi wanaowataka. Hakukuwa na uchaguzi, ni uchafuzi na uharibifu wa rasilimali za Taifa.
Katuga: Mheshimiwa imefika saa saba tumesimama toka asubuhi naomba twende Break kwa lisaa limoja na nusu.
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo siku ya Jumatatu Agosti 31, 2026
Last time tuliishia part 305 so leo tunaendelea na -;
Part 306
Muda huu ni saa tatu na madakika asubuhi naambiwa Mwenyekiti alishafika mazingira ya Mahakama majira ya saa tatu kasorobo.
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ambae ni shahidi namba mbili wa utetezi nae alishafika mapema sana tangu majira ya saa mbili kamili asubuhi.
Mahakama inakaribia kuanza.
Majaji wameingia tayari.
Mh. Lissu ameingia tayari ameshangaa kumuona Mwandishi wa ITV ana marasta anamuuliza na wewe uko kama mimi?😂
Watu wanacheka 😀😀😀😀
Leo Mhe. Lissu amekula Kombati yake ya Kaki ina mikono mifupi.
Majaji wanateta pale juu na Wakili wa Serikali Thawabu Issa anampatia karani wa Mahakama karatasi anaisogeza kwa Jaji Ndunguru, nafikiri ni majina ya mawakili wa serikali.
Anasimama Karani anasoma kesi namba kama kawaida Ajuaye Zengeli anasimama anatambulisha kikosi chake hapa. Na kusema wako tayari.
Jaji anamuita Shahidi, John Mnyika anapanda kizimbani.
Amefika Kizimba cha kwanza amepiga ishara ya msalaba pale kizimbani, huyu ni seminari OG na ukatoliki wake utamtambua kwa matendo yake.
John Mnyika amevaa Tshirt nyekundu iliyoandikwa maneno yafuatayo "HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE" Mitahali 14:34
Jaji Ndunguru anasema Shahidi nakukumbusha uko chini ya kiapo.
Mhe. Lissu: Shahidi salama maana hatuonani?
John Mnyika: Amani na Salama.
Mh. Lissu: Sasa tuendelee wakati unazungumzia mambo niliyosema kuna mengine yoyote?
Mnyika: Mwenyekiti Tundu Lissu katika hotuba yake alielezea masuala yanayohitaji mabadiliko katika mifumo yetu ya Uchaguzi alisema mambo hayo ni masuala aliyoyafanyia utafiti wa muda mrefu na pia alielezea mambo ambayo yamezungumzwa na waangalizi wa uchaguzi.
Baadhi ya mambo ninayoyakumbuka aliyoyasema Mwenyekiti Lissu ni
1. Mgawanyo wa majimbo kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu yaani population quota,
2. Kuwepo na tume huru ya uchaguzi na kuondoa madaraka ya Rais kuteua wajumbe wa tume,
3. Tume ya uchaguzi kuwa na watumishi wake huru badala ya kutumia wakurugenzi na watumishi wengine wa umma.
4. Kuweza kupinga matokeo ya Urais Mahakamani.
Na baadae Mwenyekiti akaeleza namna ambavyo kutokuwepo uchaguzi huru na Haki ambako kulipelekea kwamba HAKUNA UCHAGUZI TENA TANZANIA.
Mhe. Lissu: Wewe unasemaje hawa wanasema mimi ndie nilichapisha YouTube hayo maneno?
Mnyika: Hilo shitaka ni la uongo na la kubambikiza kwasababu Mwenyekiti wa Chama hahusiki na chochote kuhusu masuala ya waandishi wa habari na kazi zao.
Waandishi wa habari waliachwa huru kufanya kazi yao kwa kadri ya uhuru wa vyombo vya habari. Hawakupewa maelezo yoyote kuhusu kuchapisha au kutochapisha taarifa.
Mhe. Lissu: Wanasema nilichapisha maneno yafuatayo, mambo ya kukinukisha vibaya..
Mnyika: Binafsi sifahamu aliyechapisha hayo maneno na baada ya kusikia kuna kesi Mahakamani kuhusu jambo hili nikaelezwa kuwa kuna maneno yamechapishwa na Jambo TV.
Ninachoweza kusema kuhusu mkutano huo na waandishi wa habari kuwa ulikuwa wa masaa zaidi ya matatu kwahiyo haiwezekani mtu akachukua maneno machache na kuchapisha nje ya maana iliyokusudiwa.
Mhe. Lissu: Nani aliyekwambia maneno hayo kwamba yamechapishwa na Jambo TV?
Mnyika: Mwanasheria Mkuu wa Chama, Dr. Rugemeleza Nshala.
Mhe. Lissu: Hatua gani ulichukua kuhakiki ukweli wa hizo taarifa?
Mnyika: Nilifuatilia kwenye mtandao wa Jambo sijawahi kuona kwenye mtandao huo hotuba fupi yenye maneno hayo peke yake. Nilichokiona ni video link iliyokuwa na mkutano wa takribani masaa matatu. Sijawahi kuyaona maneno hayo yakiwa yamechapishwa kwenye jambo TV yakiwa peke yake.
Part 307 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 307
Mhe. Lissu: Msimamo huu unaashiria uasi maana yake ni nini?
Mnyika: Niliwahi kusikia maneno ya Mwalimu Nyerere akisema Taifa linahitaji vijana waasi dhidi ya mifumo kandamaizi na sijawahi kusikia ameshitakiwa kokote kwa Uhaini wala Ugaidi kwahiyo sioni kama kuna kosa lolote kwenye maneno hayo.
Mhe. Lissu: Kuna shida gani mtu kuhamaisha uasi?
Mnyika: Hakuna tatizo lolote maana sisi Kidemokrasia maana yake ni kuhamasisha watu kukataaa, kupinga mambo fulani.
Mhe. Lissu: Kuna shida gani mtu akisema tutazuia uchaguzi?
Mnyika: Hakuna shida maana mtu anaweza kutumia njia mbalimbali za kidemokrasia mfano kushinikiza mamlaka kuahirisha uchaguzi.
Kuna njia ya kususia Uchaguzi yaani watu wasiposhiriki, uchaguzi unakuwa haupo na haujafanyika ni njia ya kidemokrasia pia niliwahi kusoma wakati naanza
Mhe, Lissu: Acha huko kwanza. Mtu akisema wanasema msimamo huu unaashiria uasi ........ uchaguzi huu tutauvuruga hapa anakuwa ameitishiaje serikali???
Mnyika: Sijaona mahali ambapo Serikali imetajwa kwahiyo sioni ni kwa namna gani serikali inaweza kuwa imetishwa hapo
Mhe, Lissu: Huu msimamo wa kuzuia uchaguzi ulitokea wapi?
Mnyika: Baada ya kukwama katika mazungumzo ambayo nilisema hapo awali na serikali. Walipeleka miswada mitatu ya sheria na miwili inahusu Uchaguzi.
Tarehe 09/01/2024 nilitumwa na Kamati Kuu ya Chama kwenda mbele ya Kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala iliyokuwa na jukumu la kupokea maoni kuhusu miswada hiyo ya sheria.
Ambapo tulipeleka msimamo wa Chama wa kutaka marekebisho ya Kikatiba na kisheria kuwezesha Chaguzi za 2024 uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule Uchaguzi Mkuu 2025 kufanyika katika mazingira huru na haki.
Mhe. Lissu: Nini kilitokea?
Mnyika: Mapendekezo yote kuhusu Katiba nilizuiwa kuzungumza na nilizimiwa kipaza sauti. Na mapendekezo ya sheria kwa sehemu kubwa yalikataliwa.
Baada ya hapo ulifanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kanuni zilizotungwa na Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI ambae ni Mchengerwa. Na mnyororo mzima ulihusisha watumishi wa TAMISEMI ngazi mbalimbali na serikali kuu hali iloyopelekea sehemu kubwa ya wagombea wa Chadema kuondolewa na hujuma zingine mbalimbali.
Mhe. Lissu: Unamaanisha nini?
Mnyika: Zaidi ya asilimia 90 walienguliwa kwenye kinyang'anyiro na wagombea waliobaki waliondolewa na Polisi na matokeo. Na kulikuwa na matukio kwa baadhi ya maeneo watu kukamata masanduku ya kura kukamata kura ambazo zimeshapigwa.
Mhe. Lissu: Sababu za kuondolewa hao wagombea ilikuwa ni nini?
Mnyika: Wagombea waliambiwa hawajui kusoma na kuandika na wengine sio wakazi wa eneo husika?
Mhe. Lissu: Nini kilifuata baada ya hapo?
Mnyika: Tarehe 02 na 03 December 2024 tuliitisha Kikao cha Kamati kuu kutathmini yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024
Mhe. Lissu: Nani alikiitisha uwe specific?
Mnyika: Nilikiitisha mimi Katibu Mkuu wa Chama mara baada ya kushauriana na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwani yeye ndie Mwenyekiti wa Kikao. Tukakubaliana ndio tukaitisha kikao cha dharula. Kikao hicho kilipokea taarifa, kikajadili na kikapitisha maazimio 10 na nitasema machache tu.
1. Kwa yaliyotokea November 27, 2024 hakukuwa na uchaguzi huru wala halali wala wa Haki wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji.
2. Hakuna tena uwezekano kwa mazingira yaliyopo ya Katiba na sheria wa kuwa na uchaguzi huru na wa Haki Tanzania.
3. Chama kiwaunganishe Watanzania kutaka mabadiliko na marekebisho ya Kikatiba na Kisheria kabla ya Uchaguzi wa Udiwani, Ubunge na Urais wa mwaka 2025.
4. Na kwamba bila mabadiliko hakuna Uchaguzi. No Reforms, No Election.
Part 308 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 308
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Baada ya hapo nini kilitokea?
Mnyika: Tarehe 10 December, 2024 tuliitisha Mkutano na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Chama Mikocheni ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe aliyatangaza maazimio hayo kwa umma.
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya hapo?
Mnyika: Chama kiliingia katika maandalizi ya Mkutano mkuu wa Chama na kupokea mpango wa chama kwa miaka mitano. Na Tar. 20/01/2025 nilipeleka taarifa ya Kamati Kuu kwa Baraza Kuu la Chama iliyopendekeza pamoja na mambo mengine maazimio yale 10 ikiwemo la No Reforms: No Election
Mhe. Lissu: Ili iweje?
Mnyika: Ili maazimio yale yasiwe tena ya Kamati Kuu bali yawe ya Baraza Kuu. Pia, Baraza Kuu liyapeleke kwenye Mkutano Mkuu ili maazimio hayo yawe ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chama na sio ya Baraza Kuu pekeee. Na Baraza Kuu la Tarehe 20/01/2025 liliridhia mapendekezo yote mawili.
Lissu: Baada ya Baraza Kuu nini kiliendelea?
Mnyika: Tar. 21/01/2025 Niliwasilisha taarifa ya Baraza Kuu kwa Mkutano Mkuu juu ya utendaji wa Chama kwa miaka mitano. Na ndani ya taarifa hiyo nilipeleka mapendekezo ya Baraza kuu ambayo yalihitaji kwenda kupata Baraka za Mkutano Mkuu.
Anaendelea JJ. Mkutano Mkuu kupitisha maamuzi ya kutaka kufanyika mabadiliko ya Kisheria na Kikatiba kabla ya Uchaguzi wa 2025 yenye kuwezesha kuwepo na uchaguzi huru na haki na kwamba bila mabadiliko hayo hakuna Uchaguzi. No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Nani aliyekuwa Mwenyekiti wa Vikao vyote hivyo?
Mnyika: Mwenyekiti Freeman Mbowe wa wakati huo ndio aliongoza vikao vyote hivyo.
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya Mkutano Mkuu kupitisha azimio hilo?
Mnyika: Iliendelea agenda ya Uchaguzi Mkuu wa Chama ambayo iliendelea hadi Tarehe 22/01/2025 na katika Uchaguzi huo alichaguliwa Mwenyekiti Mpya wa Chama, Tundu Lissu na Makamu Wenyeviti Wawili ambao ni John Heche, Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Said.
Mhe. Lissu: Mkutano Mkuu uliamua nini kuhusu utekelezaji wa maazimio yake?
Mnyika: Utekelezaji uanze mara moja baada ya uchaguzi kukamilika.
Mhe. Lissu: Nini kilifuata?
Mnyika: Siku hiyo hiyo ya Tar. 22/01 Baraza Kuu lilikaa na Katibu Mkuu wa Chama, John John Mnyika aliteuliwa na manaibu katibu wakuu wote waliteuliwa. Na Baraza kuu lilipokea mapendekezo pia ya wajumbe wa Kamati Kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitisha uteuzi wao.
NB. JOHN JOHN MNYIKA ni Maktaba inayotembea yani Mhe. Lissu hakukosea kumteuwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama, anateleza kama hataki tu.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea sasa kuhusu maazimio ya No Reforms, No Election?
Mnyika: Niliitisha retreat na vikao vya sekretarieti, Viongozi wakuu na Kamati Kuu ya Chama vilivyofanyika Bagamoyo kuanzia Tar. 31/01 hadi 04/02 kwa ajili ya utekelezaji wa azimio hilo la No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji mpango wa utekelezaji mlioufikia kwenye vikao hivyo?
Mnyika: Tulipitisha mpango wa kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya nchi, tulipitisha mpango wa kuwatembelea viongozi wa dini, sekta binafsi na taasisi zingine za kijamii. Tulipitisha mpango wa kuzungukia vyombo vua habari na kukutana na wahariri wa vyombo vya habari, tulipitisha mpango wa kushawishi jumuiya za kimataifa na jumuiya za kikanda, tulipitisha mpango wa kukutana na wadau mbalimbali ndani ya Chama.
Mhe. Lissu: Utekelezaji ukawaje huo?
Mnyika: Mwenyekiti alianza ziara akiambatana na viongozi wengine. Mfano alikutana na Shekhe Ponda Issa Ponda. Kwa watu mashuhuri alikutana na Jaji Joseph Sinde Warioba na kwa upande wa kuvihusisha vyombo vya habari Mwenyekiti alifanya mkutano mwezi February kuelezea maazimio ya Kamati kuu ya Bagamoyo na Baadae Tarehe 02 March alikutana na Wahariri wa Vyombo vya habari.
Part 309 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 309
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Kuhusu Jumuiya ya Kimataifa je?
Mnyika: alitembelea balozi mbalimbali ikiwemo ubalozi wa Marekani. Sina orodha yote hapa.
Mhe. Lissu: Ikawaje?
Mnyika: Baadae tuliitwa ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa hapa Dar es salaam. Tulipofika tukamueleza maana ya No Reforms, No Election na tukamueleza kama oparesheni yetu hiyo inaendana na sheria za vyama vya siasa. Maana alituhoji kutaka kujua maana ya No Reforms: No Election.
Msajili wa Vyama vya siasa akasema haoni shida yoyote ya kisheria na baadaye akaja kutoa kauli kwa umma mbele ya vyombo vya habari Tarehe 10/02/2025 kuwa No Reforms: No Election ni kauli mbiu ya kisiasa haikiuki sheria yoyote.
Mhe. Lissu: Hiyo Tarehe 17/03/2025 nje ya Delegation yako nani mwingine alihudhuria?
Mnyika: Namkumbuka Sisty Nyahoza?
Mh. Lissu: Shost Nyahoza?
Mnyika: Anarudia mara nne nne.. Sisty Nyahoza, Sisty Nyahoza.
Mhe. Lissu: Nilisikia vibaya kama umesema Shost Nyahoza. Basi sawa, waeleze Majaji utekelezaji wa maazimio kwa upande wa umma ilikuwaje?
Mnyika: Tulipanga Mikutano ya Hadhara kanda ya Nyasa yenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa na mkutano mkubwa wa ufunguzi ulifanyika Mbeya Tar. 23/03/2025.
Mhe: Lissu: Hiyo Ziara ilikuwa hadi lini?
Mnyika: Iliendelea kuanzia hiyo Tar. 23/03 hadi Tarehe 02/04 tulipopanga kikao na watia nia wa uchaguzi wa Chama.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea baada ya Mkutano wa watia nia?
Mnyika: Tulipanga ifanyike Mtwara, Lindi na Ruvuma. Misafara ya maandalizi ikaanza. Makamu Mwenyekiti wa Chama John Heche alikuwa mmoja wapo hadi Tar. 09/04 kule Mbinga, Ruvuma.
Mhe. Lissu: Sasa ule mkutano na watia nia ulikuwa na utofauti gani na mikutano mingine ya hadhara?
Mnyika: Msimamo wa Chama wa No Reforms: No Election na hoja zetu zilikuwa ni zilezile. Isipokuwa kabla ya Mkutano wa Tar. 03/04/2025 nilikuwa nimepokea waraka wa baadhi ya watia nia waliokuwa na mapendekezo ya kutaka chama kibadili msimamo wake. Kwahiyo katika mkutano wa Tar. 03/04/2025 hoja hizo hizo zilizosemwa kwenye mikutano ya hadhara zilitumika kutoa majibu na kukumbusha juu ya msingi wa msimamo wa Chama wa No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Nafikiri nikurudishe tena kwenye hayo maneno wanayosema ni uhaini wewe unaelewa nini?
Mnyika: Hayo ni maneno ya kisiasa yanayotumika kuhamaisha umma ili ukatae kwa maana ya kuasi, umma uone uchaguzi una uozo mkubwa, unanuka na umma uwezo kukataaa. Uchaguzi uweze kuharibika, na umma uchukue hatua za kuzuia uchaguzi usio wa halali.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji baada ya huo mkutano wa Tar. 03/04 ulilijulisha jeshi la Polisi kuhusu maneno hayo?
Mnyika: Sijawahi kuwaambia chochote.
Mhe. Lissu: Je ulitoa maelekezo yoyote kuhusu tuhuma hizi kwa maafisa wa Chama?
Mnyika: Sikutoa kabisa.
Mhe. Lissu: Je jeshi la Polisi limewahi kukuhoji chochote kuhusu maneno hayo?
Mnyika: Sijawahi kuhojiwa lolote na jeshi la Polisi.
Mhe. Lissu: Je una ufahamu wowote wa hatua alizochukuliwa yeyote kati ya wale waliokuwepo pale makao makuu?
Mnyika: Hakuna mtia nia yeyote aliyekamatwa wala kuhojiwa na Polisi.
Mhe. Lissu: Je ufahamu wako kuhusu hatua alizochukuliwa mwandishi wa habari yeyote?
Mnyika: Sina taarifa za kwamba kuna mwandishi yeyote alichukuliwa hatua kwa jambo hilo kwa hiyo naweza kusema hakuna mwandishi aliyekamatwa wala kuhojiwa kuhusu kutenda makosa ya kusambaza na kuchapisha picha taarifa za mkutano huo.
Mhe. Lissu: Unasema ulipanga huo mkutano, ulitoa pesa na kusimamia maandalizi yote. Walichukua hatua gani polisi dhidi yako?
Mnyika: Hakuna hatua yoyote dhidi yangu au mtu mwingine yeyote ndani ya sekretarieti ambae alikamatwa au kuhojiwa kuhusu taarifa hizi au kuandaa mkutano na kikao hicho.
Mhe. Lissu: Je kuna mtu yeyote aliyeshitakiwa kwa kushiriki mkutano, kupanga au kuhusika na mkutano huo wa Tar. 03/04 hayupo huyo mtu mwingine.
Part 310 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 310
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya mimi kukamatwa na kushitakiwa kwa uhaini?
Mnyika: Siku ile ile Tar. 09/04 zilisainiwa nyaraka za kukishitaki Chama na kutaka kizuiwe kufanya kazi zake na kesho yake Tar. 10/04 mahakama ilitoa zuio hilo la kukizuia chama kufanya shughuli zake na matumizi ya mali za Chama.
Pia Msajili wa Vyama vya siasa alikuwa ametuandikia Barua ya kujieleza juu ya uhalali wa Katibu Mkuu wa Chama na Wajumbe wa Kamati Kuu ambao walikuwa wamethibitishwa kwenye Baraza Kuu na baada ya majibishano ya Barua. Aliandika barua na kusambaza kwa umma ya kutotambua uteuzi wa Katibu Mkuu, manaibu wake na sekretarieti ya Chama.
Huyu Msajili pia alituandikia barua ya kuzuia Ruzuku ya Chama na kipindi hicho hicho Tar. 12/04/2025 Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alisema CHADEMA haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi kwasababu hajasaini fomu za maadili ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea?
Mnyika: Msajili alituandikia barua ya kutaka maelezo kuhusu kauli za Mwenyekiti hizo za Tarehe 03/04 na aliandika Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya siasa.
Mhe. Lissu: Barua ya Sisty ilisemaje kuhusu uhaini wa maneno ya Mwenyekiti Lissu?
Mnyika: Hakukuwa na chochote kwenye barua ya Sisty kuhusu maneno ya Mwenyekiti kuwa ni ya kihaini?
Mhe. Lissu: Ulichukua hatua gani baada ya hapo?
Mnyika: Tuliwaandikia majibu kuwa jambo hilo tayari linashughulikiwa na mamlaka nyingine kwahiyo tusubiri matokeo ya mamlaka zingine.
Mhe. Lissu: Umesema ni mashitaka ya uongo waeleze Majaji kwanini?
Mnyika: Umetuhumiwa kwa uhaini kusema maneno ya kawaida ya kisiasa, wanasema uliitisha mkutano wakati hukuitisha wewe niliitisha mimi na sekretarieti, unatuhumiwa kuchapisha maneno hayo wakati maneno hayo hukuchapisha wewe walichapisha waandishi wa habari. Unatuhumiwa kwa kuwa na nia ya kutenda kosa hilo wakati ulichokifanya ni kutekeleza maazimio ya vikao halali vya Chama na kwanini utuhumiwe peke yako na sio na viongozi wengine. Unatuhumiwa kuhamasisha watanzania kutumia mamlaka yao kudai uchaguzi huru, haki na halali dhidi ya wanaoasi na kuhaini mamlaka ya wananchi ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Baada ya hili jibu watu wote wametabasamu. 😂😂
Na mimi nimeanza kutafakari Rozali aliyovaa John Mnyika, nitakuletea uchambuzi wake muda sio mrefu kutoka kwa mseminari niliyenae hapa.
Mhe. Lissu: Unafahamu vitendo ambavyo nimewahi kufanyiwa kihistoria?
Mnyika: Nafahamu umefunguliwa makesi mengi toka utawala wa Rais Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia.
Na nakumbuka Tar. 11/08/2024 tulipigwa na kufanyiwa matendo mabaya na jeshi la Polii, sina neno zuri la kuelezea lakini tukiwa ofisi za Chadema Mbeya walituvamia na kutupiga na kuturudisha Dar es salaam, waliongozwa na kamanda wa oparesheni Awadhi na RPC.
Walinisafirisha hadi Njombe na baadae hadi Dar es salaam na waliponifikisha Dar es salaam nikiwa nimejeruhiwa waliniambia nijidhamini na wakaninipeleka hadi nyumbani na kwakuwa nilikuwa nimeumia nikaenda hospitali kwa ajili ya matibabu.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea kwangu mimi na Sugu ambae unasema pia ilikuwaje?
Mnyika: Na nyie mlisafirishwa hadi Dar es salaam.
Sasa nimemaliza kuelezewa maana ya rozali aliyovaa Katibu Mkuu wa Chadema.
Pata huu uzi wakati Majaji wanajadiliana jambo kidogo.
Pale Kizimbani JOHN JOHN MNYIKA. Shahidi Na. 02 wa Utetezi anaonekana amevaa kitu kama Rozali hivi ina msalaba lakini sio Rozali ya kawaida. Nimemuuliza mchambuzi mmoja hapa anasema:
Rozali ile ni rozali za shirika la wafransisko wanazovaa wakatoliki (Franciscans)
Unaambiwa Kuna aina maalumu zinazohusishwa na utamaduni wao wa Kifransisko, ingawa si kwamba kila rozari ya Kifransisko ni tofauti kabisa na Rozari Takatifu ya kawaida.
Part 311 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 311
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Sasa hii rozali aliyovaa Mnyika huwa inajulikana kama Franciscan Crown Rosary, kwa Kiswahili unaweza kusema Rozari ya Taji ya Kifranzisko (Seraphic Crown).
Tofauti kubwa ni kwamba ina mafumbo saba badala ya mafumbo matano ya Rozari Takatifu ya kawaida.
Mafumbo hayo saba yanahusu furaha saba za Bikira Maria, hasa matukio ya furaha katika maisha yake pamoja na utukufu alioupokea kutoka kwa Mungu.
Kwa kawaida inakuwa na miongo saba (decades), yaani jumla ya Salamu Maria 70, badala ya Salamu Maria 50 za rozari ya kawaida.
Rozali hii ina uhusiano mkubwa na Mtakatifu Fransisko wa Asizi na mapokeo ya Kifranzisko ya kumheshimu sana Bikira Maria.
Jina "Seraphic Crown" linahusishwa na mapokeo ya Wafransisko kama Order of the Seraphic Wafransisko wanahusisha sana utambulisho wao na malaika maserafi na moto wa upendo wa Mungu.
Kuna pia mapokeo maarufu kuhusu Mt. Bernardine wa Siena, ambaye alihusishwa na ibada hii, ingawa historia ya asili yake ina maelezo na mapokeo mbalimbali.
Unaambiwa Lengo lake ni kumheshimu Maria kwa kutafakari furaha saba za maisha yake, na kupitia hizo kumtafakari Kristo.
Kuna pia rozari nyingine zinazohusishwa na Wafransisko, kama Tau Cross rosaries (zenye msalaba wa Tau), na hii ndiyo aina aliyoivaa JOHN JOHN MNYIMA.
Msalaba wa Tau (Τ) ni alama maarufu sana ya Kifranzisko na unahusishwa na Mt. Fransisko wa Asizi.
Rozali hii yenye herufi “T”, mara nyingi alama hiyo inahusishwa na Wafransisko (Franciscans) na Tau Cross (Msalaba wa Tau).
“T” ni Msalaba wa Tau (†/T), ambao ni alama ya kale ya Kikristo.
Mtakatifu Francis wa Assisi aliupenda sana msalaba huo na kuutumia kama ishara ya toba, wokovu na kujitoa kwa Kristo.
Kwa hiyo, Wafransisko wameutumia kwa muda mrefu kama alama ya utambulisho wa shirika lao.
Kwenye rozali, alama hiyo inaweza kuonyesha uhusiano wake na ibada na mapokeo ya Kifransisko, hasa ibada kwa Yesu Kristo na Bikira Maria.
Je kama unajua zaidi kuhusu Rozali hii tafadhali waseminari mtusaidie maarifa.
Tunaendelea sasa..
Mhe. Lissu: Ukiacha ya Mbeya unakumbuka nini kingine kuhusu madhira mengine?
Mnyika: Tarehe 06/02/2018 aliuwawa Mwanafunzi wa Chuo Akwilina Akwilimi kwa risasi katika tukio hilo ambalo Polisi walishambuliwa risasi tulibambikizwa kesi mimi na viongozi wengine 8 wa Chadema kwamba tumefanya ghasia na kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo.
Tarehe 10/03/2020 baada ya ushahidi wa uongo Mahakamani tukahukumiwa kifungo jela au faini ya milioni 300+ tulienda kuanza kutumikia kifungo na baadae watanzania wakatuchangia faini na kutoka.
Tulikata rufaa baada ya kuwa tumelipa ile faini na mwezi June 2021 Mahakama Kuu chini ya Jaji Mgeta ikatukuta kuwa hatuna hatia, ikatufutia hukumu hiyo kati ya mambo ambayo Jaji alisema juu ya mamlaka ya kuheshimu uhuru wa kisiasa na ukosoaji wa kisiasa hata kama utafanyika kwa kauli kali.
Na mpaka leo HATUJAWAHI KURUDISHIWA PESA ZETU MILIONI 300+ leo miaka zaidi ya minne.
Watu wanacheka 😂😂😂
Mhe. Lissu: Wenzako mlioshitakiwa nao ni akina nani?
Mnyika: Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mbowe, Katibu Mkuu Mashinji, Salum Mwalimu, Halima Mdee alikuwa Mwenyekiti wa BAWACHA, Esther Matiko na aliyekuwa Mwenyekiti Kanda ya Nyasa Peter Msigwa na Mjumbe wa Kamati Kuu John Heche.
Mhe. Lissu: Kesi zingine unazofahamu za kubambikiza za viongozi wa Chama?
Mnyika: Mwenyekiti wetu aliyepita Freeman Mbowe na Dr. Wilbroad Slaa walishtakiwa kwa kusababisha fujo ambazo zilisababisha kupigwa mabomu na vifo mwaka 2011 na 2012.
Mhe. Lissu: Hizo kesi ziliishaje?
Mnyika: Hawakuwahi kuhukumiwa na kesi zilikuja kufutwa baadae.
Mhe. Lissu: Kesi zingine?
Mnyika: Mwaka 2021 Mwenyekiti Freeman Mbowe nae pia alishitakiwa kwa kosa la Ugaidi kwamba alipanga kulipua vituo vya mafuta na matendo mengine ya kutishia serikali na usalama wa nchi.
Part 312 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 312
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mnyika : Matendo aliyotuhumiwa nayo hayajawahi kutokea na DPP alipeleka hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo na kesi ilifutwa na Mwenyekiti Mbowe alikutana na Rais Ikulu. Toka kuwa mtuhumiwa wa UGAIDI hadi MAPOKEZI IKULU.
Watu wanacheka.😂😂😂😂😂
Na Lissu anasema kwa kejeli kwamba na Mimi itakuwa hivyo hivyo?😂😂😂
Mhe. Lissu: Hayo makesi yote na hii yangu vina uhusiano gani?
Mnyika: Hizi kesi zote ni mwendelezo wa kupambana na Chadema kwa kutumia Mahakama kukwamisha mapambano ya kudai demokrasia ya kweli na mabadiliko katika mifumo ya Uchaguzi. Haya ni matumizi yasiyo ya haki dhidi ya wapinzani ambao ni CHADEMA kutoka kwa Chama dola ambao ni CCM. Lengo lao ni kukwamisha mabadiliko tunayohitaji. Hivyo huu ni mwendelezo wa mambo mabaya ambayo yamekuwa yakifanywa na hawa serikali dhalimu.
Anataka kusimama Ajuaye.
Mhe. Lissu: Subiri namaliza muda sio mrefu. Umenifahamu lini?
Mnyika: Toka 2003 tukiwa wote kwenye sekretarieti, baadae Kamati Kuu na Baadae Bungeni miaka 23 nakufahamu.
Mhe. Lissu: Huyu mtu ni mtu wa aina gani ambae umemfahamu kwa miaka 23?
Mnyika: Toka mwaka 2003 tulipoenda kule Kwembe, nimekufahamu kama mtaka mabadiliko, ni mtu mkweli ambae siku zote umekuwa ni mtu unayetaka mabadiliko. Mimi naamini MASHITAKA HAYA NI GHARAMA UNAYOLIPA KWA KUWA MKWELI NA KUTAKA MABADILIKO NDANI YA TAIFA HILI.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji nimemaliza kwa shahidi huyu.
Maneno aliyomalizia JOHN JOHN MNYIKA yamewafanya akina Mama waliopo humu MAHAKAMANI WATOE MACHOZI.
Yamekuwa ni maneno mazito sana na yenye ujumbe mzito, watu wamesikitika sana.🥹
Majaji wanaandika na kwa muda tulionao. Tutakwenda break na kurudi kwenye Cross Examination ya upande wa Jamhuri.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 313
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mahakama imerejea muda huu saa tisa kasoro alasiri.
Majaji wameingia tayari na Ajuaye Zengeli anasema wako tayari.
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika anapanda kizimbani.
Anasimama KATUGA anasema atakuwa na maswali machache labda kama wenzangu pia watakuwa nayo
Katuga: Nitakuwa na maswali machache na nafahamu wewe ni mkristu mwema. Kwa Cheo chako cha Katibu Mkuu ni mtendaji mkuu wa CHADEMA?
Mnyika: Ndio
Katuga: Chadema inaongozwa kwa sheria
Mnyika: Katiba, kanuni, Miongozo na Maamuzi ya Vikao.
Katuga: Katiba ni instruement muhimu na unaijua sana?
Mnyika: Naijua kwa kiasi cha Kutosha.
Katuga: Katiba yenu ni document inayopatikana iko public?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Katibu Mkuu anapatikanaje?
Mnyika: Anapendekezwa na Mwenyekiti wa Chama na anathibitishwa na Baraza Kuu.
Katuga: Mbona unatuchanganya?
Mnyika: Ndio nimekwambia anapendekezwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu sio kwamba nateuliwa na Mwenyekiti.
Katuga: Ibara ya 3(5) ya Katiba ya Chama inasema Chadema inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu?
Mnyika: Itabidi nirefresh sasa siwezi kujibu hivyo, nipewe nafasi.
Jaji Ndunguru: Haya angalia.
Mnyika: Ni sahihi Chadema inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi.
Katuga: Dhumuni Kuu ibara ya 4 ya Katiba ya Chama inasemaje?
Mnyika: Kuhakikisha Chama chetu kinashinda Chaguzi na kushika dola kwa njia ya Demokrasia.
Katuga: Kwa jinsi lilivyowekwa ndio kubwa kuliko yote?
Mnyika: Katiba ina madhumuni ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kushika dola sio dhumuni kuu na pekee.
Katuga: Kiwango chako cha Elimu ni kipi?
Mnyika: Ni kidato cha Sita.
Katuga: Huna uelewa wa Sheria?
Mnyika: Kwa vile sijapita law school unaweza kuniita layman.
Katuga: kwahiyo maoni yako ya kisheria unayabagaza tu?
Mnyika: Nina uzoefu wa miaka 23 wa siasa na utendaji na pia nimetunga sheria kwa miaka 10.
Mhe. Lissu: Haya mambo ya kumuuliza kuhusu maoni yake ya kisheria hakuna aliposema hivyo shahidi.
Majaji wanateta pale.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Katuga: Ulisema wewe ni afisa masurufi?
Mnyika: Masuhuli
Katuga: Wewe ndio custodian wa fedha zote za Chama.
Mnyika: Hapana.
Katuga: Kwani majukumu yako ni nini?
Mnyika: Kuidhinisha matumizi ya pesa na kupokea taarifa za fedha kadri zinavyoandaliwa na wahusika.
Katuga: Unahusika na pesa zetu za tonetone? Na unahusika na kuzipokea?
Mnyika: Mimi ni accounting officer na sipokei pesa.
Katuga: Kama Mdau ameipatia Makamu wa Rais pesa unazipokea wewe?
Mnyika: Chadema haina Makamu wa Rais.
Katuga: Nimekosea hapo.
Hivi wewe ndio unayelipa mishahara?
Mnyika: Mimi sio mlipaji wapo wanaolipa.
Katuga: Kwahiyo usipoidhinisha wewe wanalipwa?
Mnyika: Kwanza Chadema hatuna mishahara tuna posho tu.
Katuga: Usipoidhinisha wanapata:
Mnyika: Inategemea kama hizo pesa zipo. Zisipokuwepo hawawezi kupata chochote.
Katuga: Soma ibara ya nne pia
Mnyika: Kuthamini Demokrasia
Katuga: Kuna vyama havina mrengo wenu?
Mnyika: Sahihi
Katuga: Kuna vyama vingine haviamini katika No Reforms,No Election.
Mnyika: Siwezi kuvisemea.
Katuga: Vyama vingine vya siasa vina wanachama wake?
Mnyika: vyama vipi hivyo?
Katuga: Katiba ya Chama si inasema mnathamini uwepo wa vyama vya siasa. Kwenye hivyo vyama vingi kuna vyama ambavyo vina wanachama wake?
Mnyika: Siwezi kuvisemea vyama vingine ambavyo ni vya mfukoni tu, siwezi kuvijua kama kweli vina wanachama.
Katuga: Vyama vyenye usajili ni vingapi?
Mnyika: 19
Katuga: Vyama 18 vina wanachama wao na itikadi zao?
Mnyika: Siwezi kuvisemea.
Katuga: Ni kweli Chama cha siasa ili kisajiliwe lazima kiwe na wanachama?
Mnyika: Unaweza kuwa na Chama kikishasajiliwa wakahama au kuondoka. Lakini pia kwa mazingira ya sasa msajili anaweza kuvilinda vyama hewa hata kama havina wanachama. Inawezekana.
Part 314 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 314
Katuga anaendelea kumfanyia John Mnyika cross examination
Katuga: Ni kweli vyama hivyo vinaweza kuwa na Wanachama wake?
Mnyika: Siwezi kuwa na uhakika na wanachama wa vyama hivyo sina uhakika kama kweli vina wanachama.
Katuga: Hivyo vyama vingine pia vina itikadi yake?
Mnyika: Siwezi kuvisemea angalau ungeniuliza kuhusu Chadema, labda CCM na ACT ningweza kusema lolote.
Katuga: Mwanachama wa Chadema anapaswa kuheshimu Katiba?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Asiyefuata ni yule anayevunja Katiba ya Chadema?
Mnyika: Ni sahihi.
NB. KATUGA anamuuliza Mnyika kuwa ni form six. 😂 kila saa anaiulizia. Haoni hata aibu amekutana na shahidi form six lakini ana akili nyingi kuliko yeye na anamtesa vya kutosha.
Katuga: Si sawa kwa Mwanachadema yeyote kutokuamini anachokiamini mwanachama mwingine kwa itikadi yake?
Mnyika: Sasa sisi hatujasema tu habari ya vyama vingi kwa maana ya idadi.
Katuga: Kwahiyo mtu kupinga maoni ya vyama vingine ni kuvunja Katiba ya Chadema inayoamini vyama vingi?
Mnyika: Sio kweli maana upo uhuru wa maoni hata kupinga ni haki.
Katuga: Tarehe 03/04/2025 ulikuwepo kwenye Mkutano na nani alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo?
Mnyika: Hakukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano.
Katuga: Kwahiyo mkutano wa Chadema hakukuwa na mwenyekiti wa Mkutano.
Mnyika: Sahihi Kabisa, hatunaga mwenyekiti wa Mkutano.
Katuga: Uliwaambia mikutano ipo ya aina gani?
Mnyika: Aina kuu ni mbili yaani Mkutano wa Hadhara na Mikutano ya ndani.
Katuga: Mikutano ya ndani na hadhara kwa mujibu wa Katiba ikoje?
Mnyika: Hakuna aina za mikutano kwenye Katiba ni taratibu za kiutendaji tu.
Katuga: Kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama alikuwa na cheo gani?
Mnyika: Alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama.
Katuga: Huo Mkutano ulikuwa na maudhui gani? Na ulisema ulikuwa wa nani?
Mnyika: Ni Mkutano wa Chama na Mwenyekiti alikuwa Mzungumzaji Mkuu.
Katuga: Hiki Chama chetu kinapoitwa watia nia na Chama wanaenda kuongea na nani?
Mnyika: Watia nia wanaenda kuongea na Chama.
Katuga:Kwahiyo hawaendi kuongea na Mwenyekiti, Katibu, Naibu
Mnyika: Unaongea na Chama kupitia viongozi wakuu wa Chama.
Katuga: Uliwahi kuita waandishi wa habari na kusema mashahidi wa Jamhuri kuwa ni waongo?
Mnyika: Lissu sio muhaini nimewahi kusema mambo ya kuzungumzia kesi sijawahi.
Katuga: Unaposema Mwenyekiti wetu hana hatia na sio muhaini. Haya maoni yako unayatoa kwa mujibu wa ushahidi wa jamhuri au maoni yako?
Mnyika: Kwa mujibu ninavyomjua Mwenyekiti.
Katuga: Wewe ni mratibu wa vikao vyote vya Chama?
Mnyika: Sio kweli.
Katuga: Vikao vya Kamati Kuu unaratibu wewe?
Mnyika: Ndio ni mimi.
Katuga: Hiki cha juzi cha Tarehe. 29/08 ulikiita wewe?
Mnyika: Ndio ni mimi
Katuga: Mwenyekiti wa Kikao anakuwa ni nani?
Mnyika: Mwenyekiti wa Chama kama hayupo anakuwa makamu Mwenyekiti.
Katuga: Kile mlichojadili mlikitolea taarifa kwa umma.
Mnyika: Nafahamu ilitolewa kwa umma taarifa.
Katuga: Mlijadili hii kesi kwenye kikao?
Mnyika: Tulipokea taarifa ya kuwa Mwenyekiti amekutwa na hatia.
Katuga: Bado unasema kuwa Katibu Mkuu ndio mtendaji mkuu?
Mnyika: Ni sahihi.
Katuga: Ni sahihi wanaweza wakatenda au wakafanya utendaji bila Katibu Mkuu kujua?
Mnyika: Wanaweza katika maswala yakawaida ya kiutendaji.
Katuga: Umesema Mwenyekiti alipendekeza na kuthibitishwa na Kamati kuu?
Mnyika: Sio Kamati Kuu bali ni Baraza Kuu.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema wewe ni shahidi mwenye interest?
Mnyika: Nina Party interest na Public interest.
Katuga: Kwa hicho ulichokisema na umesema amekuteua. Nitakuwa sahihi nikisema wewe una maslahi?
Mnyika: Maslahi unayosema wewe sio maslahi niliyonayo mimi. Ukitaka kujua maslahi yangu mitakwambia.
Katuga: Ulisomewa yale mashitaka. Unajua aina ya uhaini alioshitakiwa nao mwenyekiti?
Mnyika: Uhaini wa kuitisha serikali kwa kuchapisha maneno.
Part 315 Itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 315
Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.
Katuga: Mwenyekiti Lissu ana utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mnyika: Sijui
Katuga: Yeye ni raia wa Tanzania.
Mnyika: Ndio
Katuga: Ulikuwa unaufuatilia Mkutano?
Mnyika: Upi?
Katuga: Huo wa tarehe 03
Mnyika: Sehemu kubwa niliufuatilia.
Katuga: Je watia nia wote walifika?
Mnyika: Sio wote ila siwezi kujua idadi ya waliofika.
Katuga: Madhumuni ya kuwaita watia nia ni yapi?
Mnyika: Kuwaeleza watia nia kama viongozi na wanachama kuwaonesha kwanini chama kilifikia msimamo wa No Reforms: No Election.
Katuga: Waliandika waraka wa kutaka kugombea?
Mnyika: Hapana, huo una maelezo yake.
Katuga: Aliyemualika Mwenyekiti wa Chama ni nani?
Mnyika: Alimpigia Amani Golugwa kumualika Mwenyekiti.
Katuga: Akimualika Mwenyekiti?
Mnyika: Alimualika Mwenyekiti na viongozi wengine.
Katuga: Ulisema tulimuandikia risala ya kuja kuzungumza?
Mnyika: Hilo sijasema.
Katuga: Je nyinyi sekretarieti ndio mliyemuandikia cha kwenda kuzungumza.
Mnyika: Msimamo huo ulishakuwepo zamani.
Katuga: Hamjamuandikia risala?
Mnyika: Mwenyekiti hatoi risala, Mwenyekiti anatoa hotuba inayoendana na maamuzi ya Chama.
Katuga: Kwahiyo unamsemea?
Mnyika: Namsemea kwasababu alichokisema ni msimamo wa Chama na alichokuwa anakisema pale ilikuwa ni kwa niaba ya Chama.
Katuga: Kwenye hiyo Hotuba ile sehemu ya kwamba majaji ni maccm uliisikia?
Mnyika: Sikusikia.
Katuga: Mapolisi wanaingia na vibegi vya kura?
Mnyika: Nilisikia
Katuga: Tutaenda kuzuia uchaguzi
Mnyika: Nilisikia
Katuga: Tutahamasisha uasi?
Mnyika: Nilisikia, hotuba nzima na alifafanua.
Katuga: Kama hiyo hotuba umeileta hapa Mahakamani?
Mnyika: Nimeileta kwa maelezo yangu ya mdomo.
Katuga: Katiba yetu ya Chadema inatambua Demokrasia ya Vyama vingi si ndio?
Mnyika: Ndio
Katuga: Uchaguzi Mkuu upo kisheria.
Mnyika: Uchaguzi mkuu halali.
Katuga: Uko timamu shahidi?
Mnyika: Wewe uko timamu?
Katuga: Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais upo kisheria?
Mnyika: Uchaguzi halali na wa haki upo kisheria.
Katuga: Uchaguzi wa wabunge madiwani na Rais upo kisheria?
Mnyika: Haupo muda wote. Bali unaitwa kwa mujibu wa sheria.
Katuga: Unajua Uchaguzi Mkuu uko Kikatiba?
Mnyika: Haupo bali umewekwa kwa mujibu wa Katiba.
Katibu Mkuu wetu Mnyika anagonga kwenye ugoko tu mpaka Mzee wa Multiple choice anavuja jasho wakati feni iko on.😂😂😂
Jaji Ndunguru kwahiyo umeuliza nini?
Mhe. Lissu: Swali limeulizwa na limejibiwa.
Katuga: Uchaguzi mkuu unaexist kwa mujibu wa Katiba?
Mnyika: Umewekwa kwa mujibu wa Katiba.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikasema kwakuwa uchaguzi huo upo kikatiba Una haki ya kuamini kuchaguliwa na kushiriki uchaguzi huo?
Mnyika: Ukiwa huru haki na halali.
Katuga: Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema mtu yeyote ana haki ya kushiriki kwa Chama chochote mbali na Chadema kushiriki uchaguzi wa haki na halali.
Mnyika: Kwenye uchaguzi wa haki na halali ana haki ya kushiriki.
KAZINI KWA KATUGA LEO KUNA KAZI. ANACHEKACHEKA TU.
Katuga: Kwahiyo haki anayo au hana?
Mnyika: Ukiitishwa uchaguzi huru na haki.
Katuga: Demokrasia ya Vyama vingi ni haki kwa mwanachama wa Chadema kuuzuia uchaguzi uliopo Kikatiba?
Mnyika: Katiba ya Chadema inatoa wajibu kwa wanachama kupambana na ukandamizaji wa kila aina ikiwemo uonevu. Kwahiyo ni Haki kwa Mwanachadema kupinga uchaguzi wa hovyo.
Katuga: Muasisi alikuwa Mbowe ulisema wa No Reforms: No Election?
Mnyika: Muasisi sio mtu ni kikao.
Katuga: No Reforms: No Election ulitafsiri vipi?
Mnyika: Bila Mabadiliko hakuna Uchaguzi.
Katuga: Kwenye hayo maneno kuna neno kwamba tutahamasisha uasi?
Mnyika: Hakuna hayo maneno ila huo uasi ni maana ya huo msimamo wetu.
Katuga: Ila ya nini tena?
Mnyika: Usikasirike sasa, mimi akupa maudhui
Mnyika leo kaamua kumpandisha Katuga kisukari mpaka amekasirika 😂😂😂😂😂
Part 316 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 316
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.
Katuga: Nimekusikia umesema mengi sana kuhusu Mwenyekiti.
Mnyika: Mengi yapi?
Katuga: Baadhi ya maneno.
Mnyika: Baadhi ya maneno ni sawa.
Katuga: Uliyarejea kwa kuyasikia au kuyaona?
Mnyika: Kwa sehemu kubwa niliyasikia.
Katuga: ushahidi wa maneno ni ushahidi wa kusikia au kuona?
Mnyika: Sifahamu. Ulishasema mimi ni layman wa sheria nitajuaje hizo aina za ushahidi?
Katuga: Mlipowaita waandishi wa habari mliwawekea kizuizi chochote?
Mnyika: Hatukuwawekea masharti.
Katuga: Chombo chochote kilichokuwa kina rusha kilifanya kosa?
Mnyika: Najuaje kuhusu makosa umesema mimi sio mwanasheria. Utajua wewe hayo mengine.
Katuga: Ni kweli kwamba mliwaita ili kuuhabarisha umma kwa maudhui mliyotaka kuyazungumza siku hiyo?
Mnyika: Ndio msimamo wa No Reforms: No Election.
Katuga: Mliwapa hotuba ya Mwenyekiti kabla?
Mnyika: Hatukuwapa.
Katuga: Mnapaswa kumueleza Mwenyekiti kuwa waandishi watakuwepo au hawatakuwepo?
Mnyika: Sio lazima ila siku hiyo tulieleza kuwa mkutano huo utakuwa na waandishi wa Habari.
Katuga: Ni kweli kwamba hawa waandishi wa habari kwa mara ya kwanza yale masaa matatu mlikuwa mmewashikilia?
Mnyika: Inategemea na tafsiri yako tu.
Katuga: Mwenyekiti anasema mliwatoa kwasababu hamkutaka part 2 iwafikie umma na wewe unasema hatukutaka kuwacontrol?
Mnyika: Ni kama hii chupa tu anaishika. Unaweza kusema half empty au half full ukawa unasema kitu kimoja. Inategemea na tafsiri yako tu.
Katuga: Unajua kwamba mshitakiwa kwa kutengeneza nia na kuchapisha maneno na kuutishia umma?
Mnyika: Ninachojua ni kuitishia serikali hilo la umma ni jipya kwangu.
Katuga: Ni kweli tuhuma ya kwamba aliyatoa maneno hayo?
Mnyika: Sema hayo maneno mahsusi sasa.
Katuga: Unajua kwamba anatuhumiwa kutoa maneno yale niliyosema?
Mnyika: Mimi sijui ninachojua ni kuchapisha.
Katuga: Kwa uzuri na kwa upole umethibitisha kuyasikia maneno niliyosema?
Mnyika: Maneno yapi?
Katuga: Kwa ushahidi wako unaithibitishia mahakama hii kwamba haya maneno umeyasikia ?
Mnyika: Niliyoyasema mimi ndio niliyasikia lakini sio yaliyopo kwenye hati ya mashitaka.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba mliita waaandishi wa habari wakati wanarekodi walikuwa wanaonekana au walitega camera kwa kificho?
Mnyika: Kulikuwa na camera zinaonekana.
Katuga: Ni kweli uliwaambia mliwaita waandishi ili warushe matangazo yenu?
Mnyika: Kwa uhuru wao wenyewe. Wanaweza kuchukua na wasirushe.
Katuga: Mliwapa tahadhari au hamkuwapa kwamba wasirushe au vipi?
Mnyika: Nilishajibu hilo swali tayari. Unasahau haraka sana.
Katuga: Nitakuwa sahihi publication kwa mujibu wa sheria ni nini?
Katuga: Tatizo umetishwa.
Mnyika: Unadhani wewe unavyotishwa serikali kila mtu anatishwa? Mimi nitishwe na nani? Unayetishwa ni wewe. Mimi nasema ninachojua hapa.
Katuga: Mliwatumia waandishi wa habari kusambaza taarifa zenu?
Mnyika: Hatukuwatumia bali tuliwaalika. Suala la kusambaza au kutosambaza ni maamuzi yao.
Katuga: Jambo TV ni chombo rafiki wa Chadema ilisemwa hapa Mahakamani?
Mnyika: Sijui
Part 317 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 317
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba kwa uhuru wao kukubali kusambaza taarifa hiyo ilifanya kazi mliyoitegemea? Jibu bila uoga.
Mnyika: Ondoa maneno ya uoga, sina uoga wowote.
Katuga: Kwahiyo walifanya kazi njema uliyowaitia.
Mnyika: Sijaiona hiyo kazi njema unayoisema.
Katuga: Huyo uliyemuita ameifanya hiyo kazi njema mliyoikusuduia?
Mnyika: Sijaiona hiyo kazi njema kwahiyo naweza kusema sio kweli kwamba ameifanya kazi njema.
Jaji Ndunguru anacheka kidogo. Ni kama anasema shahidi ana akili nyingi.
Anasimama Ajuaye anamnong'oneza Katuga.
Katuga anasema Majaji imefika saa 11 naomba tuendelee kesho nina maswali mengine zaidi, naomba tuahirishe.
Majaji wanaandika kidogo.
Mheshimiwa Lissu anamuita karani wanajadili jambo pale kizimbani.
Majaji wanamuuliza Mshitakiwa.
Mheshimiwa Lissu anasema sina pingamizi.
Jaji Ndunguru basi Tukutane kesho hakuna shida saa tatu asubuhi.
Inapigwa courtttttt watu wanasimama.
Majaji wanatoka.
Mwenyekiti anakusanya makablasha yake hapa, huku akiagana na Wanachama, Viongozi na Wafuasi waliofika Mahakamani siku ya leo.
Jioni njema kwenu.🫡
Naomba Repost yako.
Tanzania haihitaji hofu zaidi.
Inahitaji uponyaji.
Kwa sababu taifa lililojeruhiwa, mwishowe huanza kujijeruhi lenyewe.
Leo tunapaswa kusema ukweli
si kwa chuki,si kwa kisasi,bali kwa hofu ya kweli kuhusu mustakabali wa nchi yetu.
Kama Michael Jackson alivyowahi kusema:
“Tunapaswa kuponya dunia yetu iliyojeruhiwa. Machafuko, kukata tamaa, na uharibifu usio na maana tunaouona leo ni matokeo ya watu kujisikia wametengwa kutoka kwa wenzao na mazingira yao.”
Kauli hii kwa sasa
Inakuwa onyo hata kwetu sisi Watanzania, kama sehemu ya dunia
Wananchi wanapoanza kujisikia:
hawasikilizwi, wametengwa, wananyamazishwa, wanadhalilishwa,
au wanachukuliwa kama maadui kwa sababu tu wana mawazo tofauti.
umbali wa hatari huanza kujengwa kati ya wananchi na dola.
Na historia inatufundisha jambo moja la kuogopesha:
Mataifa mengi hayaanguki kwanza kwa sababu ya adui wa nje.
Huanzia kudhoofika ndani
wakati imani ya wananchi inapokufa.
Nchi haiwezi kujenga amani ya kudumu:
kama hofu inakuwa kubwa kuliko uhuru, kama utii unakuwa muhimu kuliko ukweli, kama taasisi zinaonekana kuwa za upande mmoja, au kama ukosoaji unatafsiriwa kama usaliti.
Kwa sababu jamii iliyojeruhiwa huzalisha wananchi walioumia.
Na wananchi walioumia mwishowe huzalisha:
hasira, mgawanyiko, msimamo mkali, kukata tamaa,au chuki ya kimya kimya.
Viongozi wanapaswa kuelewa:
si kila ukimya ni amani.
Wakati mwingine watu wananyamaza kwa sababu:
wamechoka,wanaogopa,au wamekata tamaa.
Na kukata tamaa ni hatari kwa taifa lolote.
Tanzania ilijengwa juu ya msingi imara ya : utu,umoja,mazungumzo,
uvumilivu,na hisia ya kuwa taifa ni la wote.
Julius Nyerere alielewa jambo kubwa sana,taifa haliishi kwa nguvu pekee (power)
linaishi pia kwa uhalali wa kimaadili.
Wananchi wakianza kuhisi kwamba:
haki inategemea upande wa kisiasa, ambao mtu yupo, taasisi si huru tena,
au demokrasia ipo kwenye maneno lakini si kwenye vitendo,
ule mkataba wa kihisia kati ya taifa na wananchi huanza kupasuka.
Kwa hiyo haya si mashambulizi.
Hili ni onyo.
Onyo kwamba:
siasa zinapokuwa za uhasama kupita kiasi,
mamlaka zinapoanza kuogopa ukosoaji,
wapinzani wanapoonekana maadui,
na wananchi wanapopoteza imani kwa mifumo ya taifa
taifa lenyewe huanza kujeruhiwa kihisia.
Na taifa lililojeruhiwa huwa taifa lisilo tulivu.
Hatuhitaji kulewa kisiasa zaidi.
Tunahitaji hekima.
Hatuhitaji viongozi wanaotaka kusifiwa tu.
Tunahitaji viongozi wenye uwezo wa kusikiliza ukweli usiofurahisha.
Kwa sababu uzalendo si ukimya.
Wakati mwingine uzalendo ni ujasiri wa kusema:
“Kuna jambo linaenda vibaya kabla hatujachelewa.”
Kama Tanzania inataka kubaki imara,
basi uponyaji lazima uwe sera ya taifa.
Uponyaji:
kati ya viongozi na wananchi,kati ya dola na upinzani,kati ya mamlaka na uwajibikaji,kati ya sheria na haki.
Kwa sababu hakuna taifa linaloweza kuishi milele kwa:
hofu, propaganda,au mgawanyiko wa kihisia.
Mwisho wa yote,
taifa huwa imara zaidi pale wananchi wake wanapoamini kwamba:
wao ni sehemu ya taifa,wanalindwa,
wanasikilizwa,na utu wao una thamani.
Mungu ailinde Tanzania isije kuwa nchi ambayo wananchi wanaogopana kuliko kuaminiana.
Na viongozi wetu wakumbuke:
historia haitawahukumu viongozi kwa barabara, madarasa , vituo vya afya walivyojenga pekee,
bali pia watahukumiwa kwa hali ya kihisia walizoliachia taifa.
Usisahau:
“Jamii iliyojeruhiwa huzaa watu waliojeruhiwa…
na watu waliojeruhiwa huongeza machafuko zaidi.”
Rev Petet simon Msigwa!
Iringa