Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mch. Peter Saimon Msigwa amemtaja Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa kama rafiki yake wa karibu, akisema wakati walipokutana Mahakamani ilikuwa ni maumivu makubwa kwake, machozi yakimlenga kwa furaha ya ujasiri aliouona kwa Mwenyekiti huyo licha ya kuwa Magereza kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Amezungumzia pia kutetereka kwa mahusiano yao pale alipokihama Chama cha Chadema na kwenda Chama Cha Mapinduzi, akisema wakati akiwa CCM alisafiri usiku mnene kwenda Arusha kukutana na Lissu na kuzungumza nae kuhusu uamuzi wake wa kwenda Chama Cha Mapinduzi CCM.
"Wengi wa marafiki zangu kama akina Lema, Heche na baadhi ya wengine hatukuwahi kupoteza mawasiliano na hawakunihesabu kama msaliti bali walinichukulia kana mtu aliyepata ajali ya kisiasa na nirudie sikuondoka kwasababu ya fedha, niliondoka Chadema si kwasababu nilikuwa naichukia." Amesema Mch Msigwa katika mahojiano yake na Mwandishi wa JamboTv Mjini Iringa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Ndg. John Heche amezungumza na watanzania jioni ya Tarehe 11 July 2026 nyumbani kwake Tarime mjini ambapo amawashukuru kwa simu na jumbe za pole.
Hivi karibuni kiongozi huyo alifiwa na aliyekuwa Dereva wake marehemu Suez Maradufu ambaye Heche amesema amekuwa karibu na marehemu Suez tangu akiwa shuleni na akiwa miaka 16 marehemu Suez alikuwa ni Dereva wa Baba yake.
Heche ameongeza kuwa sio rahisi kujibu jumbe na simu ya kila mtu, kila kiongozi, kila mtanzania ndio maana ameamua kwa pamoja kujibu pole hizo.
Katika hatua nyingine Heche amebainisha kupokea simu nyingi kutoka kwa wanachama wa Chadema na watanzania kwa ujumla wanaotaka kumtumia fedha i kumpa pole na kumtia moyo kama Kiongozi wa Chadema, akiomba wote walioguswa na harakati zake kutuma fedha hizo kwenye akaunti za Chadema ili kusaidia katika maandalizi ya Mkutano mkuu wa chadema unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
"Kamati Kuu imeazimia kuwa CHADEMA iendelee kwa nguvu kubwa na operesheni ya Katiba Mpya #FreeTundu Lissu katika Kanda za Pwani, Unguja na Pemba na awamu nyingine, Operesheni itaendelea mikoa yote ya Tanzania." Mhe. @jjmnyika
Mlemavu akienda kuchangia tonetone katika chombo alichoshika Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 John Heche @HecheJohn ambapo baada ya kupiga picha hiyo alipata nafasi ya kupiga picha na Heche.
CHADEMA imeendelea na mikutano yake ya hadhara kama sehemu ya Operesheni Katiba Mpya, Free Tundu Lissu huku ikiomba kuungwa mkono na wananchi.
Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. @HecheJohn akizungumza katika mkutano wa hadhara wa operesheni #KatibaMpya#FreeTunduLissu uliofanyika Njombe Mjini leo tarehe 21 Juni 2026. Mkutano huo umefanyika leo mchana na jioni ya leo utafanyika mkutano mwingine Makambako.
Haya magari na hawa watu wanaokuja kwenye mikutano yetu kwa njia za kufuatilia kwa njia zisizo za wazi..
Wanapaswa kujua Tunajua na tunawaona.
Sisi tunafanya siasa na tunafanya kazi yetu ya kikatiba, hatuwezi kukubali kutishiwa wala kuogopeshwa.
Acheni uhuni huu.
Ushuru wa Mabango ya Matangazo kwa sheria yetu yanalipiwa, kwa kila mita square ni zaidi ya 7,000…
Kuna Mabango ya kampeini za Samia kwenye kila Halmashauri ya Nchi hii.
Tunataka kujua fedha ambazo zimelipwa na ccm kuendelea kuweka Mabango ya uchaguzi katika maeneo ya umma.
Matukio ya mauaji, vurugu na umwagaji damu yanapotokea katika jamii, athari zake haziishii kwa waliopoteza maisha pekee. Mara nyingi huacha majeraha makubwa ya kisaikolojia kwa walioshuhudia, walionusurika, familia za waathirika, na hata wale waliohusika moja kwa moja katika matukio hayo.
Wataalamu wa afya ya akili hali hii huiita PTSD (Kiwewe cha Kisaikolojia Baada ya Tukio la Kutisha). Mtu anaweza kuendelea kuishi kwa miaka mingi baada ya tukio, lakini kumbukumbu za siku hiyo zikawa zinaendelea kumwandama.
Dalili zake zinaweza kuwa ndoto za kutisha, hofu ya mara kwa mara, kushtuka kwa sauti ndogo, kukosa usingizi, kujitenga na watu, hasira zisizo za kawaida, au kuona picha za tukio zikijirudia akilini kana kwamba linatokea tena.
Wakati mwingine hata wale waliopewa jukumu la kutekeleza amri katika mazingira ya vurugu wanaweza kubeba majeraha ya ndani yasiyoonekana. Wanaweza kuonekana wenye nguvu nje, lakini ndani wakiteswa na hatia, maswali ya dhamiri, huzuni au kumbukumbu zinazowatesa usiku na mchana.
Historia duniani imeonyesha kwamba baada ya matukio makubwa ya umwagaji damu, baadhi ya walionusurika, mashahidi na hata baadhi ya wahusika wamehitaji msaada wa kisaikolojia, kijamii na kiroho ili kurejesha utulivu wa nafsi zao.
Majeraha ya mwili yanaweza kuonekana na kutibiwa kwa haraka, lakini majeraha ya akili na dhamiri mara nyingi huchukua muda mrefu zaidi kupona. Ndiyo maana uponyaji wa taifa baada ya matukio ya vurugu hauhusishi haki pekee, bali pia ukweli, maridhiano, na huduma za afya ya akili kwa wale walioathirika.
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu ameonesha kusikitishwa na 'ukimya' wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kufuatia tukio la 'kutekwa' na kutoweka kwenye mazingira tatanishi kwa aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Malawi na Cuba Humphrey Polepole ambaye hadi sasa haijulikani alipo
Akizungumza kwenye hafla ya ACT Wazalendo mahsusi kwaajili ya kuwapokea vijana Wasomi wa Vyuo mbalimbali waliojiunga na chama hicho, Ado amesema awali alitarajia pengine Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro angejitokeza kulaani tukio hilo, hasa ikizingatiwa kuwa Polepole sio tu kwamba amekuwa Kada wa CCM bali pia amewahi kuhudumu kama Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa chama hicho Taifa, Mkuu wa Wilaya, Mbunge na Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa inaongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewasili mkoani Iringa kutoa pole kwa familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Iringa, Ibrahimu Myovela, pamoja na familia za wenzake wawili Antony Mwasika na Ally Kalolo, ambao wanadaiwa kupotea wakiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Heche alifika nyumbani kwa wazazi wa Ibrahimu Myovela na kutoa salamu za pole kwa niaba ya chama hicho, huku akiihakikishia familia kuwa CHADEMA itaendelea kusimama pamoja nao katika kuhakikisha vijana hao wanapatikana na kurejeshwa salama kwa familia zao.
Katika mazungumzo yake, Heche aliwataka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana kuwatafuta vijana hao na kutoa taarifa sahihi kwa umma, akisisitiza kuwa mazingira ya kutoweka kwao yanadaiwa kuhusishwa na jeshi la polisi baada ya kushikiliwa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 10, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, vijana hao wanatuhumiwa kuhusika katika tukio la kujeruhi lililosababisha kifo .
Taarifa hiyo ya polisi inaeleza kuwa baada ya tukio hilo, Ibrahimu Myovela na wenzake walidaiwa kutoroka huku jeshi la polisi likisema linaendelea kuwatafuta kwa tuhuma za mauaji.
Tumewaonya sana mkatuita wachochezi!
Vijana wa #Tanzania wamechoka na wamewachokeni madhulmat! Kutwa mnawakamata mnawatesa
Wao wako mamilioni - wakigundua kuwa wao ni wengi kuliko ninyi mnafikiri mwisho wenu utakuwa mzuri?
Leo Arusha mmeonja joto la jiwe @tanpol na watekaji! Acheni huu upumbavu wa kamatakamata! Mnapeleka nchi kubaya!
Sitachoka kuwatahadharisha! Hivi kuna mwenye akili na ujasiri kwenye mfumo anayeweza kusimamisha huu uendawazimu?
#TutaelewanaTu
Young man resists brutal illegal arrest/ abduction and others stand up to police brutality in Arusha today! Tanzania is headed down a disastrous path with Samia Suluhu - a complete collapse of rule of law and the economy! Hear ye! Hear ye!
That is why #SamiaMustGo
“Let the oil flow; Acha mafuta yatiririke!”
Rais wa Marekani Donald Trump kupitia ukurasa wake wa TRUTH SOCIAL ametangaza rasmi kwamba Serikali ya Marekani imefikia na kukamilisha makubaliano au mkataba maalum wa amani/kibiashara na Jamhuri ya Kiislam ya IRAN.
Lango la Hormuz (Strait of Hormuz) ni njia kuu na muhimu majini duniani kwa ajili ya usafirishaji wa mafuta ghafi. Kutokana na mkataba huu, Trump ameruhusu njia hiyo ifunguliwe ili meli zipite bila kutozwa ushuru au vikwazo (toll free).
Jeshi la Majini la Marekani lilikuwa limeweka Kizuizi cha Kijeshi (Naval Blockade) katika eneo hilo kudhibiti mienendo ya Iran. Kupitia amri hii, Trump ameamuru kizuizi hicho dhibiti kiondolewe mara moja ili kuruhusu uhuru wa meli kupita.
Kauli yake ya “Meli za Ulimwengu, washeni injini zenu. Acha mafuta yatiririke!” inaashiria kufunguliwa upya kwa biashara ya kimataifa ya mafuta ambayo ilikuwa imekwama au kuwekewa vikwazo vikali kutokana na migogoro kati ya nchi hizo.
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif amethibitisha kupitia ukurasa wake wa 𝕏 akisema “Tunafurahi kutangaza Makubaliano ya Amani kati ya Muungano wa Madola ya Amerika (Marekani) na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamefikiwa.”
Shehbaz Sharif anasema “Pande zote mbili zimetangaza kusitishwa mara moja na kwa kudumu kwa operesheni za kijeshi katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na nchini Lebanon. Sherehe rasmi ya utiaji saini itakuwa Ijumaa, Juni 19 nchini Uswisi.”
Pamoja na habari njema ya kushuka kwa Brent Crude kwa zaidi ya 3.8% na hiyo dili ya amani na kibiashara kati ya MAREKANI na IRAN, kuna ukuta wa kiuhalisia unaoweza kuzuia bei ya mafuta isishuke kwa kiwango ambacho watu wengi wanatarajia kukiona.
Mafuta yatakayotumika mwezi August nchini Tanzania hayatanunuliwa kwa bei ya leo katika soko la dunia. Kupitia mfumo wa (Bulk Procurement System - BPS), mafuta yanayotumika mwezi June yaliagizwa na kulipiwa miezi mitatu iliyopita.
Hii ina maana kwamba faida ya kushuka kwa bei ya mafuta leo katika soko la Dunia tutaanza kuiona katika bei za pampu labda Oktoba. Ndiyo maana nasema hii ni biashara ya CARTELS. Wahuni Wametengeneza ‘makorokocho’ wapige dili.
Bei ya mafuta katika pampu Tanzania haitegemei bei ya Brent Crude pekee katika soko la Dunia. Bei katika pampu inategemea zaidi bei ya mafuta yaliyosafishwa (Platts) pamoja na gharama za usafirishaji wa meli, bima, na faida ya muagizaji.
Hata kama bei ya pipa (barrels) inashuka, kama gharama za meli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam, Tanga au Mtwara ziko juu (kwa sababu ya changamoto watakazoeleza), EWURA watatumia gharama kubwa kupiga hesabu zao.
Halafu, uzoefu wetu na Serikali hii dhalimu ya CCM unatueleza, mafuta yakishuka katika soko la Dunia kwa 20%, pampu ya Tanzania inaweza kushuka kwa 3% hadi 5% tu, huku visingizio vya kupanda kwa dola na gharama za meli zikitolewa kama utetezi.
Hii bei ya mafuta Tanzania tunaweza kuishi nayo miaka mitano ijayo. Ni biashara ya CARTELS. Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa Ratchet Effect. Bei za vitu huwa ni rahisi kupanda lakini ni ngumu sana (sticky downwards) kushuka. EWURA wanaitumia
Bei ya mafuta ilivyopanda kwa kisingizio cha vita ya Russia – Ukraine haikuwahi kushuka tena. Serikali ya awamu ya sita (2021) wamekuta bei ya lita moja ya mafuta ni Tsh. 1,887 sasa hivi lita moja ya mafuta wameifikisha Tsh. 4,086 na HAITASHUKA.
Wafanyabiashara wakubwa wa kuagiza mafuta (CARTELS) na serikali yenyewe wakishazoea kupata mapato makubwa katika kiwango fulani cha bei, wanaamua kutengeneza mazingira ya kulinda hicho kiwango kisirudi chini kwa njia za “kihalali”
Kutoka Tsh. 1,887 (2021) hadi Tsh. 4,086 (2026) ni ongezeko la zaidi ya 110%. Ongezeko la zaidi ya 110% ndani ya miaka michache tu ni pigo kubwa kwa uchumi wa kaya na biashara. Lakini unafikiri Serikali hii katili na haramu ya CCM wao wanajali?
Ni wazi ‘wese’ kuwa juu ya Tsh. 4,000 sasa ndio msingi mpya wa maisha yetu ya kila siku (new norm), na madhara yake ndio haya tunayaona kwenye nauli na bei ya vyakula kila kukicha. CCM hawajawahi kumhurumia Mtanzania wa kawaida.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.