Usifurahie kumfanyia mtu ubaya, wala usimwombee mabaya. Kumbuka, Mungu huangalia matendo na nia za moyo. Usimwangushe mwingine ili uinuke; baraka za mwenzako si laana kwako. Kila kitu cha dunia hupita, hivyo mtendee mema kila mtu na umwachie Mungu yaliyo nje ya uwezo wako🙏🏽.
Ninaamini yupo. Uumbaji wangu, uwepo wangu hata leo ni neema na rehema zake katika maisha yangu. Kila ninachopitia katika maisha yangu, ni namna ya kutengenezwa kwangu. Hata nisipoelewa kila jambo linalotokea, sitaruhusu hali yangu yoyote izime imani yangu kwake. Mungu yupo🙏🏾.
Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.
Isaya 6:5
Hii ni dunia, ina utaalam sana wa kupandisha na kushusha vyeo.
Ni heri ukawe mnyenyekevu ili siku ukishuka asiwepo wa kukunyooshea kidole.
Wakati ni ukuta, hata uwe mzuri wa namna gani, kuna wakati utaisha soko.
Mungu atusaidie sana.
Sipaswi kuruhusu hofu yangu ya kifo kuzidi hofu yangu ya dhambi.
Naweza kufa mara moja tu kwa mwili, lakini mimi hufa milele ninapoing'ang'ania dhambi.
Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
1 Yohana 4:18
Ukifikiri kwa kina utagundua ulipokaa alikuwepo mwingine kabla yako!!
Mungu humwinua yeyote wakati wowote. Usidharau mtu!!
Mara nyingi Mungu hutumia watu dhaifu kujitukuza!!
#Haki_ni_kwa_kila_mtu__Sifa_ni_TOBA
Kuwa makini sana, maana #URAFIKI na #UNAFIKI vinatofautiana kwa herufi moja tu!!
Mpe nafasi ajione mshindi🙌, chukua muda kujijenga upya🙏.
#Vina_Muda_basiiii
Daima uwe tayari kuishi peke yako, watu wengine hubadilika ghafla, leo wewe ni muhimu kwao kesho sio kitu kwao, na hayo ni maisha halisi.
#Maisha_Halisi
Ukiumia na ukataka kulia, lia kadili unavyotaka, lakini hakikisha kuwa wakati utakaponyamaza kulia, kamwe hutolia kwa sababu ileile iliyokiliza mwanzo!!
#Mzani_wa_maisha
@Baraka__Mpenja Mpenja Adson Baraka, utajuwa wewe nimebadili lipi kikubwa nikupe maua yako mtu boooooooooraaaaaa kabisa.
Jana umeitangaza mechi kwa viwango vya kimataifa kabisa kuanzia mwanzo hadi mwisho, Respect sana Mwamba wa Umalila❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥
Usimuamini kila mtu, maisha yamejaa watu fake ambao wanajifanya kujali, lakini pale unapowahitaji zaidi hawapatikani, inauma lakini wanakufundisha kujiamini mwenyewe ambapo itaweka moyo wako salama katika maisha.
Ni vigumu kuvumilia maumivu, lakini ni rahisi kusababisha maumivu
Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.
#Hosea 10:12
Hata uwe na macho mazima kiasi gani, yana ukomo wa umbali wa kuona, iwe ni tambarare au juu ya kilima, huwezi kuona kila kitu!
#Kila_jambo_lina_wakati_wake